Tatizo wanafunzi hawa nao hawana msimamo na elimu yao haiwasaidii kuwa na utambuzi mwisho wa siku wanajiendea tu kama nao ni watu wasio na elimu ya kutosha,maana taarifa niliyonayo ya muda mrefu hapo Mhimbili hakuna serikali ya wanafunzi ilishavunjwa na wamepigwa mkwala wakanywea,sasa leo hii kwa kuwa mmekuwa waoga wa kudai haki zenu kwa muda mrefu na mmekuwa na tabia ya kujitenga haya leo ndo yanayowakuta.cha msingi muungane na mdai haki zenu kwa nguvu zote na kwa taratibu zote na kama wakiendlea kuiminya basi mgomo ni moja ya njia mbadala.