Wanafunzi tukumbushane vilivyotupata kwenye daladala

kitengo mawe ha ha ha hawa jamaa walikuwa mazuzu kuna mmoja aliuliwa kama mwizi kurasini unamkumbuka ?
Makonda tumewachukulia sana hela pale fire ila nilikuwa staff magari mengi mpaka naona noma tabu sikuwahi kupata ila shifti ya jioni tulikuwa tunatembea si unajua migo migo

hahshaa dah kitengo mawe ilikua hatari .. na kutembea mdogo mdogi hadi magomeni namiss sana azaboy
 
Kugombana na makonda ilikuwa ibada kwangu that time nipo Kigurunyembe sec- moro, yani kutoka Mazimbu hadi ufike town center ulikuwa ni mtiti mzito hasa kutokana na kashikashi za makonda,
 
Niliwahi panda dala dala nikijua kabisa nina hela mbovu nilibakia na 150 tu baada ya gari la hostel kuniacha, nikatembea toka loyola hadi Sinza, nikapanda daladala nikiwa na 150 tuuuu.
Gari ikaharibika nikatembea hadi mwenge tokea sinza. Nikapanda gari za Tegeta ili nishukie Afrikana... konda akaniomba nauli nikampa 100 mbovu akaniuliza huna nyingine nikamdanganya kuwa nina 10000 na sh 50 akaniangaliiiiiiia akanitupia ile 100 akachukua 50, najiuliza kama angetaka hiyo 10000 ningemjibu nini wakati nilikuwa sina hela
 
Hahahaha,makonda bana niliwafanya kama babu zangu,kipindi sha naul 50 nilikuwa pale azaboy nilikuwa natoka k/koo to bunju,g/mboto/mwengee bure kabsa nilihakikisha nina mwekundu konda akinidai tu nauli nampa elf 10 anashindwa kunipa chenji ya 9950 basi nilikuwa napanda bure karibu kila siku.

mkuu we mkali duh kumbe mengi sana yamefanyika!! we ukijua hili mwenzio lile
 
Nshatembea ktoka fire mpka ubungo kipindi kile cha kikao cha summit mcty daladala ziligoma....nyingine nilitobolewa mkononi na kibati kwenye daladala za kipanya wakati wa kuminyana kupanda...nilivuja damu balaa...nna visa vingi...kuna siku tulipanda wote siti ya nyuma tukatoa hela ya mwanafunzi...kipindi kile wanafunz wameruhusiwa kukaa kwenye siti...nikiwa la saba nilisukumizwa na konda ubungo nikaanguka nikachubuka mguuni mpka leo kovu....ila salute kwa azania walikua wanatusaidia sana...hata mateja pia niliwazoea mpka juzi mepita kkoo wakanisalimia aisee....
 
mmh! mkuu we noma aisee!!
 
Niliwahi panda dala dala nikijua kabisa nina hela mbovu nilibakia na 150 tu baada ya gari la hostel kuniacha, nikatembea toka loyola hadi Sinza, nikapanda daladala nikiwa na 150 tuuuu.
Gari ikaharibika nikatembea hadi mwenge tokea sinza. Nikapanda gari za Tegeta ili nishukie Afrikana... konda akaniomba nauli nikampa 100 mbovu akaniuliza huna nyingine nikamdanganya kuwa nina 10000 na sh 50 akaniangaliiiiiiia akanitupia ile 100 akachukua 50, najiuliza kama angetaka hiyo 10000 ningemjibu nini wakati nilikuwa sina hela

Teh Teh Teh dah umetisha bandugu! Hapo uso wa mbuzi kama nakuona!!
 
Sie tumesoma enzi za mwalimu, unatembea dk 10 umeshafika shule na ufagio wako.
 
nilisukumwa na konda bus ikitembea nikadondoka chupuchupu nikanyagwe ila kipondo alichopokea kutoka kwa abiria kilimtosha. Ilikuwa kituo cha mabasi Makongo
 
mmh! pole mkuu nakumbuka nikiwa f1 kuna jamaa flani wa Azania alisukumwa na konda akadondoka na akakanyagwa na tahiri akafa maeneo ya yombo dah! alazwe pema!!!
 
dah mbaya sana asee. RIP mwanafunzi.

hawa makondakta ni matatizo
 
Back
Top Bottom