Wanafunzi zaidi ya 31000 kukosa mikopo ya elimu ya juu 2017/2018

Halafu kuna watu unasikia wanasema serikali ya Magufuli itatufikisha mbali,mara ni jembe na blaablaa kibao.Bodi inauwezo wa kutoa mikopo kwa 49% pekee ya waombaji huku 51% wakilia na kusaga meno na kurudi vijijini.

Watanzania sijui kama tumelogwa na nani! tulitangaziwa kumchagua Lowassa ili elimu iwe bure kutoka Kindergarten mpaka chuo kikuu tukachagua tunachopenda zaidi, sasa tunalia na bodi ya mikopo kwanini? Tumechagua wenyewe kwa hiyo tuvumilie na tujifunze kujitegemea, it is our choice!
 
Tanzania ya viwonder

WANAFUNZI 31,000 KUKOSA MIKOPO ELIMU YA JUU
download-5-4.jpg


Na LEONARD MANG’OHA -DAR ES SALAAM

WANAFUNZI zaidi ya 61,000 wamewasilisha maombi ya mikopo katika Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa mwaka mpya wa masomo wa 2017/2018, unaotarajiwa kuanza Oktoba, mwaka huu, huku idadi kamili ya wanaotakiwa kupewa ni 30,000.

Pia kati ya hao, waliowasilisha maombi yaliyokamilika ni wanafunzi 43,811, huku 11,200 taarifa zao zilibainika kuwa na kasoro na upungufu mbalimbali.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi kwa njia ya simu hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razak Badru, alisema wanafunzi hao ni wale waliofanikiwa kuomba katika muda uliofikia ukomo Agosti 11, mwaka huu.

“Hawa tunaweza kusema ni incomplete kwa sababu wako ambao wamekosa baadhi ya nyaraka kama vile vyeti vya kuzaliwa au taarifa za wazazi,” alisema.

Pamoja na kuwapo kwa kasoro hizo, alisema wale wote walioomba katika muda maalumu uliopangwa watapata fursa ya kusahihisha taarifa zao.

Alisema kwa sasa wanaendelea kufanya uchambuzi wa taarifa za waombaji ili kubaini walio na sifa za kupewa mikopo na baada ya kukamilika kwa uchambuzi huo watatoa majina ya wale waliopitishwa kupata mikopo hiyo na kuanza kuwapangia mikopo yao.

“Kwa mujibu wa kalenda yetu ambayo ndiyo inayotuongoza, inaonyesha kuwa, hadi kufikia Oktoba 10, mwaka huu, taratibu zote za uchambuzi na kutangazwa kwa majina ya wale walio na sifa ya kupata mikopo inatakiwa kuwa imekamilika na tayari wanafunzi waanze kupelekewa mikopo hiyo vyuoni kwao,” alisema.

Katika hatua nyingine, Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Omega Ngole, alisema wataangalia vigezo mbalimbali kwa wanafunzi 30,000 wanaotarajiwa kupewa mikopo hiyo.

Alivitaja baadhi ya vigezo hivyo kuwa ni kwa wanafunzi waliopata nafasi katika vyuo vikuu, wawe raia wa Tanzania, wawe wamemaliza kidato cha sita si kwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita na vingine vyote vilivyoelekezwa na HESLB.

Chanzo: Mtanzania
31000 watakosa mkopo ili hali wamelipia Tsh 30000 kila mmoja jumlisha kutuma EMS walio wengi wametuma kwa Tsh 13100 ukijumlisha ni sawa na Tsh 133,610,0000.

LAkini licha ya kukusanya pesa yote hiyo na ukichanganya bajeti yao ya mwaka bado utasikia hata hao 30000 ambao inasemekana ndio watakao pata huo mkopo bado utasikia wamepewa asilimia mbili, wengine asilimia 5.

Dah inasikitisha sana nchi kama hii ambayo kila kukicha mifumo ya ukusanyaji kodi inazidi kuimarika lakini unashangaa nikivipi inashndwa kuwalipia wanafunz elfu 61.
 
"Kila mwenye uhitaji wa kweli atapata mkopo" vs Watakaopata mkopo wanatarajiwa kuwa 30, 000. Walioomba ni zaidi ya 61,000. Kwa hiyo serikali imepiga hesabu na kuona 31,000 "hawana" uhitaji au wametenga mikopo kwa watu 30000 na sio issue ya uhitaji? Serikali iwe wazi sidhani kwa hali za watanzania kuwa ni hao 31000 kweli hawana uhitaji.
Ni kitu cha kushangaza kuwa unataka nchi ya viwanda lakini human capital investment inakuwa ndogo kiasi hiki. Vijana na wazazi watavurugwa kwa takwimu hizi. Hapo hapo kuna investment zinafanywa na serikali kwa pesa ambayo haikuidhinishwa bungeni.
Hatuwekezi vya kutosha kwenye elimu (mikopo ni mfano)-lakini pia hata vyuo vya serikali ni kilio tu. Mafungu ya kuendesha masomo (hasa elimu ya vitendo-practials) ni chini ya kiwango, vyuo vinashindwa kupiga kelele (ndo uzalendo wetu) lakini tunalalamika kuwa vijana watokao vyuoni hawajaiva.
Kuanzia tarehe 2 Oktoba 2017 watu watakuwa na furaha-wengine vilio, lakini mikopo itakapo tangazwa kwa taarifa hii, vilio vitakuwa vingi tu labda serikali iamue vinginevyo.
Hao 30,000 Watakaopata Mkopo
Ni Including Na Waliokosea?
 
Kitu ambacho watanzania inabid tupigane nacho ni elimu, dunia inatawaliwa na watu wenye taarifa na maarifa
 
Hao 30,000 Watakaopata Mkopo
Ni Including Na Waliokosea?
Ameahidi waliokosea watapewa nafasi ya kurekebisha mambo, ikiwa hivyo ina maana nao watafikiriwa kupata mikopo na wenzao mara baada ya kurekebisha.
 
*BREAKING NEWS*

*ZAIDI YA WANAFUNZI 31000 KUKOSA MIKOPO MWAKA WA MASOMO 2017/2018*

*BODI YA MIKOPO IMEPOKEA JUMLA YA MAOMBI YA WANAFUNZI 61000*

*LAKINI ITATOA MIKOPO KWA WANAFUNZI ELFU 30 TU*

*PIA KUNA MAJINA YA WANAFUNZI ZAIDI YA ELFU 11 WALIOKOSEA KUJAZA FORM ZA MIKOPO,WATAPEWA MUDA WA KUREKEBISHA HIVI KARIBUNI*

*SOMA TAARIFA KAMILI HAPO>>>>>>>>>>* 31000 STUDENTS TO MISS LOANS FROM HESLB 2017/2018 | 2017/2018 selection OFFICIAL BLOG

*_Tafadhali sambaza kwa wenzako wote*
d3b617a77fa10f2bd19dee48da8b7ccc.jpg
 
Mtetezi wa wanyonge ni yule anayepata shida hospitali ya Nairobi waliosalia ni watafuta sifa na ubabe mwingi pasipo kujali mateso ya wananchi.
 
Back
Top Bottom