Wanafunzi wenye mimba

Wanafunzi wenye mimba

Wong Fei

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2016
Posts
5,509
Reaction score
7,263
Nchi nyingi duniani inautaratibu wake katika masuala ya elimu, ndiyo maana kuna sheria mbali mbali zimetungwa ili kuwafanya wanafunzi kuwa na nidhamu. Siwezi kumshangaa Bwana yule kwa sabb huu utaratibu ulikuwepo kipindi cha nyuma kabla ya kubadilishwa na kumruhusu mwanafunzi kuendelea na masomo baada ya kujifungua. Ila kwasasa jambo hili limekuwa gumzo sana na baadhi kushangilia na wengine kuchukizwa. Waliosoma miaka ile wanajua huu utaratibu. Ukipata mimba (Ndiyo maana wanafunzi wa kike walikuwa wanapimwa kila baada ya muda fulani), utoro uliokithiri, kumpiga au kumtukana mwalimu, ukikutwa unafanya ngono, una picha za utupu, na mengine yanayohusiana na hayo unafukuzwa shule hakuna mjadala. Huu utaratibu siyo Tanzania tu ni kwa karibu nchi zote duniani.
Anachokifanya bwana yule ni kutaka sifa tu. Hivi ukifanya jambo kimya kimya haliwezi kufanyika? anachokifanya nikujiongezea maadui wengi na kuchukiwa tu. Utamsikia nawajua waliofanya madudu haya, unatuambia sisi ili iweje? Ngoja nikuulize swali
Mtu aliyekula wali na nyama kisha akaanza kutangaza na kujigamba amekula wali na nyama na mwingine amekula ila akaa kimya nani hapo ataonekana mwenye hekima?

Haya mambo yako hivi "Raisi amekataa mwanafunzi aliyepata mimba kuendelea na masomo katika shule za serikali hata baada ya kujifungua lkn ni ruksa kwa mwanafunzi aliyepata mimba au kuolewa kuendelea na masomo yake kwenye shule binafsi" . Ndiyo maana utamsikia "mnaotetea mambo haya jengeni shuleni zenu" kwann asikataze pote yaani serikalini na binafsi? Kipindi nasoma nilisoma na wanafunzi wengi wenye watoto, wengine walikuwa wameachika. Ila ilikuwa ukigundulika una mimba (siyo kuwa na mtoto) ulikuwa unafukuzwa shule, ila baada ya kujifungua unatafuta shule nyingine unasoma kama kawaida. Nakumbuka kipindi kile tulikuwa tunasoma na mama mzima (Sister-roman catholic).

Hivyo ndivyo ilivyo duniani kote. "DAMU NZITO KULIKO MAJI" Bwana yule alishawahi kuwafukuza wanafunzi wa chuo fulani kuwa hawana sifa na kuwaita v...i..l..a...za lkn mtoto wake alifeli. Je, unafikiri mtoto wa bwana yule analima matikiti au anafanya kazi ya umamantilie sasa? Damu ni nzito kuliko maji.
Huwa naamini sheria zimetungwa kwa watu wa chini tu. Uhakiki umepita ushasikia mama uhakiki kajihakiki? Bwana yule kafuta ajira na kuongeza makato ya HELSB 15% lakini hatusikia watoto wake wanalalamika kwa hili. Kupanga ni kuchagua, uchague mtoto wako aliyepata mimba akae nyumbani au umpeleke shule akasome ili baade naye ajitegemee. Siku ukiwa na familia utajua haya, Huu ni muda wa kupongezana ila muda ukiisha.......KILA ABIRIA ATACHUNGA MZIGO WAKO
 
Back
Top Bottom