Wanafunzi wa darasa la saba wanatarajia kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kesho

Ryan Herman

Member
Jul 26, 2019
42
46
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde
Dar es Salaam. Wanafunzi 947,221 wa darasa la saba kutoka shule 17,051 za Tanzania bara, wanatarajia kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kesho Jumatano na keshokutwa Alhamisi Septemba 12, 2019.

Kati ya watahiniwa hao, wavulana ni 451, 235 sawa na asilimia 47.64 na wasichana ni 495, 986 sawa na asilimia 52.36.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo Jumanne Septemba 10,2019 jijini Dar es Salaam wakati akitangaza kuanza kwa mitihani hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde amesema masomo matano yatatahiniwa katika mitihani hiyo ambayo ni Kiswahili, Kiingereza, Sayansi, hisabati na maarifa ya jamii.

“Kati ya watahiniwa 947, 221 waliosajiliwa kufanya mitihani hiyo mwaka 2019, watahiniwa 902, 262 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 44, 959 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiingereza ambayo wamekuwa wakiitumia katika kujifunzia,” amesema Dk Msonde

Amesema watahiniwa wenye mahitaji maalumu wapo 2,678 ambapo kati yao 81 ni wasioona, 780 wenye uoni hafifu, 628 wenye ulemavu wa kusikia, 325 ni wenye ulemavu wa akili na 864 ni wenye ulemavu wa viungo vya mwili.

“Maandalizi kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa karatasi za mitihani, fomu maalumu za ‘OMR’ za kujibia mtihani na nyaraka zote muhimu zinazohusu mtihani huo katika halmashauri na manispaa zote nchini,” amesema Dk Msonde

Katibu mtendaji huyo amewataka wamiliki wa shule wote kutambua shule zao ni vituo maalumu vya kufanyia mtihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi.

“Baraza halitosita kuendelea kukifutia kituo chochote cha mitihani endapo litajidhilisha pasipo na shaka kuwa uwepo wake unahatarisha usalama wa mitihani ya Taifa,” amesema Dk Msonde
 
Nawatakia mitihani myema akiwemo my first born anafanya mtihsni hio kesho maombi yenu muhimu mnoo jamani
 
MUNGU amsaidie mwanangu jamani amalize mitihani yake salama na amtie nguvu na afya njema katika kipindi hiki muhimu Sana aweze kufanya mitihani yake na kufaulu vizur Amina
 
....

“Kati ya watahiniwa 947, 221 waliosajiliwa kufanya mitihani hiyo mwaka 2019, watahiniwa 902, 262 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 44, 959 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiingereza ambayo wamekuwa wakiitumia katika kujifunzia,” amesema Dk Msonde
....

... 95% kati ya hao 44,959 wana uhakika wa kufika vyuo vikuu wakati hao wengine zaidi ya 95% vyuo vikuu wataishia kuvisikia tu maishani mwao! Not fair!
 
Hakuna cha mtihani mwema ni matokeo makubwa sasa, siku hizi darasa la saba ‘wanafunzi’ wote wanafaulu.... wa kufeli hamna kitu hata kama ni mwanao kubali tu wala usihangaike naye kuhusu shule.
 
Maombi yenu Wana jf. Binti yangu nae kesho yupo kwenye kundi lawatahiniwa.
IMG-20190903-WA0036.jpeg
 
Back
Top Bottom