Wanafunzi vyuo vikuu wataka mjadala na Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi vyuo vikuu wataka mjadala na Rais Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by BAK, Nov 25, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,550
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Date::11/25/2008
  Wanafunzi vyuo vikuu wataka mjadala na Rais Kikwete
  Na Hussein Kauli na Angela Mwakilasa
  Mwananchi

  MARAIS wa Serikali za wanafunzi wa vyuo vinavyounda Umoja wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini (UVEJUTA), wameomba kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili wamweleze juu ya athari za Sera ya uchangiaji wa elimu ya juu nchini.

  Wanafunzi ho walisema jana jijini Dar es Salaam kwamba wanataka kukutana na Rais Kikwete kwa sababu ndiye anayeweza kuyapatia ufumbuzi matatizo yao.

  Hatua hiyo imechukuliwa na wanafunzi hao mikutano yao na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa. Jumanne Maghembe, kujadili suluhisho la madai yao kutotoa mwelekeo sahihi.

  "Tumefanya majadiliano mengi tu na viongozi wa Serikali, lakini ufumbuzi wa madai yetu haukupatikana. Sasa kwa kuwa tunapenda kutumia nji ya majadiliano tumeona mtu pekee anayeweza kuyapatia ufumbuzi madai yetu ni Rais Jakaya Kikwete," alisema Rais wa DARUSO, Anthony Machibya.

  Hata hivyo baadhi ya viongozi hao, wameipokea kwa mitazamo tofauti kauli ya Rais Kikwete ya kuwataka wanafunzi waliofukuzwa ambao wanakubaliana na sera ya uchangiaji, warejee vyuoni, wakisema kuwa inalenga kuwagawa wanafunzi walio na wasio na uwezo wa kuchangia elimu.

  "Sisi viongozi wa wanafunzi hatuna matatizo na matamko yaliyotolewa viongozi wa serikali, ila matatizo yetu yako kwenye masharti magumu ya kurejea vyuoni ambayo yanaonesha kuwa viongozi wa Serikali hawana lengo la kumaliza migomo ya wanafunzi kutokana na sera mbovu ya uchangiaji," alisema Machibya.

  Naye Rais wa Chuo Kikuu Ardhi, Masawe Anthony alisema hali ya kifedha kwa asilimia kubwa ya wazazi wa wanafunzi mbaya hivyo kuwaambia wachangie Sh400,000 hadi Sh1 milioni kunawafanya wanafunzi wengi washindwe kulipa.

  Naye Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT), Cleophas Mahalangata alisema: "Tumeipokea kauli ya Rais Kikwete kwa masikitiko makubwa kwa sababu, inalenga kuwagawa wanafunzi wenye uwezo na wasio na uwezo na kibaya zaidi inawakandamiza wasio na uwezo".

  Kwa upande wa Rais wa serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Muhimbili, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja huo, Godbless Charles, alisema anashangaa Rais Kikwete kutoa kauli tofauti na aliyoitoa mwaka jana katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kuwa hakuna mwanafunzi atakayeshindwa kusoma kwa kukosa ada.

  Viongozi hao pia wamepinga masharti yaliyotolewa na Wizara ya Elimu ya kuwataka wanafunzi waliofukuzwa vyuoni kujaza fumu za kukubaliana na sera ya uchangiaji kabla hawajareshwa vyuoni, wakisema haina lengo la kumaliza kiini cha matatizo yao.

  Walibainisha kuwa wanafunzi wanaotoka katika familia masikini hawataweza kukidhi vigezo vya sera hiyo na kwamba, wanaweza wakajaza fomu za mikataba hiyo lakini wengi watashindwa kulipa kwa sababu ya kukosa uwezo.

  "Tumesikitishwa na kauli ya Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Gaudensia Kabaka akiwataka wanafunzi wanaotaka kurejea vyuoni kujaza fomu za kukubaliana na sera ya uchangiaji, kwa sababu si rahisi kupata fedha hizo katika kipindikifupi," alisema Gogbless.
   
 2. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kimsingi suala la mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ni tata na sijepesi kama tunavyoliona. Vile vile ni vema kutambua kuwa watanzania wengi hawana uwezo wa kujisomesha kwa level ya university. Awali ilikuwa mkombozi wa mtoto wa mkulima 'rural poor'' ilikuwa nikuhakikisha anafauru vizuri form six na kujihakikishia udhamini wa serikari.

  Kauli ya kisiasa ya kikwete kutaka kupata cheap populality ndio chimbuko la migogoro ya vyuo vikuu bongo sasa. Kwani haikuchambua kwa kina namna suala la mikopo litaendeshwaje au nikwa jinsi gani swala hili litakuwasustainable kwa kuzingatia uchumi wa nchi, scheme management na mahitaji halisi ya wanafunzi Vs wanafunzi waliopo vyuoni.

  Ushauri wangu kwa marais wa Vyuo vikuu. Try to come up with a Strategic Plan that can be translated into an operational plan on how feasible should funding for university student be in terms of loans in a long run. Similarly, propose a short term alternative on what should be done for you to continue with your studies for we all know that JK made a very naive political statement which proved failure the very first year of implementation for I was a student in Tanzania by then.

  Basically I regarded as a silly decision, though it could be made possible but not under abrupt implementation for we had a number of issues to put in place before we implement that.

  So guys all the best lakini have something feasible for him to make decision just at hand. I guess he is also confused and he do not know what to do so help him. If you go there and just say we need money today without giving him how best do you think he can handle that I'm sure guys it wont work. This is some thing very technical that needs brainy people.

  cheers
  +44 7551 479 114
  UK
   
Loading...