Wanaharakati wa Tanzania na kasumba sugu

MTAZAMO

Platinum Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
20,166
Reaction score
35,730
Wanabodi,

Wanaharakati wetu wengi wana tabia hizi kwa uchache na unaweza kuongezea zako;

1) Wanaamini uanaharakati maana yake kuunga mkono upinzani

2) Hawana ajenda zaidi ya kubeba vilio vya wanasiasa hasa wa upinzani(fatilia walivyo sharp kukosoa hotuba/hoja za viongozi wa chama tawala lakini huo uharaka wa kukosoa/kuhoji haupo akiongea kiongozi wa upinzani.

3) Hawana vitu wanavyosimamia/kuamini bila kuyumbishwa na upepo. Mfano akitoa hoja ya kuwapiga Chadema baadae lazima atafute hoja ya kuipiga CCM ili abakie relevant na kuonekana "kamanda"

4) Hakuna mwanaharakati ambaye kwa nguvu ile ile wanayoitumia kuikosoa CCM na serikali anaweza kuikosoa Chadema au upinzani kwa ujumla zaidi ya mafumbo ili kuonesha hawana upande.

Kwa ujumla, Wanaharakati mnayo fursa nzuri ya kuaminiwa na wananchi kwasababu mbalimbali. Tumieni ushawishi wenu kueleza ukweli ili kusaidia kuimarisha demokrasia. Unafiki na kutokuelezana ukweli kwa wazi imetugharimu uchaguzi wa 2015 na matokeo yake yanaendelea sasa.

Sasa hivi mpo tena kwenye mtego wa kuishambulia CCM kununua wapinzani bila kutumia nguvu hiyo hiyo kuhoji namna upinzani wanavyoshughulika na hili badala ya kulialia.

Mmeanza kuaminisha umma kuwa wasitegemee wanasiasa kutuletea mabadiliko wakati wao kikatiba ndio wawakilishi wetu. Hawataki kusema ukweli juu ya udhaifu wa upinzani ambao wanategemea CCM wawape ikulu!! Hivi wangekuwa Rwanda wangesimamisha hata mgombea wa udiwani kwa kulialia huku?

Tunashindwa kuhoji chama kikuu cha upinzani kuachia kata 41 CCM kupita bila kupingwa! Tutapakana mafuta hadi lini? Tunahitaji uelekeo mpya wa upinzani ambao utaaminika na wananchi na kuwa tayari kwa lolote.

Kesi, vipigo vya polisi na harassment si vitu vipya kulalamikiwa na upinzani. Nafikiri ipo haja ya kuwapa takwimu ya kesi na vipigo huko nyuma ili tuache kutafuta chaka la kumtupia kila zigo JPM. Kama kuna kigugumizi cha kupata viongozi wapya wenye uwezo kutupa kasi mpya against CCM basi ikulu ni ndoto.

Kazi yenu nzuri kuikosoa CCM mngeifanya kwa nguvu hiyo hiyo vyama vyote hasa vyama vikubwa mngesaidia sana siasa zetu. Otherwise endeleeni kuikosoa CCM ili izidi kuwa bora na endeleeni kupotezea ya upande wa pili wabakie kuwa wapinzani wa kudumu.
 
Nyie mpaka da...m imwagike ndio mtaacha hizi kejeli.

Tukianza kutendeana inavyostahili na kila mmoja akaonja machungu ya tunachokitafuta, hizi kejeli na dharau ndipo vitakoma.

Ziko njia nyingi tu za kufanya kila upande uonje ladha ya matendo mnayotendea wengine na kisha kuwakejeli.
 
Kasaini buku Saba yako mkuu lumumba, imeshaingia....
 
Nyie mpaka da...m imwagike ndio mtaacha hizi kejeli.

Tukianza kutendeana inavyostahili na kila mmoja akaonja machungu ya tunachokitafuta, hizi kejeli na dharau ndipo vitakoma.

Ziko njia nyingi tu za kufanya kila upande uonje ladha ya matendo mnayotendea wengine na kisha kuwakejeli.
Tatizo hampendi facts ....ningeandika Chadema yazidi kuimarika nikula likes buku ...
 
Mmeshaona watu kama makondo ila mnasahau ni kazi ndogo sana kubadili hali ya mambo.

Unaweza kutenda matendo kumi ila mwenzako akatenda moja tu likarudisha nidhamu na kuheshimiana.
 
Mimi mwenyewe ningependa kujuzwa majukumu ya wanaharakati ni yapi, ili nijue pa kuanzia.
 
huwezi kuwalaumu upinzani kwa hali ilivyo hivi sasa coz ni ngumu mpinzan kujipanga au kufny siasa kwa namna yeyote ile, labda km unatk wafanye fujo ambayo hamna mtu mwenye interest hio, ndio maana hata ww ,mleta mada umishia kuulaumu tu upinzani hujagusia hata ni kitu gan ambacho ni right kwa wao kufanya sasa hivi,
 
Mmeshaona watu kama makondo ila mnasahau ni kazi ndogo sana kubadili hali ya mambo.

Unaweza kutenda matendo kumi ila mwenzako akatenda moja tu likarudisha nidhamu na kuheshimiana.
Siasa ulizong'ang'ania zimepitwa na wakati. Zama hizi watu wanataka siasa fikirishi. Tangu mwaka 2005 mmebeba siasa za namna ile ile hakuna ubunifu. Siasa za kulaumu laumu na kutukana ni za kishamba. If you don't change, situation will change you.
 
Mimi ningependa kujuzwa kwanza majukumu ya wanaharakati ni yapi?
 
Hao ni Maria Sarungi,Carol Ndosi,Fatuma Karume
 
Halafu cha kushangaza wanajiita wanaharakati watetezi wa jamii lakini wabaguzi kweli na kauli zao zimejaa mihemko. Ukiwauliza maswali ya maana kwenye mitandao wana kublock. Hawana tofauti na Mange. Kichwani wapo empty. Hawawezi mijadala mipana ya kujenga nchi.
 
MTAZAMO, Nyani Ngabu,

..hapa MHESHIMIWA MBUNGE amepigwa na green guard.

..Polisi walikuwepo, na hawakumpa msaada wowote.

..naomba muwashauri CDM jinsi ya kukabiliana na mazingira hayo ya kisiasa.

Hapa mliowezaje
Screenshot_2018-08-14-22-24-11.jpg
 
Nyie mpaka da...m imwagike ndio mtaacha hizi kejeli.

Tukianza kutendeana inavyostahili na kila mmoja akaonja machungu ya tunachokitafuta, hizi kejeli na dharau ndipo vitakoma.

Ziko njia nyingi tu za kufanya kila upande uonje ladha ya matendo mnayotendea wengine na kisha kuwakejeli.
Keyboard warrior! Unasubiri wengine waandamane ww uje kupost 24/7, ukitaka damu imwagike na ww uwe wa kwanza kuimwaga na sio kusubiri uje kupost jf!
 
Back
Top Bottom