WANAFUNZI washinda kesi yao..

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Hatimaye,wanafunzi kwa mamia waliokuwa na kesi dhidi ya Chuo Kikuu cha Ardhi,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wameshinda tena kesi yao.Kesi hiyo,ambayo ni ombi dogo,ni nambari 69/2008 iliyokuwa chini ya Jaji Dr.Feuz Twaib wa Mahakama Kuu ya Tanzania-Dar es Salaam.

Wanafunzi hao waligomea kupewa vyeti vya Chuo Kikuu cha Ardhi na kutaka kupewa vyeti vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Hoja ya wanafunzi hao waliowakilishwa na Wakili Kamuzora ilikuwa ni kuwa wao walidahiliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye kumaliza wakiwa Chuo Kikuu cha Ardhi(zamani UCLAS) baada ya Chuo hicho kuanzishwa.

Katika hukumu yake,Jaji Twaib amekiamuru Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwapa vyeti wanafunzi wote waliokidhi vigezo vya shahada walizosomea.Hukumu hiyo ilisomwa mnamo saa nne na dakika kumi asubuhi ya leo.Umebaki utekelezaji...
 
Nijuavyo mimi UDSM ni sehem inayozalisha watalam wengi sana wakiwemo wanasheria lakin haijawah hata siku moja kushinda kesi mahakamani.
 
Nijuavyo mimi UDSM ni sehem inayozalisha watalam wengi sana wakiwemo wanasheria lakin haijawah hata siku moja kushinda kesi mahakamani.

Kwahiyo unafikiri hata kama mahakama zote ziko chini ya serikali inahararisha serikali kushinda kila inaposimama mahakamani,sheria ni msumeno unaweza kukata mbele na ukakata nyuma pia
 
Hongereni sana kwa matokeo mazuri ya kesi yenu.
Haki ya mtu haipotei...ikipotea inatafutwa,isipopatikana inapiganiwa kwa nguvu.
 
Back
Top Bottom