Wanafunzi wa UDOM kufukuzwa: Chanzo cha mgogoro na Serikali inavyohusika

Mossads

New Member
May 27, 2016
4
7
Someni taarifa ya wafanyakazi udom kuhusu mgogoro wa diploma.

===========================

TANZANIA HIGHER LEARNING INSTITUTIONS TRADE UNION, UDOM BRANCH-OFFICE OF THE CHAIRMAN

MAELEZO YA KINA KUHUSU UFUNDISHAJI WA DIPLOMA YA SAYANSI, HESABU NA TEHAMA

1. Utangulizi

Kuanzia Novemba 2014, Chuo Kikuu cha Dodoma kilianza kupokea wanafunzi wa kusomea stashahada maalum ya diploma ya Elimu, Sayansi, Hisabati na Tehama (DE-SMICT). Lengo kubwa la programu hii maalum ni kutimiza azma ya serikali kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la walimu wa sayansi katika shule za sekondari nchini. Serikali iliamua kuwaleta wanafunzi hawa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) badala ya kupeleka kwenye vyuo vya ualimu ikiamini kwamba UDOM kuna miundombinu ya kutosha hasa majengo na rasilimaliwatu ya kutosha kuweza kuhifadhi wanafunzi hao. Menejimenti na jumuiya nzima ya UDOM iliona ni heshima kupewa jukumu hili na kulipokea kwa mikono miwili. Kukubaliwa na kupokelewa jukumu hili UDOM ililazimika kujipanga upya kimkakati, kimfumo pamoja na kufanya mabadiliko kadha wa kadha katika utendaji wake wa kila siku ili kuweza kuhimili jukumu hili kubwa la kitaifa. Mojawapo ya hatua zilizochukuliwa ilikuwa kuunda Kikosi Kazi (Steering Committee- SC) cha kushauri namna ya kukabili jukumu hili.

1.1 Kuundwa Kamati Maalum ya Uratibu (Steering Committee-SC)

Kuundwa kamati ya kuratibu ufundishaji wa wanafunzi hawa (SC) ulionekana kuwa ni muhimu sana kutokana na ukweli kwamba ni lazima kutafuta utaratibu tofauti wa utoaji taaluma kwa vijana. Kamati hiyo iliundwa kwa kuwashirikisha Koleji, Skuli na Idara zinazohusika na masomo ya sayansi, ualimu na TEHAMA.

Kwa msingi huu, Koleji za Elimu, Sayansi asilia na Kumpyuta ndizo zilizohusika katika kuunda kamati hiyo. SC iliyoundwa ilipewa jukumu la kuratibu namna bora ya kushughulikia masuala ya taaluma, malazi, nk. na kupeleka mapendekezo ngazi za juu kwa maana ya Menejimenti ya UDOM na vyombo vya maamuzi ya kitaaluma kama Udhibiti wa Ubora (Quality Assurance) na Seneti ya UDOM (Senate).

Kabla ya kuanza kufundisha, SC ilipendekeza mikakati, mifumo na mabadiliko yaliyokuwa ya msingi ili kukabili swala hili. Changamoto kubwa, ilibainika ni, ufundishaji wa hawa vijana. Masuala mengine yahusuyo malazi na malezi kwa ujumla wake yaliandaliwa ingawa hayakuwa na changamoto kubwa kama suala la

UFUNDISHAJI. Suala la ufundishaji lilihitaji jicho la pekee kwani vijana hawa waliopokelewa ndiyo kwanza wamemaliza kidato cha nne, hivyo bado ni wadogo kwa kiasi fulani na pia hawakupaswa kufundishwa kama wenzao wanaosomea masomo ya shahada na kuendelea. Ifuatayo ni mikakati ya ufundishaji iliyoshauriwa na SC-UDOM ili kuweka mazingira mazuri ya vijana hawa kusoma kwa ufanisi.

1.2 Ugawaji wa Mikondo (Streams)

Kama ilivyobainishwa hapo awali kwamba ni lazima kutafuta utaratibu tofauti, kamati ya uratibu ilijadili kwa kirefu na kwa kina namna ya kugawa wanafunzi katika mikondo inayoweza kufundishika katika misingi na maadili ya utoaji taaluma na zaidi sana kutofautisha utoaji wa taaluma kwa wanafunzi wanaosoma programu za diploma na wale wanaosoma shahada. Sababu ya pili ni kwamba, masomo ya sayansi yanahitaji uzito wa pekee tofauti na masomo ya sanaa yasiyohusisha vitendo katika maabara. Baada ya mjadala mrefu, ilikubalika kugawanywa mikondo (streams) ya ufundishaji kwa utaratibu ufuatao;

a. Masomo yote ya UALIMU yawe na wanafunzi 120 katika mkondo mmoja.

b. Masomo yote ya SAYANSI ASILIA yawe na wanafunzi 80 kwa mkondo mmoja.

c. Masomo yote ya TEHAMA yawe na wanafunzi 60 kwa mkondo mmoja

2 Kwa mtiririko huo hapo juu, ina maana kwamba kwa kila somo, itabidi wanafunzi wagawanywe katika mikondo kwa idadi iliyokubalika na si kuwarundika wote sehemu moja. Utaratibu huu ndio ulioonekana kutenda haki katika ufundishaji wa vijana hawa kwa kufuata misingi na maadili ya utoaji elimu. Kamati hii ilianza kazi vizuri. Vijana takriban 2000 walipokelewa, wakafundishwa na (semester) huhula wa kwanza ukamalizika vizuri bila migogoro mikubwa.

Pamoja na kasoro ndogo ndogo zilizojitokeza katika semester/muhula wa kwanza (2014/15), ufundishaji ulifanyika kwa ufanisi. Matatizo yalianza kujitokeza pale waalimu walipotakiwa kulipwa kwa kufanya kazi ya ziada katika ufundishaji wa hawa vijana. Kulingana na mapendekezo ya SC ambayo yalikuwa yamekubalika, kila mwalimu aliyefundisha masomo ya DE-SMICT kama somo la ziadi alitakiwa kulipwa Shilingi Milioni Moja (endapo tu somo hilo litakuwa ni ziada katika idadi ya masomo anayoruhusiwa kufundisha). Mvutano wa kuwalipa waalimu hawa ulipelekea wanafunzi kuchelewa kuanza masomo yao ya muhula wa pili kwa wiki mbili. Makamu Mkuu wa Chuo (VC) alipoligundua hili aliamuru malipo yafanyike na baada ya malipo wanafunzi walirejea madarasana na kazi ikaendelea. Mgogoro huu ulipelekea aliyekuwa mwenyekiti wa SC ambaye ni Mkuu wa Koleji ya Elimu kuondolewa katika wadhifa huu. Hatimaye Dean wa Skuli ya Elimu ya Ualimu aliteuliwa kuwa mwenyeti wa SC.

Kutokana na ufanisi uliopatikana katika mwaka wa masomo 2014/15, Serikali na UDOM waliamua kuleta tena wanafunzi wengine kwa muhula wa 2015/16. Idadi ya hawa wanafunzi ni takriban 6000. Kulingana na idadi hii kuwa kubwa mno, upatikanaji wa waalimu wa sayansi wanaoweza kuenea/kutosha mikondo yote iliyogawanywa ulishindikana.

Hali ya wingi mkubwa wa wanafunzi na upungufu mkubwa wa waalimu ililazimu kubuniwa mbinu za ziada ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaingia madarasani. Kwa maneno marahisi kabisa, kundi hili la pili lililodahiliwa na

3 kusajiliwa ambalo lilikuwa na wanafunzi takriban 6000, lilifanya UDOM

KUELEMEWA na MZIGO. Koleji na Skuli zinazohusika kuwafundisha vijana hawa zilibeba MZIGO uliowazidi kwa kilo/tani nyingi kuliko ilivyopaswa kubeba. Jedwali Namba 1 ni ushahidi wa mzigo unaobebwa na idara mbalimbali;
View attachment 352177
Kwa ushahidi uliotolewa katika jedwali Namba 1, yeyote hahitaji kutafuta elimu ya ziada kugundua kwamba idara husika zimeelemewa na mizigo ya ufundishaji. Kwa
taarifa tu, mgawanyo wa masomo ya ufundishaji ulioelezwa kwenye jedwali 1 hauhusishi masomo ya Shahada, Diploma za kawaida, Astashahada, cheti na shahada za juu. Hii inadhihirisha wazi kwamba, mzigo kwa walimu wanaofundisha masomo ya sayansi tayari umeshawazidi na bado wanahitajika kufundisha masomo mengine ya kawaida. Kwa vyovyote vile, jitihada zozote za kutafuta suluhu ya mgogoro uliopo zililazimu kuwepo na ushirikiano wa karibu kati ya Menejimenti ya Koleji husika na Utawala Mkuu wa Chuo yaani Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma (DVC-ARC) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala (DVC_PFA). THTU na UDOMASA ilishauri toka mwanzo umuhimu wa ushirikiano wa wadau mbalimbali ndani ya chuo katika kulishughulikia suala la ufundishaji wanafunzi hawa. THTU ilitoa tamko Januari 2015 kuelezea namna isivyoridhishwa na mtindo wa kushughulikia matatizo yanayojitokeza. Tunaweka nukuu mbili tu kati ya mengi ya tamko hilo ambalo lililalamikiwa sana na kufikia hatua ya kutaka kuwajibisha viongozi wa THTU. Hali iliyoelezwa mwaka jana 2015 imejirudia tena mwaka huu 2016 na kuibua mgogoro;

a. Pia kwa nyakati mbalimbali chama cha wafanyakazi (THTU-UDOM) na jumuiya ya wanataaluma (UDOMASA) mara kadhaa walishauri menejimenti ya chuo kushirikisha wafanyakazi wa kada mbalimbali katika hatua zote za maandalizi ya programu hii ili kuleta ufanisi katika kuwaandaa walimu hawa wa masomo ya sayansi.

b. Tunaishauri menejimenti ya chuo na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza kwa wanafunzi wa diploma ya sayansi kwa kuleta vifaa vya maabara, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, usafiri ndani ya chuo, na kuwa na uratibu na usimamizi ulio wazi katika kila idara na kada inayohusika moja kwa moja kuwahudumia wanafunzi hawa. Hii itasaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazoibuliwa na wafanyakazi na wanafunzi katika utoaji wa huduma.

2. Kutumia Wafanyakazi wasio wanataaluma

Kutokana na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi, kamati ya uratibu ilipendekeza kwenye menejimenti ya UDOM kwamba wafanyakazi ambao si wanataaluma lakini walisoma shahada ya masomo ya sayansi wapewe masomo ya kufundisha kwa makubaliano ya kulipwa baada ya kazi. Wazo hili lilikubalika na kutekelezwa kwa nia ya kutumia rasilimali watu iliyopo ndani ya UDOM badala ya kuwaleta watu wengine kutoka nje ya UDOM. Hata hivyo, waswahili husema,

5 shukurani ya punda ni mateke. Methali hii imejidhihirisha katika hili baada ya watu hawa walioombwa na Menejimenti ya UDOM kusaidia kupunguza upungufu wa walimu wa sayansi kuishia kupewa barua za ONYO ya kwamba walijipa majukumu yasiyowahusu.

3. Jitihaada za uongozi wa Koleji ya Sayansi Kavu na Hisabati (CNMS)

Ili kuhakikisha kuwa wanafunzi hawarudi nyumbani wala kwenda barabararani, uongozi wa CNMS ulijitahidi kuushirikisha uongozi wa chuo na kuomba msaada kila palipoonekana kuhitajika msaada huo. Baadhi ya maswala muhimu yaliyotakiwa kushuhulikiwa ni kuwaongezea uwezo wa kupata waalimu wa ziada, kupata sehemu za kufundishia na kupata vifaa vya maabara. Hata tunapoandika hivi sasa, DVC-PFA, pamoja na kupokea nyaraka mbali mbali zinazomwomba aagize vifaa na madawa ya maabara (laboratory equipments and reagents) hajanunua hata kitu kimoja. Wanafunzi wamefundishwa bila kupewa mazoezi ya vitendo yanayokidhi mahitaji kwa sababu za kiburi cha DVC-PFA. Katika jitihada za kutafuta waalimu wa ziada, DVC-ACR amekataa katakata kutoa mwongozo wa kimaandishi ama ushauri wowote utakaowasaidia viongozi wa CNMS kuboresha hali ya ufundishaji. Aliyekuwa Mkuu wa Koleji ya CNMS anaweza kuonyesha nyaraka ambazo alizituma kwa viongozi hawa wawili wa juu akiomba msaasda bila majibu. Kama kuna watu waliozembea katika kazi hii ni DVC-ARC na DVC-PFA. Kwa mdomo, DVC-ARC alimshauri aliyekuwa Mkuu wa CNMS atumie sera ya uzito wa kazi kutatua suala la uhaba wa waalimu. Hili lisingaliwezekana.

4. Sera ya Uzito wa Kazi (waorkload policy)

UDOM imetengeneza sera ya uzito wa kazi (Workload Policy) ili kusimamia utekelezaji wa utoaji wa taaluma ndani ya chuo. Sera hii ilitokana na; pamoja na mambo mengine, usumbufu mkubwa ulioletwa na walimu wa muda (part time instructors) kutoka vyuo vingine waliokuwa wanapewa mikataba ya kufundisha kuziba pengo la uhaba wa walimu. Sera hii imesaidia sana kupunguza adha iliyokuwa inatokea kabla ya kutengenezwa kwake. Sera hii imeeleza kwa uwazi wa namna ya kugawa uzito wa kazi kwa kila mwanataaluma kama ifatavyo;

6 a. Mkufunzi Msaidizi (Tutorial Assistant - TA) ambaye hana likizo ya masomo lazima afundishe somo moja la diploma na kusimamia semina ya shahada. Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe

b. Mkufunzi Msaidizi (Tutorial Assistant - TA) ambaye ana likizo ya masomo lazima afundishe somo moja la diploma au cheti. Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe

c. Mhadhiri Msaidizi (Assistant Lecturer – AL) ambaye hana likizo ya masomo lazima afundishe masomo mawili ya shahada. Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe

d. Mhadhiri Msaidizi (Assistant Lecturer – AL) ambaye ana likizo ya masomo lazima afundishe somo moja la shahada. Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe

e. Mhadhiri (Lecturer), Mhadhiri Mwandamizi (Senior Lecturer) na Profesa ambaye hana majukumu ya madaraka lazima afundishe masomo matatu kuanzia ngazi ya shahada. Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe.

f. Mhadhiri (Lecturer), Mhadhiri Mwandamizi (Senior Lecturer) na Profesa ambaye ana majukumu ya madaraka lazima afundishe somo moja kuanzia ngazi ya shahada. Akipangiwa somo la ziada lazima alipwe.

g. Ukubwa wa darasa (class size) itashughulikiwa na kila Koleji lakini

hairuhusiwi kugawa darasa moja zaidi ya mara tatu hata kama lina wanafunzi zaidi ya 3000.

h. Kuhusu mapato yatokanayo na programu zote ambazo si za shahada (Non degree Programs), sera inatamka kwamba 70% ya mapato hayo yapelekwe kwenye Koleji husika ili kuimarisha utoaji wa taaluma. 30% inabaki utawala mkuu kwa ajili ya shughuli muhimu kama utoaji vyeti na mengine.

Tumeamua kutaja sera hii ili kuonesha namna ambavyo isingewezekana kutumika kushughulikia ufundishaji wa wanafunzi wa DE-SMICT ambao wanahitaji uangalizi wa pekee. Hii itasaidia kuondoa upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu ndani ya menejimenti ya UDOM kwamba Diploma husika inaweza kuhudumiwa kwa kutumia sera hii. Limekuwepo jaribio kubwa la Menejimenti kulazimisha jambo hilo

7 litokee kwa sababu wanataka kukumbatia mapato yanayotokana na Diploma hiyo huku wakiwadhulumu wanafunzi na waalimu kwa KUKATAA KUANDAA

MAZINGIRA MUAFAKA YA KUFANYA KAZI HII.

DVC-PFA na DVC-ARC wanalazimisha sera hii itumike pale wanapotaka kukwepa jukumu la kununua vifaa vya kufundishia, kukwepa kuwalipa waalimu na kulazimisha ULIPUAJI KAZI. DVC-ARC na DVC-PFA hawataki kabisa kukumbuka sera hii inaafiki kutolewa asilimia 70% ya mapato kwa Koleji husika.

5. Mgogoro Uliosababisha Wanafunzi kutofundishwa

Kutokana na maelezo yote hapo juu, jambo moja linajitokeza hapa, Koleji zinazofundisha DE-SMICT zimezidiwa na kazi hasa CNMS na Koleji ya Elimu (CoEd). Kutokana na kuzidiwa huko, hivi majuzi imeibuka mgogoro uliopelekea wanafunzi kutofundishwa. Mgogoro huu unafana na ule wa kipindi cha masomo cha mwaka 2014/15 uliopelekea SC kuundwa upya kama ambavyo nukuu mbili zimewekwa hapo juu. Sisi chama cha wafanyakazi (THTU) tawi la UDOM, tunaamini kwamba mgogoro huu umesababishwa na mambo yafuatayo;

5.1 Utamaduni wa bora liende unaolazimishwa na DVC-PFA pamoja na DVC-ARC

Katika mgogoro huu, DVC ARC na DVC-PFA wamekataa katakata;

1. Kununua vifaa vya maabara kwa ajili ya kufundisha waalimu hawa wa sayansi;

2. Kuusaidia uongozi wa CNMS na CoEd kupata waalimu kwa idadi inayokidhi mahitaji;

3. Kutoa ushirikiano wa hali na mali ili kuhakikisha kazi inafanyika katika ubora unaowezekana na kukubalika;

4. Kuwalipa waalimu kila inapotakiwa kufanya hivyo; Na;

5. Kusema ukweli kwa Waziri, Katibu Mkuu na Watanzania kuhusu hali halisi ya uendeshaji wa mafunzo haya.

8 Uzembe huu wa DVC-PFA na DVC-ARC pamoja na kiburi cha makusudi ndiyo chanzo cha hali ilivyo hivi sasa ambapo takriban kwa WIKI TATU SASA WANAFUNZI HAWA WA DE_SMICT WANAOCHUKUA MAFUNZO CNMS na CoED HWAJAINGIA MADARASANI.


Imedhihirika pasipo shaka kwamba viongozi hawa wawili bila kujali uharabifu unatokea kwa wanafunzi, chuo na Taifa kwa jumla wanapendelea utendaji kazi na utamaduni wa BORA LIENDE pale wanapotakiwa kuwajibika.

Badala ya kufanya kazi hii kwa ari, weledi na uaminifu kama ilivyostahili, viongozi hawa wawili wameamua kuwa waongo, wasiojali maslahi ya wanafunzi na umma na taasisi wanayoiongoza katika ujumla wake. Badala ya kushirikiana na wahusika kutatua changamoto zinazojitokeza, wameamua kukaa ofisini na kutafuta suluhisho kwa njia ya simu na kuandika barua. Kikubwa kinachokifanywa na DVC-ARC pamoja na DVC-PFA ni kutoa taarifa za uongo kwa viongozi wa Serikali waliojaribu kuingilia hili swala ili kunusuru hali kwa kubambikia watu wasiowapenda makosa na kuanza kushughulika nao badala ya kutatua taizo.

Ni vema tukaweka kumbukumbu sahihi kwamba, Makamu Mkuu wa Chuo Prof

Idriss Kikula tunamtoa katika hili. Tunaamini yeye binafsi angekuwepo, suala hili lisingefika hapa tulipo sasa. Yapo matukio yanayoonesha kwamba tangu mwanzo wa kudahiliwa wanafunzi, DVC-ARC na DVC-PFA hawajawahi kuwa na nia njema ya kuona mambo yanakwenda vizuri. Baadhi ya mambo hayo ni

a. Kumdanganya aliyekuwa waziri wa Elimu Dr. Shukuru Kawambwa kwamba vifaa vya kutosha vipo wakati ni uongo mkubwa. Hili ni bora liende.

b. Kudiriki kulazimisha Diploma hii maalum iingie kwenye mfumo wa kawaida ya utoaji elimu wakati ilishaelezwa toka awali kwamba hii ni programu maalum, hili pia ni bora liende.

c. Kutokuwa tayari hata siku moja kukaa meza moja na walimu wanaofundisha masomo hayo ili kufahamu tatizo la ziada. Badala yake wanamlazimisha Mkuu wa Koleji kutatua mgogoro bila kumpa nyenzo, Bora liende linahusika

9 d. Kukiuka makubaliano halali yaliyofikiwa ya kuunda kamati ya kushughulikia mgogoro huu wakati Naibu Waziri Elimu na Katibu Mkuu walipokuja UDOM. Menejimenti ya UDOM ilikataa majina yaliyopendekezwa na UDOMASA kuingia kwenye kamati na kuwachagua watu wao inaowafahamu kuwakilisha UDOMASA. Hii peke yake inaonesha dhahiri kwamba hawana chembe ya nia kutatua mgogoro isipokuwa bora liende.

e. Kusimamia misingi ya ubabe, vitisho, dharau na kutojali pale inapofuatwa na viongozi wa UDOMASA na THTU kuangalia namna ya kupata suluhu ya mgogoro. Pia hii inaonesha utamaduni wa bora liende.

Haya ni machache tu yanayohusu swala hili. Hitimshoi ni kwamba;

1. Kwa ujumla wake, kazi hii ya kuendesha programu hii ya DE-SMICT imefanyika vibaya na kizembe kwa makusudi. (Hakuna vifaa vya maabara, hakuna waalimu wa kutosha, hakuna vyumba vya kufundishia vya kutosha)

2. DVC-ARC na DVC-PFA katika wajibu wao kama makaimu wa VC wameamua kuboronga hii kazi zaidi ya ilivyokuwa imeborongwa na kupelekea wanafunzi kutokuingia madarasani kwa WIKI TATU hivi sasa.

3. DVC-ARC na DVC-PFA wameamua kuwadanganya viongozi wa Serikali na

umma wa Watanzania kuhusu chanzo cha mzozo uliopelekea wanafunzi kutokuingia madarasani kwa wiki tatu sasa.

THTU imeamua kuuweka ukweli huu wazi ili hatua za kusahihisha swala hili zichukuliwe kwa haraka. Endepo ukweli huu hautazingatiwa, basi hatua zitakazochukuliwa hazitakidhi hali halisi.

DVC-ARC na DVC-PFA wanatakiwa kuwajibishwa kwa uzembe huu wa makusudi. THTU inaomba DVC-ARC na DVC-PFA walazimishwe kuwaonyesha viongozi wa Serikali nyaraka zote zilizotoka CNMS zikiomba ushirikiano wa kuwawezesha CNMS kutimiza majukumu yao katika hili swala ambazo hawakujali kuzijibu.

10 Mwisho kabisa;

THTU inaomba kuwa, kwa yeyote asiyeamini hii hali, yaani UGUMU WA KUPANGA RATIBA INAYOKIDHI MAHITAJI, basi atume wataalamu kutoka popote waje UDOM kupanga ratiba kwa ajili ya DE-SMICT kama inavyoagizwa na DVC-ARC ili tuweze kuona kama itaweza kukidhi mahitaji. Kwa hali ilivyo HAITOWEZEKANA!
 

Attachments

  • taarifa ya chama cha wafanyakazi.pdf
    317 KB · Views: 157
  • Mdahalo wa BBC , Ndalichako, nk1.aac
    4 MB · Views: 92
  • Mdahalo wa BBC, Ndalichako, nk2.aac
    4.2 MB · Views: 82
Juzi juzi tu, nimesoma taarifa ya Prof. Mkandara wa UDSM akiwasema walimu kutanguliza maslahi yao mbele kuliko taaluma zao kwa ziara za kila mara kutoka chuo hadi chuo. Mimi ambaye si mwalimu wa chuo (lakini niliyefanya kazi za kiutawala kwenye vyuo) naamini pamoja na matatizo mengine ya uhaba wa pesa serikalini, kwa sasa hivi walimu wengi wa vyuo hawana uzalendo. Wanataka kulipwa pesa kubwa hata kwa kazi ndogo waliofanya au kutofanya kabisa. In fact ni trend ambayo ipo katika sekta zote nchini. Kila mtu anataka kujenga ghorofa na kuendesha SUVs. Tulikuwa tukiambiwa kwamba kazi ya udaktari na ualimu ni kazi za wito. That's gone forever. Pamoja na matatizo mengine yaliyo andikwa katika attachment, tatizo la mgogoro huu ni maslahi. Period.
 
Juzi juzi tu, nimesoma taarifa ya Prof. Mkandara wa UDSM akiwasema walimu kutanguliza maslahi yao mbele kuliko taaluma zao kwa ziara za kila mara kutoka chuo hadi chuo. Mimi ambaye si mwalimu wa chuo (lakini niliyefanya kazi za kiutawala kwenye vyuo) naamini pamoja na matatizo mengine ya uhaba wa pesa serikalini, kwa sasa hivi walimu wengi wa vyuo hawana uzalendo. Wanataka kulipwa pesa kubwa hata kwa kazi ndogo waliofanya au kutofanya kabisa. In fact ni trend ambayo ipo katika sekta zote nchini. Kila mtu anataka kujenga ghorofa na kuendesha SUVs. Tulikuwa tukiambiwa kwamba kazi ya udaktari na ualimu ni kazi za wito. That's gone forever. Pamoja na matatizo mengine yaliyo andikwa katika attachment, tatizo la mgogoro huu ni maslahi. Period.
Walipeni, nyie si mmeamua kuwalipa vizuri wanasiasa tena wanaojua kusoma na kuandika tu, wao wafanyeje, wapeni hela zao
 
Hivi huyu jamaa ni nani Nchi hii, huyu jamaa UDOM kama shamba lake, anaamua anavyotaka, Siku zote yeye ndo amekuwa chanzo cha matatizo.

Lakini wala huwezi sikia anaguswa, kuna sehemu nimekutana na taarifa ya wafanya kazi wa UDOM wakidai yeye ni mmoja wa matatizo yanayotokea sasa!
 
Juzi juzi tu, nimesoma taarifa ya Prof. Mkandara wa UDSM akiwasema walimu kutanguliza maslahi yao mbele kuliko taaluma zao kwa ziara za kila mara kutoka chuo hadi chuo. Mimi ambaye si mwalimu wa chuo (lakini niliyefanya kazi za kiutawala kwenye vyuo) naamini pamoja na matatizo mengine ya uhaba wa pesa serikalini, kwa sasa hivi walimu wengi wa vyuo hawana uzalendo. Wanataka kulipwa pesa kubwa hata kwa kazi ndogo waliofanya au kutofanya kabisa. In fact ni trend ambayo ipo katika sekta zote nchini. Kila mtu anataka kujenga ghorofa na kuendesha SUVs. Tulikuwa tukiambiwa kwamba kazi ya udaktari na ualimu ni kazi za wito. That's gone forever. Pamoja na matatizo mengine yaliyo andikwa katika attachment, tatizo la mgogoro huu ni maslahi. Period.

Yes, yawezekana ikawa ni maslahi. Lakini si ndivyo ilivyokubaliwa kwa kutumia utaratibu husika na kila upande (mlipaji na mlipwaji) kuridhia?

Ni kwa nini sasa upande mmoja hasa hasa ule unaopaswa kulipa ukiuke makubaliano halali?

Well, tuchukulie mfano hawa walimu wanaowafundisha wanafunzi hawa waanze kudai kulipwa huku wakiwa hawakufanya kazi yao kabisa au waliifanya isivyokikamilifu, mlipaji angewalipa kweli??

The opposite ni kwamba, mtu kafanya kazi yake kikamilifu basi ni sharti alipwe sawa sawa na makubaliano/mkataba wake. Kinyume chake ni kuwa mtaingia ktk mgogoro tu iwe isiwe!

Hapa hakuna cha uzalendo wala nini. Makubaliano ni sharti yaheshimiwe.

Hata wewe unafanya kazi ili ulipwe not anything else...!!
 
Hapa kinachotoke ni kutaka kuwaangushia zigo DVC-ARC na DVC-PFA yaani kinabo na mlacha respectivelly sasa tatizo hapo ni serikali kwanini haikuwalipa mishaara waadhiri ili waendelee kufundisha? Mm nasema hv ni swala la mda tuu utawala wa jakaya mrisho utakuwa bora
 
...acheni kuingiza siasa vyuoni....walipeni wakufunzi kama mlivyoamua kuwalipa vizuri wanasiasa(wabunge) wenu...basi walipeni vema waalimu vyuoni....kama mnataka taifa la wasomi basi kupanga ni kuchagua...acheni siasa...walipeni wakufunzi ili wawafundishie watoto wenu....TZ inasumbuliw na ugonjwa sugu wa kufanya siasa kwenye kila kitu....lipeni vizuri waalimu wenu...acheni siasa wabongo....ndio maana kila mtu siku hizi anakimbilia siasa.....mnapowalipa wanasiasa wenu kuliko wataalm mnategemea nini?..
 
Hapa kinachotoke ni kutaka kuwaangushia zigo DVC-ARC na DVC-PFA yaani kinabo na mlacha respectivelly sasa tatizo hapo ni serikali kwanini haikuwalipa mishaara waadhiri ili waendelee kufundisha? Mm nasema hv ni swala la mda tuu utawala wa jakaya mrisho utakuwa bora
Tatizo si mshahara bali malipo ya ziada. Nashangaa wanasakamwa wasaidizi wakati kuna VC ambaye ndiye aliyekabidhiwa Chuo Na serikali. Kuna shida hapa
 
Hapa kuna vurugu nyingi sana na chanzo cha yote ni kulazimisha kuingiza chuoni mambo ambayo hayana utaratibu unaoeleweka... Yani source ni hao wanafunzi kukosa vigezo mbona wengine hawasumbui... Ukishavunja utaratibu kila kitu kitaenda hovyo Ndalichako ni kama anajaribu kutibu kansa iliyosambaa tayari anaonekana kama anataka kuua mgonjwa.
 
405337294203e520fd37dbec5bea2c83.jpg
 
#Hoja_Ya_Wanafunzi_wa_UDOM
Watu wengi wanaohoji nini kiini cha tatizo la wanafunzi wa UDOM? Wamefanya nini? Kwanini wamefukuzwa? Kwanini iwe usiku wa manane? Nini hatma yao?

#Majibu
Mgogoro huu una historia ndefu kidogo. Miaka michache iliyopita aliyekua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete alizindua program maalumu ya kusomesha waalimu wa masomo ya sayansi ktk shule za sekondari nchini. Hii ilikua ni program maalumu ya kukabiliana na changamoto ya uhaba wa waalimu wa sayansi nchini.

Ilionekana kuwa wastani wa waalimu 8,000 wa masomo ya Sayansi wanaweza kusaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ukosefu wa waalimu wa Sayansi nchini. Lakini hakukua na chuo cha waalimu chenye kuweza kudahili walimu wote hao. Hata wizara ingeamua kuwagawanya kwny vyuo vya ualimu vya diploma wasipata nafasi za kutosha.

Hivyo basi Rais Kikwete kwa kushirikiana na mamlaka ya Elimu (TEA), Tume ya vyuo vikuu(TCU), Mamlaka ya elimu ya ufundi (NACTE) na wadau wengine wakafikia maazimio ya kudahili wanafunzi hao chuo kikuu cha Dodoma baada ya kufanyika assesment na kuonekana nafasi zipo za kutosha wanafunzi wote hao.

Lakini ili kuepuka kupata walimu "wasio na sifa" serikali ikaset standards za udahili, kwamba itakua ni kwa wahitimu wa kidato cha 4 waliopata daraja la kwanza hadi la tatu (division 1 hadi 3) na pia wawe wana ufaulu wa alama "A" au "B" katoka masomo ya sayansi. . Lakini je unawezaje kumshawishi Mwanafunzi aliyepata Division 1 au 2 aende kusomea Ualimu wa sayansi ngazi ya Diploma? Wengi wana malengo tofauti na wangependa kuendelea na kidato cha 5 na hatimaye chuo kikuu kama "priority number 1".

Kwahiyo serikali ikaona njia rahisi ni kuwapatia mikopo ya 100% wanafunzi hao na kuwaahidi ajira pindi wamalizapo masomo. Kwa hali hii wakafanikiwa kuwashawishi hasa wale watoto wa maskini wasio na uwezo wa kujisomesha "private". Hawa wajajikuta wamekua wahanga wakuu wa mfumo huu. Wakakubali kujiunga na Program hii maalumu kwa kuwa wana uhakika watapata mkopo na wamehakikishiwa ajira baada kuhitimu. Lakini wale watoto wa vigogo waliofaulu kwa division 1 na 2 hawakua na muda wa kupoteza kwny programu hii. Wakaenda kidato cha 5 na 6 kwenye shule nzuri za binafsi zenye kulipiwa mamilioni.

Watoto wa mama Ntilie waliofaulu vizuri wakadahiliwa UDOM tayari kuianza safari yao ya kuwa waalimu (Diploma in Education - Special Program). Program hii ilizinduliwa na Rais Kikwete kwa pesa zilizoombwa bungeni kisheria. Bunge liliridhia kuwasomesha vijana hao kwa gharama za serikali ili wakafundishe O-level katika shule za serikali ktk kulabiliana na changamoto ya walimu wa Sayansi nchini. Programu hii ilienda vizuri tangu kuanzishwa kwake hadi serikali ya Magufuli ilipoingia madarakani.

#Kiini_cha_Mgogoro
Serikali ya Magufuli ilipoingia madarakani kwanza ikasitisha kupeleka fedha kwenye program hii, hali iliyopelekea wahadhiri waliokua wakifundisha kukosa, posho walizokuwa wakipata. Hali hii ilipelekea wahadhiri hawa kukagoma kufundisha. Walidai kwamba mikataba ya ajira zao haihusishi ufundishaji wa course hiyo, kwa hiyo inabidi walipwe posho ya ziada. Serikali ikakataa. Wahadhiri wakagoma na wanafunzi wakaungana nao kugoma.

Punde si punde serikali ikasitisha mikopo kwa wanafunzi hawa kwa madai kuwa wanafunzi wa kidato cha nne hawana sifa ya kwenda chuo kikuu, na hata wakienda kwa "equivalent pass" hawastahili kupewa mkopo kwa mujibu wa sera ya mikopo. Yani hoja ikahama kutoka kugoma hadi kukosa sifa zakusoma. Mgogoro ukawa mkubwa zaidi pale serikali ilipowafukuza kazi viongozi wakuu wa TCU eti kwa kudahili wanafunzi "wasio na sifa" chuo kikuu. Serikali ikastaajabu eti wanafunzi wa kidato cha 4 wamefikaje chuo kikuu na kupata mkopo asilimia 100%??

Serikali ikaenda Bodi ya Mikopo na kufukuza Watendaji wote walioshiriki kuwapa mikopo vijana hawa. Vyombo vya habari navyo vikaandika kishabiki bila hata kufanya utafiti eti "Wanafunzi vihiyo chuo kikuu waanza kukiona", wengine wakaandika "Waliowapa mkopo wanafunzi vihiyo wafukuzwa". Yani kila mwandishi akaandika lake kuonesha kufurahishwa na uamuzi huo wa serikali. Lakini ni waandishi hawahawa walioandika miaka miwili iliyopita kuwa "Waliofaulu vizuri sekondari kupewa mkopo 100% kusomea ualimu wa sayansi". Leo vijana walewale waliotajwa kufaulu vizuri na serikali ya JK ikapongezwa kuwaanzishia program maalumu, ndio wanaitwa "vihiyo" na waandishi walewale waliowasifia.

Hivi mtu aliyepata division 1 au 2 na akafaulu masomo ya Sayansi kwa alama A au B miaka miwili iliyopita leo anakuaje "kihiyo??". Wanafunzi hawa waliofaulu vizuri masomo yao ya O-level wakaitwa "magenius" na kuombwa wakasomee ualimu leo wanaitwa "vihiyo" na serikali ileile. Leo serikali ya chama kilekile iliyokuja na mpango huu, kupitia wizara ileile inawafukuza viongozi wa TCU waliowadahili wanafunzi hawa. This is typical unfair.

Mbaya zaidi hawakuishia hapo; wakakwenda chuoni na kusitisha mishahara ya wahadhiri. Hawakuishia hapo wakazuia mikopo ya wanafunzi hawa kutoka familia duni. Hawakuishia hapo, hatimaye jana usiku wakawafukuza wanafunzi hawa wasio na hatia. Hakika nimeshindwa kuelewa kabisa jambo hili. Yani serikali ya JPM inataka dunia iamini kuwa serikali iliyopita ni nyingine kabisa na haina mazuri iliyoyafanya na ilikua inaongozwa wajinga?? Ina maana mtangulizi wake hakumueleza juu ya programu hii maalumu ya kuongeza idadi ya walimu wa sayansi nchini? Kama alielezwa mbona anafanya maamuzi kwa kukurupuka?

Yericko Nyerere anahoji kuwa; inawezekanaje Katika bunge lilelile na spika wa chama kilekile wanazuia hoja binafsi ya Mbunge Joshua Nassari aliyetaka bunge lijadili mgogoro huu na kunusuru hatari inayowakumba watoto wetu hapo UDOM?? Badala yake mbunge huyo ananyanyuliwa mzobemzobe na polisi na kutupwa nje ya lango la bunge. Vijana hawa wamefukuzwa jana usiku na kupewa notice ya masaa 24 wawe wameondoka ndani ya eneo la chuo, huku magari ya polisi, na polisi wenye silaha, mabomu ya machozi na maji ya kuwasha wakiwa wamezingira maeneo ya chuo hicho tangu usiku.

Wamefukuzwa kama mbwa bila hata kusikilizwa. Wamelazimishwa warudi makwao bila kupewa hata nauli. Watarudije? Baadhi ya wanafunzi kutokana na kuhofia usalama wao walifungasha mizigo yao na kwenda kujilundika stand ya mabasi Dodoma wakiwasiliana na ndugu zao wawatumie nauli. Polisi wakawavamia leo asubuhi na kuanza kuwapiga wakiwashinikiza waondoke Dodoma haraka. Lakini wataondokaje bila nauli? Kama serikali inajali utu kwanini isiwakodishie mabasi yawarudishe kwao? Mbona Mwalimu Nyerere alipowafukuza kina Samuel Sitta UDSM alitoa mabasi yaliyowapeleka hadi majumbani kwao? Serikali hii ya JPM inashindwa nini?

Mwanafunzi aliyeamua kujisitiri stand ya mabasi akihofia asije kufia chuoni peke yake, hana ndugu Dodoma, hana nauli ya kurudi kwao, anapiga simu kwa ndugu zake wamtumie nauli. Amelala kwa kusimama na kuumwa mbu hadi asubuhi inafika hajapata nauli. Polisi wanamkuta na kuanza kumpiga eti kwanini yuko stand na hataki kusafiri. Huu ni ukatili mkubwa sana dhidi ya binadamu. Mahali pekee ambapo wanafunzi hawa wanaweza kupata haki yao kwa sasa ni Bungeni tu. Serikali imeshawakana wakati ndio iliyoanzisha hiyo programu. Maafisa wa TCU waliowadahili wameshafukuzwa. Viongozi wa Bodi ya Mikopo waliowapa mikopo nao wamefukuzwa. Tumaini pekee la maisha yao limebaki bungeni.

Halafu Mbunge Nassari analeta hoja ya kujadili suala hili kwa dharura Naibu Spika anakataa, anaagiza Polisi wamtoe nje Nassari. This is very unfair. Wanafunzi hawa wamekua "valnurable" na wako kwenye hatari nyingi ikiwa ni pamoja na kubakwa (kwa wale wa kike) au kufanyiwa vitendo vya kihuni hata kuuawa. Wanahitaji msaada wa dharura ili waweze kujua hatma yao. Na mahali pekee pa kupata msaada huo ni bungeni, lakini Naibu Spika hataki. Anasema hoja hiyo siyo ya dharura. Huu ni unyama. Ni ukatili. Ni Ukosefu wa utu. Ni ushetani. Yani wadogo zetu wafie Dodoma halafu tuambiwe si dharura? Hivi huyu mama amezaa? Ingekua wanae ndio wapo kwenye mazingira hayo angefanya hivyo?

Kwanini tunawaadhibu watoto hawa kwa makosa ambayo hawajafanya. Kama ni kukosea basi aliyekosea ni JK na serikali yake, kwanini Magufuli awaadhibu hawa watoto wasio na hatia? Nini hatma yao? Wengine wako mwaka wao wa mwisho kumaliza elimu yao ina maana wamepoteza muda bure? Nani atawalipa muda waliopoteza? Leo ni vijana hao hao kama wangeamua kwenda kidato cha tano wangekuwa wamemaliza form six mwaka jana na sasa wapo first year chuo kikuu na wengine wangekua wanasubiri kujiunga first year mwaka huu. Wapo waliokua na ndoto za kuwa maribani, madaktari, wahandisi lakini walijitolea maisha yao na kuamua kwenda kusomea ualimu kwa ajili ya Tanzania; licha ya kufaulu kwa division one na two. Leo wanafukuzwa kama mbwa na Polisi wenye silaha.
 
Umenena vyema sana mkuu, hakika lengo la hawa viongozi lilikuwa jema sanaa. Lakini naomba ujaribu kuulizia kwa kufanya utafiti kidogo, kati ya hao wanafunzi 7000 ni wangapi walikuwa na hizo sifa tajwa hapo juu? Ni wangapi walikuwa na As and Bs katika masomo hayo ya science? Kaulize uambiweee!!! Nimefanya utafiti mkuu na ingawa ukweli unauma lakini lazima usemwe, kwenye kudahili hao wanafunzi asilimia 98% hawakuwa na sifa tajwa, wengi walikuwa na daraja la tatu, na sana sana utakuta kapata C masomo ya art na D ya hesabu. Na ikumbukwe hizi C na D tunazosema hapa sio hizi tulizopata mm na ww, ni hizoo za mwaka 2013 za distinction na credit. Hampendi kuambiwa ila ukweli ni kwamba VIJANA HAO HAWAKUWA NA HIZO SIFA ZA KUSOMEA DIPLOMA YA SCIENCE
 
Kama kulikuwa na makubaliano na serikali. Wabunge waliotaka kulipeleka bungeni wawasaidie kuanziasha harambee ya kwenda Mhakamani kudai haki zao. Mimi nipo tayari kuchangia?
 
Umenena vyema sana mkuu, hakika lengo la hawa viongozi lilikuwa jema sanaa. Lakini naomba ujaribu kuulizia kwa kufanya utafiti kidogo, kati ya hao wanafunzi 7000 ni wangapi walikuwa na hizo sifa tajwa hapo juu? Ni wangapi walikuwa na As and Bs katika masomo hayo ya science? Kaulize uambiweee!!! Nimefanya utafiti mkuu na ingawa ukweli unauma lakini lazima usemwe, kwenye kudahili hao wanafunzi asilimia 98% hawakuwa na sifa tajwa, wengi walikuwa na daraja la tatu, na sana sana utakuta kapata C masomo ya art na D ya hesabu. Na ikumbukwe hizi C na D tunazosema hapa sio hizi tulizopata mm na ww, ni hizoo za mwaka 2013 za distinction na credit. Hampendi kuambiwa ila ukweli ni kwamba VIJANA HAO HAWAKUWA NA HIZO SIFA ZA KUSOMEA DIPLOMA YA SCIENCE
skia mkuu.. You can have reason and that's why wabunge wanataka walijadili Hilo swala ili kujua muafaka WA dharura WA kuweza kuwasaidia vijana... But that naibu spika of yours hataki swala lijadiliwe why??? Kwani wacongo hao wanafunzi?? SI Ni watanzania wenzetu?? Na even if wanamatokeo mabaya nani alaumiwe?? Wao? Serikali?? Au waliopewa dhamana ya kuwadahili?? Jamani tatizo linaweza kuwa tatizo au ndani yake Kuna tatizo zaidi but kujadiliwa na kutolewa muafaka ndo jambo la muhimu na busara but why they don't want to discuss this matter In the parliament!!!!!!!????? So fu*****kkk
 
Umenena vyema sana mkuu, hakika lengo la hawa viongozi lilikuwa jema sanaa. Lakini naomba ujaribu kuulizia kwa kufanya utafiti kidogo, kati ya hao wanafunzi 7000 ni wangapi walikuwa na hizo sifa tajwa hapo juu? Ni wangapi walikuwa na As and Bs katika masomo hayo ya science? Kaulize uambiweee!!! Nimefanya utafiti mkuu na ingawa ukweli unauma lakini lazima usemwe, kwenye kudahili hao wanafunzi asilimia 98% hawakuwa na sifa tajwa, wengi walikuwa na daraja la tatu, na sana sana utakuta kapata C masomo ya art na D ya hesabu. Na ikumbukwe hizi C na D tunazosema hapa sio hizi tulizopata mm na ww, ni hizoo za mwaka 2013 za distinction na credit. Hampendi kuambiwa ila ukweli ni kwamba VIJANA HAO HAWAKUWA NA HIZO SIFA ZA KUSOMEA DIPLOMA YA SCIENCE
Kwa majibu haya sijui kama kuna mtu ataendeleza mjadala huu. Umemaliza Mkuu
 
Back
Top Bottom