Wanafunzi watatu wauawa kwa radi na wengine 19 kujeruhiwa Kagera

Matukio Jamii

Member
Sep 9, 2015
12
8
Wanafunzi watatu na wengine 19 wamejeruhiwa kutokana na radi wilaya ya Ngara mkoani Kagera. Wanafunzi hao walifariki wakati wanapatiwa matibabu katika hospitali Teule ya Murugwanza wilayani Ngara.

Wanafunzi hao waliambiwa warudi darasani wakati wa michezo na walimu wao baada ya mvua kuanza kunyesha na ndipo radi ilipowakuta kwenye darasa walilokuwepo. Wanafunzi 22 walipoteza fahamu na wengine kujeruhiwa sehemu za miili yao.

Walimu walishtuka walipoona wanafunzi wanatoka madarasani kwa kasi na kwenda kujaribu kuwapa huduma ya kwanza, walipojaribu kupiga simu kuomba msaada zaidi hakuna iliyofanya kazi. Walimu walienda kumchukua muuguzi wa zahanati ili kuwapima na baadae kufanikiwa kuwapeleka hospitali teule.

Mkuu wa wilaya ya Ngara, Honorata Chitanda amesikitishwa kutokea kwa tukio hilo na kuwapa pole wote walioathiriwa kwa tukio hilo na kusema serikali itakua pamoja kipindi chote mpaka hali za watoto hao zitakapoimarika na kurejea shuleni.
 
Back
Top Bottom