Wanafunzi walishwa kinyesi na mkojo chuo kikuu Msumbiji katika hafla ya kuwakaribisha chuoni

Snipperkilungu

JF-Expert Member
Feb 16, 2018
253
423
Sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi wapya katika chuo kikuu cha Msumbiji imezua hisia kali baada ya picha kusambazwa katika mitandao ya kijamii zikioinyesha wanafunzi hao wanavyolazimishwa kunywa na kuoga mikojo na kinyesi.

Kulingana na mwandishi wa BBC Jose tembe mjini Maputo, baadhi ya wanafunzi wanaojiunga na chuo hicho cha kilimo, misitu na uhandisi cha Unizambeze katikati ya mkoa wa Zambezi pia walinyolewa.

Kulingana na runinga ya kibinafsi ya STV , sherehe hiyo ilifanyika siku chache zilizopita. Mwathiriwa mmoja , Artemiza Nhantumbo aliambia runinga hiyo kuhusu alivyoteswa.

''Waandalizi wa sherehe hiyo walitukata nywele zetu .Ilikuwa inatisha, ilikuwa haiwezikuvumilika. Walitulazimisha kula mikojo na kinyesi .

Tuliogeshwa na mikojo huku wakifuta pua zetu na vinyesi''. Mwanafunzi mwengine Quiteria Jorge, alisema kuwa mwanafunzi ambaye alikuwa katika mwaka wa pili aliwatoa katika darasa lao ili kuwafanyia sherehe hiyo ya kukera.

''Walitukata nywele zetu kwa sababu wao wanahisi ni ndefu mno, lakini hatukuweza kufanya chochote, Nililia nikalia hadi nilipofika nyumbani''. Kisa hicho hakikuwafurahisha wazazi wa wanafunzi hao ambao wamewataka wasimamizi wa chuo hicho kuwachukulia hatua hali wahusika.

Cardoso Miguel ambaye ni mkurugenzi wa elimu ya juu mkoani humo alisema kuwa uchunguzi unaendelea , ''kama tunavyoweza kuona picha katika mitandao ya kijamii ni wazi kwamba tabia hiyo haifai'' Kamati iliobuniwa itachunguza kiwango cha mateso hayo kwa kila mwanafunzi, huku wengine wakirudishwa nyumbani na wengine kufutiliwa mbali .

Sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya sio rasmi lakini hufanyika sana katika vyuo vikuu nchini humo zikiandaliwa na wanafunzi waliopo katika mwaka wa pili.

Chanzo: BBC
 
Wanafanya ubabe wa kizamani kupiga simu chooni , unapewa sh.100/= unaagizwa ununue chapati 5 na chenji irudi.
 
nchi za Africa zinamaboya wengi ...pia wanaangalia na Sura sisi marasta awawez kutufanyia ujinga kama uwo.
 
Habari kama hizi zikikosa picha hazinogi kabisa, hapa ilitakiwa tuone picha ya watoto wa chuo wakilishwa gogo.
 
Back
Top Bottom