Wanahabari fanyeni haya haraka sana

GRAMAA

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
1,155
3,399
Kutokana na ripoti ya CAG inayoonesha upigaji wa hali ya juu katika serikali ya awamu ya tano chini ya Mwendazake basi haraka sana fanyeni yafuatayo:

i/ Acheni kuandaa makala na vipindi vinavyosifu mambo aliyofanya Mwendazake. Umeshaambiwa ATCL imeingiza hasara ya 153bilioni kwa miaka mitano. Unapata wapi ujasiri wa kuandaa makala au kurusha kipindi kinachosifu manunuzi ya ndege yaliyofanywa na Mwendazake huku ukijua kabisa midege hiyo ni hasara tupu?

ii/ Achani haraka sana kupiga nyimbo za wasanii makanjanja waliokuwa wanaimba kwa kusifu mambo ya kihuni yaliyokuwa yanafanywa na serikali ya Mwendazake. Unapata wapi ujasiri wa kupiga nyimbo zinazosifu mambo yanatia hasara nchi. Mfano SGR, midege n.k?

iii/ Mtafuteni Hamisi Kigangwala haraka sana na mumuulize hivi watanzania anawachukuliaje mpaka akaamua kuwafanyia upuuzi ule? Hivi anajiamini nini mpaka akaamua kutufanyia ufisadi ule?

iv/ Watafuteni viongozi wa dini haraka sana ili watubu na kutuomba msamaha sisi wananchi kwa kutuaminisha kwamba Mwendazake na serikali yake walikuwa watakatifu sana kumbe ukweli ni kwamba walikuwa wapigaji waliotukuka. Wasipofanya hivyo Mungu atawanyoosha kwa njia yake.

v/ Na mwisho japo sio kwa umuhimu. Naomba haraka sana mkamuulize Ndugai yeye ni kiumbe wa aina gani mbona haeleweki?

Uzi ndiyo huo. Mods nawazuum tu kwa mbaaali.
 
'
IMG_bzi0yj.jpg
 
Embu tuwajaribu na kina Ndaki mashimba kuwapa u waziri mkuu Napo tuone au Tamisemi tu, Maana wasomi wanaikula Sana hii nchi, ni majizi makubwa hata soni hayana
 
Uzi wako wa kipuuzi tu huu.

Unatakiwa uwataje na wafutao.
1. Rais.
2. PM.
3.

Uzi wako wa kipuuzi tu huu.

Unatakiwa uwataje na wafutao.
1. Rais.
2. PM.
3. VP.
Hawa ndio wa kwanza kuuliza na kususia habari zao kama unaakili.
Nisome tena unielewe mkuu mimi naongea kwa nafasi yangu ila kama na wewe una yakwako anzisha uzi wako uwataje hao uliowataje. Hujakatazwa mkuu
 
Pia wapeni wapinzani press conference wazungumze ukweli na mstakabali wa nchi yetu manake wao ni muhimu mno kuzuia madudu kama ya Magufuli.
 
Back
Top Bottom