DOKEZO Wanafunzi wa kidato cha tano kukataliwa kisa hawajamaliza michango ni usumbufu kwa wanaotoka mbali

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mawele

Member
Jul 25, 2023
30
116
Habari, nawasalimi kwa jina la muungano......

Nina kero yangu haswa kwa shule za advance wanaopokea kidato cha tano walimu wakuu wanachukua maamuzi ya kumkataa mtoto kumpokea ikiwa tu hajamaliza michango na vifaa vingine kama vile vya usafi ukiangalia umbali uliotoka na mtoto ni mbali sana.

Mfano mimi mwanangu kupangiwa Kibaigwa Girls iliyopo Dodoma mwalimu mkuu na makamo Mkuu wa shule wamenigomea kumpokea mtoto kisa nimelipia nusu ya pesa za michango na sijakamilisha vifaa vya usafi ukizingatia nimetokea mkoa wa Mtwara sijui cha kufanya, naomba waziri husika kufuatilia hili jambo wazazi tunashindwa kuwapeleka shule mapema watoto kutokana na hizi changamoti. Naomba kuwakilisha🤝
 
Back
Top Bottom