Wanahabari Watembelea Machimbo ya Almasi Kongwa.

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Friday, June 15, 2012

Na Mwandishi Wetu, Songwa-Shinyanga

Baadhi ya waandishi kutoka jijini Dar es Salaam na mkoani Shinyanga wametembelea machimbo ya almasi yanayofanywa na wananchi eneo la mjini mdogo wa Songwa.

Ziara ya waandishi hao imekwenda sambamba na kufanya uchunguzi juu ya huduma mbalimbali za kijamii zinazotolewa na Serikali kwa wakazi wa maeneo hayo, yaliomo ndani ya Wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga.

Waandishi hao wameshuhudia namna wananchi na hasa vijana wanavyojishughulisha na shughuli nzima za machimbo ya madini ya almasi licha ya Kata ya Songwe kukabiliwa na huduma duni za maji safi na salama kwa matumizi yao pamoja na yale ya shughuli za machimbo.

Mtandao huu utawaletea mahojiano ya wananchi eneo hilo pamoja na hali halisi ya huduma anuai za kijamii kwa wakazi wa Kata hiyo ya Songwa iliyopo Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga muda si mrefu.

Chanzo: Mo blog

Tafadhali Waandishi Wa Habari Msiwauze wachimbaji wetu na Machimbo yetu huko SONGWA kwa Walafi Nchi za Nje;

Wakijua tu watailazimisha Serikali wauze hayo Machimbo; itakuwa kama Geita - Kabla iliitwa Nyarugusu.

Lakini, Mwandishi wa Mo Blog kafika huko Mmmm... Sijui tena!!!
 
Mkuu kila nikisoma hiyo Kongwa napata mshituko. Najua ni ile ya Dodoma kumbe kuna nyingine!
 
Mkuu kila nikisoma hiyo Kongwa napata mshituko. Najua ni ile ya Dodoma kumbe kuna nyingine!

Ni Songwa, Unajua JAMII FORUM WEBSITE nime correct the error lakini still inakuja as Kongwa; Ndio ya kwetu tuvumiliane

Ni Songwa - Shinyanga.
 
Ni songwa na sio KONGWA.

Is just the Tittle but if you look on the Message it has SONGWA and not KONGWA; Tatizo ni Jamii Forum Web Site haikupi ruhusa ya kubadilisha Tittle kama kuna typo Error.

It is very difficult sometimes for some who are trying to be perfect or reading a perfect articles with no errors
 
juu ya shughuli za uchambaji na matatizo yake ki ujumla, mm ni mdau na nipo hapa .
 
Is just the Tittle but if you look on the Message it has SONGWA and not KONGWA; Tatizo ni Jamii Forum Web Site haikupi ruhusa ya kubadilisha Tittle kama kuna typo Error.

It is very difficult sometimes for some who are trying to be perfect or reading a perfect articles with no errors

Mkuu naomba nikuweke sawa kidogo, kunatofauti kubwa kati ya www.jamiiforum.com na www.jamiiforums.com. Kwasasa unatumia jamiiforums.

Tuendelee na mada.
 
Back
Top Bottom