Wanaharakati wa Tanzania na kasumba sugu

Wanaharakati wa Tanzania na kasumba sugu

Nyie mpaka da...m imwagike ndio mtaacha hizi kejeli.

Tukianza kutendeana inavyostahili na kila mmoja akaonja machungu ya tunachokitafuta, hizi kejeli na dharau ndipo vitakoma.

Ziko njia nyingi tu za kufanya kiupande uonje ladha ya matendo mnayotendea wengine na kisha kuwakejeli.

Tema mate chini, mara zote hasira hasara.... Unapenda damu imwagike eehhh [emoji48][emoji48] anza kuimwaga mkuu
 
Ungekuwa na akili ungeoneksha kuwa ni njia ipi sisi kama wapinzani wa ccm tuitumie lakin kwa kuwa huna umeishia kutaja na tena sio kuelezea ya unataja afu unajitia unatoa conclusion.Unabariki unfairness kwenye nchi? Siasa za majitaka za ccm zina mwisho na watatoka kwa njia yoyote ile wakati utakapowadia
 
Siasa ulizong'ang'ania zimepitwa na wakati. Zama hizi watu wanataka siasa fikirishi. Tangu mwaka 2005 mmebeba siasa za namna ile ile hakuna ubunifu. Siasa za kulaumu laumu na kutukana ni za kishamba. If you don't change, situation will change you.
Hii nimeipenda sana! Naona wananchi pia wamechoka kabisa na siasa zao, sasa wanawanyoosha tu kwenye sanduku. #SiasaZaKishamba zilizojaa matusi na kejeli
 
Tema mate chini, mara zote hasira hasara.... Unapenda damu imwagike eehhh [emoji48][emoji48] anza kuimwaga mkuu
Kama hampendi damu imwagike wekeni usawa na acheni demokrasia ifanye kaze kazi yake.Nje ya hapo damu itamwagika tena na tena kama inavyoendelea kumwagika itamwagika zaidi na zaidi na itakaa juu yenu na juu ya vizazi vyenu vyote
 
Huyo carol ndosi hamna kitu kabisa, nakumbuka alileta bandiko lake leefu humu akiamini watu wataandamana 26/4. Mwisho wa siku akaumbuka
Lina mantiki na bandiko lake you can't know one oneday bandiko lake likamwonesha ushujaa wake.ndio maana yule DC mchumba wa kisarawe uchafu wake ulianikwa alionika mwenyewe huko nyuma akijua ataendelea kuwa kama alivyo
 
Kama hampendi damu imwagike wekeni usawa na acheni demokrasia ifanye kaze kazi yake.Nje ya hapo damu itamwagika tena na tena kama inavyoendelea kumwagika itamwagika zaidi na zaidi na itakaa juu yenu na juu ya vizazi vyenu vyote
Acha kujitenga kuwa damu itakaa juu yetu, na nani wakati we ndio waombea mabaya....
 
Wanabodi,

Wanaharakati wetu wengi wana tabia hizi kwa uchache na unaweza kuongezea zako;

1) Wanaamini uanaharakati maana yake kuunga mkono upinzani

2) Hawana ajenda zaidi ya kubeba vilio vya wanasiasa hasa wa upinzani(fatilia walivyo sharp kukosoa hotuba/hoja za viongozi wa chama tawala lakini huo uharaka wa kukosoa/kuhoji haupo akiongea kiongozi wa upinzani.

3) Hawana vitu wanavyosimamia/kuamini bila kuyumbishwa na upepo. Mfano akitoa hoja ya kuwapiga Chadema baadae lazima atafute hoja ya kuipiga CCM ili abakie relevant na kuonekana "kamanda"

4) Hakuna mwanaharakati ambaye kwa nguvu ile ile wanayoitumia kuikosoa CCM na serikali anaweza kuikosoa Chadema au upinzani kwa ujumla zaidi ya mafumbo ili kuonesha hawana upande.

Kwa ujumla, Wanaharakati mnayo fursa nzuri ya kuaminiwa na wananchi kwasababu mbalimbali. Tumieni ushawishi wenu kueleza ukweli ili kusaidia kuimarisha demokrasia. Unafiki na kutokuelezana ukweli kwa wazi imetugharimu uchaguzi wa 2015 na matokeo yake yanaendelea sasa.

Sasa hivi mpo tena kwenye mtego wa kuishambulia CCM kununua wapinzani bila kutumia nguvu hiyo hiyo kuhoji namna upinzani wanavyoshughulika na hili badala ya kulialia.

Mmeanza kuaminisha umma kuwa wasitegemee wanasiasa kutuletea mabadiliko wakati wao kikatiba ndio wawakilishi wetu. Hawataki kusema ukweli juu ya udhaifu wa upinzani ambao wanategemea CCM wawape ikulu!! Hivi wangekuwa Rwanda wangesimamisha hata mgombea wa udiwani kwa kulialia huku?

Tunashindwa kuhoji chama kikuu cha upinzani kuachia kata 41 CCM kupita bila kupingwa! Tutapakana mafuta hadi lini? Tunahitaji uelekeo mpya wa upinzani ambao utaaminika na wananchi na kuwa tayari kwa lolote.

Kesi, vipigo vya polisi na harassment si vitu vipya kulalamikiwa na upinzani. Nafikiri ipo haja ya kuwapa takwimu ya kesi na vipigo huko nyuma ili tuache kutafuta chaka la kumtupia kila zigo JPM. Kama kuna kigugumizi cha kupata viongozi wapya wenye uwezo kutupa kasi mpya against CCM basi ikulu ni ndoto.

Kazi yenu nzuri kuikosoa CCM mngeifanya kwa nguvu hiyo hiyo vyama vyote hasa vyama vikubwa mngesaidia sana siasa zetu. Otherwise endeleeni kuikosoa CCM ili izidi kuwa bora na endeleeni kupotezea ya upande wa pili wabakie kuwa wapinzani wa kudumu.
CCM kama kweli mnakubalika......

kwa nini mumuue yule binti masikini Aquiline?

au kwa nini mumtwange risasi Lissu?

au kumpoteza Ben Saanane?

kwa nini mnatumia polisi badala ya hoja lakini?

kwa nini m/kiti wa chama chenu awatishie kuwafukuza kazi wakurugenzi watakaowatangaza wapinzani wameshinda uchaguzi?

ni mimi mwanaharakati.
 
Tatizo hampendi facts ....ningeandika Chadema yazidi kuimarika nikula likes buku ...
Mzee wa MTAZAMO na MITAZAMO dhaifu, mtazamo wako dhaifu sana ( kwa mtazamo wangu) hukubaliani na facts yeyote juu ya udhaifu,ubabe,ufujaji, u-Dikteta wala BIASHARA ya Bin-ADAMU Iliyozuka.
Kisa wamsapoti jiwe kibwegebwege TU.
 
Siasa ulizong'ang'ania zimepitwa na wakati. Zama hizi watu wanataka siasa fikirishi. Tangu mwaka 2005 mmebeba siasa za namna ile ile hakuna ubunifu. Siasa za kulaumu laumu na kutukana ni za kishamba. If you don't change, situation will change you.
Za kibabe ni za KISHUA?, kweli Annah ni HANA.
 
Acha kujitenga kuwa damu itakaa juu yetu, na nani wakati we ndio waombea mabaya....
Sio naombea mabaya mkuu.La hasha point yangu ni kwamba kukosekana kwa usawa kwenye hii nchi kutasababisha damu kumwagika.Na hii ni principle kwa kuwa sehem zote damu ilipomwagika sababu ni unfairness.Na awamu hii unfairness ni kubwa sanaa.Imezidi kipimo
 
Mzee wa MTAZAMO na MITAZAMO dhaifu, mtazamo wako dhaifu sana ( kwa mtazamo wangu) hukubaliani na facts yeyote juu ya udhaifu,ubabe,ufujaji, u-Dikteta wala BIASHARA ya Bin-ADAMU Iliyozuka.
Kisa wamsapoti jiwe kibwegebwege TU.
Wewe utakuwa Rapper naona umeshuka vina vinavyokinzana ....🤣🤣
 
Lema ni mtu wa ajabu sana habari za kuambiwa na yeye anazisukuma live kwenye vyombo vya habari.
 
Magezi,

..kwanini tufike huko kwenye kuumizana?

..mbona ni rahisi zaidi kupambana kwa hoja?

..na siyo kwamba ccm haina wajenga hoja.

..napinga matumizi ya nguvu ktk siasa.
 
Mkuu mtazamo, wakati wa uchaguzi 2015 wana usalama waliwakagua hawa wanaharakati kwenye ofisi zao. Walikuwa wanacheza mchezo mchafu ili nchi iingie mikononi mwa wapigaji.

Wakasahau kuwa hii nchi kwanza iliwekwa nchi ya nguvu za kiasili kupitia wazee wa Dar. Halafu pia nchi ikawekwa mikononi mwa nguvu za Mungu kupitia makanisa. Nchi hii inao ulinzi wa kiroho ndio maana inaishinda mitihani mingi inayoanzishwa na watu wenye ubinafsi waliozoea kufaidika na jasho la wanyonge.

Hawa wanaharakati wanapoteza muda kwenye awamu hii, kinachopangwa ndicho kinachotekelezwa, watu wanapiga kazi.
 
Kama hampendi damu imwagike wekeni usawa na acheni demokrasia ifanye kaze kazi yake.Nje ya hapo damu itamwagika tena na tena kama inavyoendelea kumwagika itamwagika zaidi na zaidi na itakaa juu yenu na juu ya vizazi vyenu vyote
Sio naombea mabaya mkuu.La hasha point yangu ni kwamba kukosekana kwa usawa kwenye hii nchi kutasababisha damu kumwagika.Na hii ni principle kwa kuwa sehem zote damu ilipomwagika sababu ni unfairness.Na awamu hii unfairness ni kubwa sanaa.Imezidi kipimo
Angalia post yako ya juu,, "Kama hampendi damu imwagike" hapo unamaanisha nn [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Angalia post yako ya juu,, "Kama hampendi damu imwagike" hapo unamaanisha nn [emoji16][emoji16][emoji16]
Mbona ipo sawa mkuu yaani kama ccm hawataki damu imwagike waweke usawa kwa wote.wasipofanya hivo wajue damu itamwagika na wao ndio watasababisha.kwa mfano ukiongea kwa kiburi ukilenga sehem fulani ta watu wa jamii.sisi tuna polis tuna mahakama hawana cha kutufanya. Sasa haponunaonesha unfairness then watu wanaanza kuchukua sheria mkononi.kauli mkuu zina nguvu balaa.Wajitahidi wawaache wapinzani wafanye yao maana wao wanakubalika kama wanavyojinasibu kwa media.
 
Tatizo hampendi facts ....ningeandika Chadema yazidi kuimarika nikula likes buku ...

Bila kupinga hili andiko lako kwani naona kuna facts fulani fulani na ninaziheshimu. Hili bandiko lako umeliweka kama mtu huru ama una upande?
 
Bila kupinga hili andiko lako kwani naona kuna facts fulani fulani na ninaziheshimu. Hili bandiko lako umeliweka kama mtu huru ama una upande?
Mkuu always nipo huru ..
 
Back
Top Bottom