Wanafunzi vyuo vikuu waongezeka kwa 200% | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi vyuo vikuu waongezeka kwa 200%

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mwanajamii, Nov 7, 2011.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Idadi ya Wanafunzi katika vyuo vikuu imeongezeka kutoka 45,501 mwaka 2006/2007 hadi 139, 638 mwaka 2010/2011 sawa na ongezeko la asilimia 206 katika kipindi cha miaka mitano.


  TUMEWEZA, TUMETHUBUTU TUNASONGA MBELE.

  Mungu Ibariki Tanzania. Wote wanaobeza maendeleo yaliyofikiwa WASHINDWE NA WA WALEGEE KWA JINA LAKO BWANA.
   
 2. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,819
  Trophy Points: 280
  Tuangalie ubora wa elimu inayotolewa na sio idadi ya wahitimu. Kuna faida gani wa wahitimu kuwa mamilioni lakini kwenye suala job hiring hawa employers hapa nchini wengi wanapenda grads kwa waliosomea nje ya Tanzania sababu wanaelewa mapungufu ya elimu ya vyuo vikuu vyetu?
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ni wangapi kati ya hao wanapata ajira?
  Utasema wajiajiri je mitaji ipo?
   
 4. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  nyie ndo mnaokimbia thread za arusha kwa kuweweseka mnaamua kujibalaguza kwa kutujazia uharo humu, mwaka huu hakuna rangi mtaacha ona lazima mvae bukta jezi
   
 5. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Lakini walimu ni walewale, hawaongezeki na maslahi hayaongezeki!!! mwisho wa siku ni bilabila!!!
   
 6. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hata huko pia kuna mapungufu!!!
   
 7. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Yani wanafunzi wa vyuo vikuu wanapata shida juu ya miundombinu ya vyuo vyao halafu wewe unaleta uzi wa kujipongeza? Wewe ni mtu au jini? Husikii vilio vya vijana wetu kuhusu uhaba wa hostels za chuo unaowalazimu kupanga vyumba vya watu binafsi na kusababisha gharama ya maisha kuwa kubwa?

  Husikii malalamiko ya kujazana kwao katika darasa moja halafu mbaya zaidi vipaza sauti kuwa vibovu na kusababisha wanafunzi kulala mwanzo mpaka mwisho wa kipindi kwa uchovu wa kusikiliza makerere ya muhadhili?

  Husikii wakilalamika juu ya ubabe wa hivyo vizee hapo chuo kuandaa mikakati madhubuti ya kupunguza idadi kubwa ya wanafunzi kwa kuwapa Discontinue? Tena hii ni kawaida sana kwa vyuo vinavyo chukua idadi kubwa ya wanafunzi.

  Usiwe mvivu kufikiria kabla hujatoa uzi angalia unachokiwasilisha kina ukweli kiasi gani kuliko kufikia hitimisho la kujipongeza kwa mambo ya kipuuzi.
   
Loading...