Wanafunzi UDOM warudishwa, udini na siasa vimezingatiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi UDOM warudishwa, udini na siasa vimezingatiwa?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Chief Lugina, Jul 19, 2011.

 1. C

  Chief Lugina JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 290
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Leo limetoka tangazo la kuwataka kurudi chuoni wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) college of Informatics and Vitual Education.
  Chuo hiki kilifungwa tar 28.04.2011 baada ya maandamano ya siku tatu mfululizo wakidai pesa yao ya SPECIAL FACULTY REQUIREMENTS ambazo kimsingi ni haki yao kwa mjibu wa mkataba kati ya mwanafunzi na Bodi ya mikopo. Lakini taarifa zilizopatikana kipindi cha Semina ya wakuu wa mikoa na wilaya kilichofanyika Dodoma walitaka warudi wana-CCM pekee na wana-CHADEMA waachwe, yalisemwa mengi na sasa baada ya miezi miwili wanafunzi wamerudisha na wanafunzi 56 hawajarudishwa. Kuhusu udini mara nyingi chuo hicho kimekuwa kikidaiwa kuwa kina upendeleo wa kidini kwa maana ya waislamu kupewa Priority zaidi wa wakristo, na mara nyingi uongozi wa chuo umekuwa ukikana madai hayo. Please kwa yeyote mwenye taarifa sahihi juu ya watu hao 56 kutorudi chuoni atuambie je ni sababu ya SIASA AU UDINI ndiyo umechukua hatamu!

  waliofukuzwa ni: http://www.udom.ac.tz/DOCUMENTS/TAARIFA%20KWA%20WANAFUNZI%20WOTE%20WA%20SHAHADA%20ZA%20AWALI%20-%20CIVE%20-%2018.7.2011.pdf
  Naomba kuwasilisha!!
   
 2. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Sidhani kama udini umetumika, kweli majina yaliyotangazwa mengi zaidi ya asilimia 90 ni ya wakristo, pia tambua kuwa asilimia zaidi 75 Tz ni wakristo sasa usitegemee kuwa sehemu kama vyuoni kutakuwa na watu wengi wa dini nyingine. Kisiasa naweza kukubali kidogo sababu imekuwa kasumba kwa viongozi wengi wa uma kujifanya wao ni wanamagamba, hiyo ipo hata kwenye vyombo vya dola, kwahiyo kama kulikuwa na kundi la wanafunzi lilionekana kuipinga serikali kwa kitendo chao cha kudhurumu hiyo pesa basi moja kwa moja wao watachukuliwa kuwa ni upinzani hasa CDM.
   
 3. mpiganiahaki

  mpiganiahaki Senior Member

  #3
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Nikiwa kama mmoja wa wanafunzi wa hapo Informatics, katika urudishwaji wa wanafunzi, ni ukweli kabisa udini haujazingatiwa bali kilichozingatiwa moja kwa moja ni itikadi za vyama. Wote walioondolewa ni wale ambao walikuwa viongozi wa chadema katika college. Inashangaza sana kuona Jina la Rais wetu wa Informatics Jafet Yesaya halipo wakati yeye ndiye aliyeweka msimamo kuwa tusiingie darasani! Ila chakushangaza hajawekwa kwenye list ya walio simamiishwa.Bila shaka hii ni kwasababu yeye ni kada wa chama cha mapinduzi(ccm).
   
 4. G

  GHANI JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 685
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hakuna udini Udom,wewe mwenyewe ndio mdini hata thread yako umeiandika kidini,acha kuigawa nchi kiudini st*pid!!!
   
 5. C

  Chief Lugina JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 290
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi siamini katika udini but nilitaka kujua kama huo udini uli-apply kwenye kurudisha watu.Maana sisi tulio mbali tunasikia chuo kina udini but kama hakuna udini God bless them!!!
   
 6. Vanpopeye

  Vanpopeye JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 600
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Udini hakuna kabisa hapo,ukisema udini na waislamu wanapendelewa kama siamini vile,maana hata ukianzia ngazi ya sekondari waislamu hua ni asilimia kumi kushuka chini!yote inayobak ni dini zngne!!!sa 10% ya waislam af ipendelewe hyohyo tena c chuo kizima kinafukuzwa?
   
Loading...