kALEnga kidamali
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 542
- 735
Nimekuwa nijiuliza sana hasa huko miaka ya nyuma shule ya msingi tu unakutana na wanafunzi wakubwa yaani ni watu wazima na ukimkuta anayesoma kwa malengo ni kweli anasoma kwa bidii na hata akienda sekondari basi anakuwa akijua anachokifanya kwa sababu ya u utu uzima wake na kupevuka ki akiri kisawa sawa.
Kwa asilimia kubwa wanafunzi wa sekondari walikiwa wakiheshimika na kuogopewa sana mitaani kwa kuamini wao wana uwezo tofauti na wanajielewa vya kutosha na ni kweli yaani hata familia na ndugu pamoja na majirani waliwategemea hawa wanafunzi hata kwa kutoa ushauri kwa baadhi ya masuala muhimu yanayowakumba yaan ilikuwa ni heshima kubwa sana mwanafunzi kusoma shule sekondari imani ya jamii pia ilitawala kwa mwanafuzi wa sekondari kwanza kimwonekano ilitosha kujua kama anajielewa ipasavyo.
Sasa nije kwa hiki kizazi cha sasa ambacho mtoto anapelekwa form one akiwa bado yuko na miaka 13 akifika kule bado ana ile michezo ya kupigana mateke na wenzake, kurushiana tunda za ubuyu, n.k sasa na wakati huo huo asome physics na hesabu pamoja na chemistry... Hata akieleweshwa akaelewa baada ya muda akienda cheza michezo ya kitoto na wenzake lazima asahau kutokana na uchanga wake wa akili hii hadi anafika form three ndo angalau anaanza kujua kumbe nipo shule anaana kutia jitiahada anajikuta mambo ni mengi ana panic necta form four hii hapa basi huku na huku anapata zake division 4 ya mwisho point 34 au 35 anaenda zake kumuonesha baba na mama ake nyumbani baada ya hapo maisha yanaendelea.
Kutokana na hili nini kifanyike kwa sababu najua hiki kizazi cha digitali ambacho mwanafunzi ana smartphone anaweza access kila kitu mtandaoni mbali na notes za darasani ingawa najuwa wanafunzi wengi huwa wakijikita sana kwenye masuala tofauti na yale ya kielim pindi waingiapo mitandaoni. Lakini licha ya upatikanaji rahisi wa materials na notes za darasani ndio matokeo yanakuwa mabovu kuliko kipindi kingine chochote hapa kwetu tanzania hadi inafikia muda hata NECTA wanarudia sahihisha mitiani ili kupunguza waliofeli.
Sasa je turudishe utaratibu kwa kuanza kuzingatia vigezo vya umri pindi mtoto anapo anza shule ili angalau akifika sekondari awe anajielewa kama wale wanafunzi wa zamani? nikimaanisha 2005 kurudi nyuma angalau na wale nyuma ya 2010 nao kidogo walikuwa wakijielewa tofauti na hili wimbi la sasa ambao wanasoma hadi form then wanakuja endesha bodaboda mitaani na kunyoa viduku huku wakiwa na zero zao makabatini huko magetoni mwao.
Yaani sasa hivi imefika mda hata ambae hajasoma sekondari anajiona analinganga na mwanafunzi wa sekondari au akajiona ni bora zaidi ya huyo mwanafunzi na wala hajutii kutokusoma sekondari kwa vile anavyomuona mwanafunzi wa sekondari alivyo.
Tena hata kwa level ya chini kwa maana ya mwanafunzi wa primary wala haogopi wala kutishwa na ukubwa wa level ya sekondari na akimuona mwanafuzi wa sekondari anaona kawaida tu na wakati mwingine anacheza nae au anaweza akamshinda hata kujibu maswali madogo madogo ya uelewa tu.
Sasa nini kifanyike kwa hawa wanafunzi wetu wa sasa ili heshima irudi mitaani na majumbani ikipita njian uniform ya sekondari watu wakatishe story zao kuwatazama na kujawa na heahima juu yao.
===================
Wenu
Kalenga kidamali