KA SHFA ZAIDI VIONGOZI WA MECKI
Viongozi wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Kilimanjaro wameingia kwenye kashfa mpya baada ya kupokea rushwa na kuzuia kuchapishwa kwa habari ambayo mwandishi mwenzao alipigwa na kujeruhiwa vibaya na askari wajeshi la polisi.
Habari zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea huko moshi Kilimanjaro hivi karibuni pale askari mmoja wa jeshi la polisi alipompiga mwandishi wa habari paul wiliam wa na kumuumiza vibaya.
Taarifa zinaeleza kuwa mwandishi huyo alikua anafuatilia habari ambayo ilikuwa inamhusu askari wa jeshi la polisi kwenye kituo cha polisi na ndipo askari huyo alipogundua kuwa ni mwandishi wa habari akampiga vibaya na kumuumiza pua baada ya kupasuka mishipa ya ndani ya pua
Mwandishi huyo alitoa taarifa kwa wenzake ili apate msaada kutokana na kuvuja damu nyingi huku maaskari wakikataa kumpeleka hospitali na ndipo wanahabari wakakusanyika na kwenda kituo cha polisi cha kati na kumkuta mwenzao huyo yuko hoi bin taabani wakalazimisha apelekwe hospitalini maana askari walikuwa wanataka aandike maelezo kwanza huku akiwa anavuja damu na nguo zake zikiwa zimelowa damu zote
Alipelekwa hospitali ya mawenzi na muda usio mrefu wanahabari wengine kama 7 wakiwemo viongozi wa mecki mwenyekiti rodrick makundi na katibu mkuu msaidizi dikson busagaga walifika kujua kulikoni huku mwandishi huyo akiendelea kupata matibabu
Baada ya kupatwa matibabu hayo wanahabari hao waliandamana na wiliam hadi kituo cha polisi kwa ajili ya kuandika maelezo na kasha wakaonana na kamanda wapolisi mkoa rpc
Hapo ndipo kasi ya rushwa ikaanza kupanda. Makundi na busagaga waliwaomba wenzao kuwa wasubiri yafanyike mazungumzo kati ya viongozi waliokuwepo na baadhi ya maofisa wa polisi pamoja mjeruhiwa na ndipo walipotoka nje mwenyekiti makundi alipowasihi wenzake kuwa habari hiyo isiandikwe kwa vile polisi wameomba yaishe.
Lakini baada ya hapo ndipo ikajulikana kuwa makundi na busagaga walipewa kiasi cha shilingi 300,000 kwa kusaidia kuziba midomo waandishi wa habari fedha ambazo waligawana viongozi hao wawili huku waandishi wengine wakipewa fehda nyingine nje ya hizo kiwango cha 20,000 kila mmoja.
Pia inasemekana makundi na busagaga walitoa orodha ya uongo ya waandishi wa wa habari waliokuwa eneo hilo wanoahitaji kuzibwa midomo yao kwa kuongeza majina mengine 6 ingawa wahusika hawakuwepo na kupata zingine 120,000 ambazo waligawana viongozi hao wawili
Waandishi waliokuwepo wanadai kuwa walipohoji ni kwanini wasiandike habari za mwandishi wiliam aliedhuriwa, busagaga alijibu kwa kebehi na dharau kuwa anaetaka kujua sababu aandike barua kwenye chama ajibiwe kiofisi
Jee hii ni halali?, hivi kweli dhamani ya damu ya mwandishi huyu ni shilingi 20,000?, viongozi hawa wana nia njema kweli ya kuwoangoza wenzao kwa kufuata maadili? Hivi walipowaongoza wenzao kuandamana baada ya mwangosi wa iringa kuuwawa si ilikuwa ni unafiki tu? Sasa nafasi ya wanahabari Kilimanjaro na usalama wao ni ipi kufuatia ufisadi wa viongozi kama hawa ambao ni watetezi wao waliowachagua kwa kura zao?
1. Ikumbukwe viongozi hawahawa wameshatuhumiwa kubadilisha kiwanja cha chama chao kilichoko hai kwa kigogo kwa ushirikiano na kiongozi wa halmashauri ya hai huku wakipokea shilingi milioni 28 wakati mchakato huo ukiendelea
2.
Pia viongozi hawa wa mecki hivi karibuni wakiongozwa na mwenyekiti wao makundi walishiriki kuihadaa mamlaka ya maji moshi kuwa kuna wanahabari 5 wamegundua kuwa mradi wa maji uliozinduliwa kiboriloni hautoi maji na muwasa wakatoa shilingi laki 5 kuwaziba midomo jambo ambalo si kweli na fedha hizo wakagawana
3.
Pia makundi huyu huyu na busagaga huyu inasemekana majuzi walimshawishi mwenyekiti wa kncu swai anaetuhumiwa kwa kashfa mbalimbali aitishe kikao cha waandishi wa habari kukanusha habari zilizoandikwa na nipashe kuhusu kuzwa kwa nyumba za kampuni ya kukobolea kahawa na swai akakubali na waandihi waliofika wakalipwa fedha za wakulima shilingi 50,000 kila mmoja
4.
Pia inasemekana viongozi hao wa mecki wameandaa mazingira ya kumtoza tena swai wa kncu fedha ili kuziba kashfa ya kutafuta na serikali kwa kukata miti kwa kisingizio cha kupewa kibali na mkuu wa mkoa kumbe sio kweli maana mkuu wa mkoa hawezi kutoa kibali hicho wakati yeye ndiyo yuko mstari wa mbele katika kuokoa mazingira Kilimanjaro
5.
Ni viongozi hawahawa ambao hivi majuizi waliripotiwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa walikwenda kwenye taasisi moja na kuchukua shilingi milioni kadhaa kwa jina la chama na kugawana
Utpc mpo? Mct mpo? Angalieni tasnia ya habari inavyochafuliwa na watu wenye tama za fedha! Hii ni fedheha kubwa na waandishi wataendelea kupigwa maana dhamani yao imeshawekwa wazi na makundi pamoja na katibu wake busagaga, hii ni aibu kubwa kwa tasnia ya habari hapa nchini.