Wanafunzi waua Chuo kikuu Mzumbe

Wanafunzi waua Chuo kikuu Mzumbe

uhurumoja

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Posts
11,499
Reaction score
27,284
Wanafunzi chuo kikuu Mzumbe Morogoro wamemuua mwanakijiji cha Changarawe kijana anaekadiriwa kuwa na miaka 24 kwa tuhuma za wizi, kijana huyo ameuliwa jana majira ya usiku na wanafunzi katika maeneo ya bweni la kimweri na kibasila.

Hii ni mara ya pili ndani ya miezi isiyozidi mitatu kwa wanafunzi hao kuua raia ambao walishukiwa kujihusha na vitendo vya wizi wa mali za wanafunzi.

Ikumbukwe kuwa wanafunzi wa Mzumbe baadhi tuko chuoni sasa katika semester yumbishi kutokana na chuo kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi.
 
Kijana ametutoka na binafsi niko hapa msibani nyumbani kwa wazazi wake. Alikuwa maarufu kwa ukwepuaji wa laptop za wanachuo. RIP a.k.a 'bad boy'
 
Kijana hajawatoka bali mmemtoa na mkome kusema bwana alitoa na bwana ametwaa ila dhambi ya kuua iko pale pale maana amri ya Mungu ilisema tusiue na haikufafanua kuua kwa vipi. Hapo mseme bwana alitoa na nyie mmetwaa sio bwana ametwaa ila nawapa pole wanakijiji kwa kumpoteza kijana wao kabla hajampokea Yesu kama Bwana na Mokozi wa maisha yake. Kama alipata nafasi ya kutubu kabla hajakata roho ataenda mahali pema peponi.
 
Aiseehh! Namkumbuka yule wa takriban miezi mi3 au mi4 iliyopita nilihusika kumbeba kwenye chaga akiwa anakata Roho. Simpatii picha huyo alipokea kipondo cha haja gan!?
 
Dah! Changarawe kitambo sana kuna madogo tulikuwa tunapiga nao ball kina Mlotwa a.k.a masai na Kulwa vijiti alikua anauza jamaa mmoja anaitwa Kenge. Msalimie Matangalu.
 
Wanafunzi chuo kikuu Mzumbe Morogoro wamemuua mwanakijiji cha Changarawe kijana anaekadiriwa kuwa na miaka 24 kwa tuhuma za wizi, kijana huyo ameuliwa jana majira ya usiku na wanafunzi katika maeneo ya bweni la kimweri na kibasila.

Hii ni mara ya pili ndani ya miezi isiyozidi mitatu kwa wanafunzi hao kuua raia ambao walishukiwa kujihusha na vitendo vya wizi wa mali za wanafunzi.

Ikumbukwe kuwa wanafunzi wa Mzumbe baadhi tuko chuoni sasa katika semester yumbishi kutokana na chuo kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi.

Siungi mkono suala la kujichukulia sharia mikononi na kuua mtu. Ila kama jamaa alikuwa kibaka kweli basi yaliyomkuta ni 'occupational hazard'. Hawa jamaa wameibia sana wanafunzi pale kwenye kile chuo na walifikia hatua ya kupora kabisa hasa wadada! Yaani mtu anayeiba huwa simuelewi kabisa, mali ni yangu halafu unaninyang'ang'anya kinguvu huku unanidhuru? Nikikukuta unapigwa, sitashiriki kukupiga ila pia sitakutetea!
 
Angalieni msije mkaanzisha vita kati ya wanafunzi na wanakijiji.

Wana ugomvi wa muda mrefu na wanakiji sababu ikiwa ni mademu wa hapo vijijini mara kadhaa wanakijiji wamekua wakiwafukuza hao vijana wa mzumbe kila wanapoonekana kwenye baa za uchochoroni.so hao vijana wakiona mtu yeyeto wasiyemfahamu hata asiye mwanakijiji humvamia na kumpiga.hovyo kabisa hao vijana
 
Siungi mkono suala la kujichukulia sharia mikononi na kuua mtu. Ila kama jamaa alikuwa kibaka kweli basi yaliyomkuta ni 'occupational hazard'. Hawa jamaa wameibia sana wanafunzi pale kwenye kile chuo na walifikia hatua ya kupora kabisa hasa wadada! Yaani mtu anayeiba huwa simuelewi kabisa, mali ni yangu halafu unaninyang'ang'anya kinguvu huku unanidhuru? Nikikukuta unapigwa, sitashiriki kukupiga ila pia sitakutetea!

By choosing to remain neutral when someone is oppressed means u've decided to be on the side of the opposer-Desimon Tutu.
 
By choosing to remain neutral when someone is oppre ssed means u've decided to be on the side of the opposer-Desimon Tutu.

Ahsante kwa kuonyesha uwezo wako wa kunukuu. Ila umetumia maneno mazuri mahali pasipofaa. Yaani by 'oppressed', unamaanisha mwizi anayepora watu na kuwaumiza/kuwaua kabisa au watu wanaompiga mwizi baada ya kuibiwa!?
 
Mtumishi umenena vyema kabisa inabidi sisi vijana tulioona nuru tuongeze kasi ya kuwafikia watu wasiomjua mungu waokolewe maana dunia imeshaharibika mtumishi
kijana hajawatoka bali mmemtoa na mkome kusema bwana alitoa na bwana ametwaa ila dhambi ya kuua iko pale pale maana amri ya mungu ilisema tusiue na haikufafanua kuua kwa vipi. Hapo mseme bwana alitoa na nyie mmetwaa sio bwana ametwaa ila nawapa pole wanakijiji kwa kumpoteza kijana wao kabla hajampokea yesu kama bwana na mokozi wa maisha yake. Kama alipata nafasi ya kutubu kabla hajakata roho ataenda mahali pema peponi.
 
Wapigwe,nasema hawa wezi wapigwe tu maana tumechoka.
 
Kuna jamaa yangu alikosa nafasi pale akiwa na point tano ingali sister moja ana point 12 kapata kwa same faculty. Shame on them
 
Wizi pale hauishi toka nipo mzumbe sec tunakimbizana nao usiku kumbe mpk leo, ila mmefika mbali kama mmeua
 
Back
Top Bottom