Wanafunzi wengi wa Vyuo Vikuu Ni Wakina "AKWILINA"

Wanafunzi wengi wa Vyuo Vikuu Ni Wakina "AKWILINA"

MimiJoel

Member
Joined
Sep 22, 2017
Posts
42
Reaction score
46
Kifo cha Akwilina ni Tukio lililoacha Simanzi, huzuni na Masikitiko Ndani ya Mioyo ya Watanzania wengi, wakiwemo Wanasiasa, Wanafunzi wenzie, ndugu na jamaa. Lakini kubwa zaiid Kifo cha AKWILINA kimeacha pengo katika Familia yake ya Mzee Akwilini Shirima Na kuua Kabisa Ndoto za Familia ya Akwilina (BABA na MAMA) ya kuamini kuwa ipo siku wataagana na umasikini. Kwakua AKWILINA ndiye mtu pekee aliyekuwa Tegemeo kwa Familia yake..

AKWILINA Alikuwa Mwanafunzi wa Chuo kikuu katika Chuo cha usafirishaji NIT, Walioenda kwa ndugu zake Mbezi na wale wa Rombo Kilimanjaro wamejionea maisha halisi ya wapi anatoka AKWILINA na hali ya wazazi wa AKWILINA.
Sasa Basi AKWILINA huyu ambaye Leo Tunamlilia na kumsikitikia Tunaomba Awe Balozi Mzuri wa Kuonesha Maisha Halisi ya Wanafunzi Wengi wa Vyuo Vikuu Hapa Nchini Kwetu Tanzania.


Wanafunzi wengi wa Vyuo Vikuu hapa Tanzania Ni watoto wa Masikini waliopambana Kufa na Kupona katika harakati zao za Kuhakikisha Wanafaulu vizuri Sekondari na badae Wafike Vyuo Vikuu, Wakiamini Wanaenda kutimiza Ndogo zao za kuwa Madoctor, Maengineer, Waalimu, Wanasheria n.k Asilimia Kubwa ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu ni WakinaAKWILINA, Naposema ni AkinaAkwilina Namaanisha Wao Ndio Tegemeo kwa Familia zao huko watokako.

Watu wengi Huamini Wanachuo Ni watu wa Maisha Mazuri huko watokako na wanapesa za kutosha kujikimu na maisha ya chuo, ndio maana Kuanzia Wenye Nyumba Jirani na maeneo ya Vyuo Vikuu Bei Huwa Juu, Wafanyabiashara pia Bei Juu na Kila huduma Jirani na maeneo ya chuo bei huwa Juu..

AKWILINA huyu ambaye leo tunamlilia tunaomba awe nembo kwenu na mpate picha halisi ya sisi Wanachuo, kuanzia tunapotoka, nafasi zetu katika familia na maisha yetu kiujumla.. Wanachuo hatuna Maisha mazuri, Wanachuo ni Tegemeo kwa familia zetu, pamoja na kuwa wapo Wanachuo wanakosa kabisa mikopo na kuamua kukatisha masomo yao njiani na kuua kabisa Ndoto zao kutokana na hali Duni za Familia zetu huko Tutokako.

Mwanachuo huyu ni tegemeo kwa familia akiwa ndani ya chuo, Lakini ni Imani ya familia yake kwamba Mtoto Wao anakuja kuwa mkombozi wa familia baada ya kumaliza masomo yake, kwa kuamini atapata ajira nzuri na kuitoa familia katika janga la umasikini. Elimu Yetu haimuandai mwanafunzi kujiajiri, elimu Yetu inamuandaa AKWILINA huyu ambaye ndiye mkombozi wa familia KUAJIRIWA kwa asilimia Kubwa...

Leo tunaona Ajira Hakuna, Wale wakinaAKWILINA waliotegemewa kuja kuzikomboa familia zao, wanarudi majumbani wakiwa wahitimu wa Vyuo Vikuu na vyeti safi kabisa... Je? Huu sio msiba kwa Wazazi Wao, Je vipi kuhusu mategemeo ya wazazi wao na Ajira Hakuna?

AKWILINA umeondoka mapema sana, AKWILINA Umetuachia Majonzi Sisi wenzio, Tunakulilia LEO haupo nasi Tena, Akwilina hatutoacha kukulilia baada ya kumaliza Chuo kama Dada na Kaka zetu, Na Tukarudisha Misiba Majumbani Mwetu Badala ya Furaha ya ukombozi wa Janga La umasikini Kwa Ukosefu wa Ajira Pamoja na Mitaji ili Tujiajiri..
Wanavyuo Wote Tunaotoka Kwenye Familia Masikini ni WakinaAkwilina, Sisi Ni Tegemeo kwa Familia Zetu Huko Tutokako!!!


[HASHTAG]#AKWILINA[/HASHTAG] [HASHTAG]#AKWILINA[/HASHTAG] [HASHTAG]#AKWILINA[/HASHTAG]
 
Huo ndio ukweli japo wengine wakija mjini hujisahau na kuwa masister duu na mabrazamen na kusahau hali walizoziacha kwao in short maisha ya chuo ni fake.
Wanachuo badilikeni msituangushe wazazi wenu tunawategemea.
 
natamani hata mtu yeyote angemfanya aghairi kwenda makumbusho jioni ile.... nikiona picha najisikia vibaya sana
 
Message sent hakika aqwilina ni Pigo kwa Taifa nzima hasa wanavyuo ambao ndio Taifa la sasa lenye kutegemewa.....
 
natamani hata mtu yeyote angemfanya aghairi kwenda makumbusho jioni ile.... nikiona picha najisikia vibaya sana
Mkuu mimi nilitamani ata alipo ona lile gari akuna siti asingepanda kifo chake ni funzo kubwa alipanda vizuri akiona kabisa ni gari kumbe ni jeneza akujua muda mchache ndio kitabu cha safari ya maisha yake hapa duniani kinafungwa rasmi kweli kifo kinaumiza sana ila atunajisi
 
[HASHTAG]#Akwilina[/HASHTAG] weeee tulimalize tatizoo ..ololoooo [HASHTAG]#akwilina[/HASHTAG] mpenzi na kupenda ...

ASANTE MUANDISHI UMENIPELEKA MBALI MNOO KIFKRA ..HAYO YOTE ULIYOYANENA NIUKWELI MTUPU nayanapaswa kutazamwa kwa jicho la tatu ili kumkomboa maskini huyu ambaye ni M TANZANIA ambaye amekuwa anapamban usiku na mchana katika kuhakikisha anajikomboa kwenye tanuri linalo nuka shida...
 
Back
Top Bottom