Wanafunzi Nairobi waunda chaja ya simu ya baiskeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi Nairobi waunda chaja ya simu ya baiskeli

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Iga, Jul 24, 2009.

 1. I

  Iga Senior Member

  #1
  Jul 24, 2009
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hullo, Wahandisi wetu Mlimani Chuo Kikuu. Bado migomo inaendelea au kuna utafiti mnaoufanya ? Wenzenu Nairobi wameiadapt dynamo ya baiskeli na wana kusudia kuwafikishia wanavijiji huduma ya kuchaji simu zao kwa kutumia baiskeli hizo hizo zinazotumika kwa usafiri.

  KUBWA zaidi ni kuwa vijana hao wa Nairobi University sasa ni wajasiriamali na wenye kiwanda kidogo cha kutengeneza teknolojia yao hiyo iliyohitaji kutumia fikra na akili kidogo tu. Lakini kwa kuwa nyie hamtazami matatizo yanayowasumbua wazazi wenu bali kulalamika na kuandamana kila siku hamna muda wa kutumia akili zenu kujitajirisha wenyewe. Poleni sana! Na pole kubwa ziaidi kwa Watanzania maana wasomi wa namana hii hawatatupeleka kokote kule. Tutaendelea kuwa masikini hadi Yesu arudi tena!

  Computer Centre shikamooni ? Toka muanzishwe mmeshagundua nini toka aliyoyafanya Kyaruzi ? Au mankwenda kwenda tu kiasi cha kushindwa hata kutoa vyeti vya wanafunzi wanaohitimu kwa wakati ? Kwa njia hiyo kweli mnaweza kugundua kitu?

  Nimechoka na tabia yetu ya kuonesha kwamba ni juu tu mambo hayafanyi kazi kumbe na huku chini ni uozo mtupu. Amkeni Watanzania au mnasumbuliwa na ugonjwa gani usiotibika?

  Uhandisi zaidi ya miaka ishirini mwashindwa kugundua pampu za maji, sindano, pasi, simu rahisi, redio rahisi, umeme wa sola na umeme wa upepo.Mmmmh ama kweli mna vichwa vigumu au rasilmali watu Tanzania ni tasa na gumba hasa!!!!
   
 2. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Elimu ya kusolve na kukariri madesa italetaje wahindisi wagunduzi? They don't think outside the box...they fight to get good GPAs and finish up their courses!!What would come thereafter sio muhimu sana.
  Lakini vijana hawa wakenya wameonyesha kwa vitendo mhandisi anatakiwa afanye nini.Na promo wanayoipata sasa hivi, lazima watatoka tu.
   
 3. C

  Chief JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2009
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,488
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Sioni wivu, laikini that's definitely not a big deal. Kuchukua Dynamo ya baiskel, kuweka rectifier (mimi sio electrical engineer lakini naaminihiyo ndio basic circuit) ndio kitu cha kupiga kelele kwenye radio? Hiyo ni sayansi ya O level and sio ya graduate wa chuo.
   
 4. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2009
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 741
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Nothing special for a gradute.
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kwanza kabisa Iga shukurani kwa kuleta nyeti hii, ingawa umewafanyia overkill vilaza wetu wa Choo Kikuu Manzese.Mimi sishangai sana kwa sababu kuna ma engineer wetu wa bongo wengine wameingia humu na kusema historia si muhimu, sasa watu kama hawa wanaoelea katika cloud ya isolation hata wakiyajua matatizo ya wananchi watayaona yako too basic.Einstein alisema imagination is more important than knowledge, hata kama waliijua hii teknolojia na hawakuifanyia kazi kwa sababu walifikiri iko too basic, Wakenya washawapiga bao kwa sababu wameonyesha imagination zaidi.Hii pia naweza kui attribute to capitalistic thinking, hii incident ina underscore point kwamba wabongo bado hatujaweza kuelewa free market na implications zake, tunataka prestigious academic credentials wakati hatusolve problems.Hata kama hii kitu inatumika lakini haijawa patented hawa wanaweza kuipatent na kuwa rightful owners of the technology.Leibniz na Newton wote waligundua calculus simultaneously, tena kuna accounts nyingi zinasema Leibniz aligundua calculus kabla ya Newton, lakini mpaka leo Newton ndiye anajulikana kama mgunduzi kwa sababu ya publicity.

  Na hao wanaosema hii ni teknolojia ya O level na wala si graduate shame on them, kwa sababu kama ni teknolojia ndogo hivyo walikuwa wanasubiri nini kuifikisha kwa wananchi? The fact that this technology is so basic neither absolve them nor excuse them.Kama wananchi wangeweza kufaidika na teknolojia it does not matter how basic it is.Hii inaonyesha hawa watu hawaelewi maana ya elimu, hususan hii ya kieengineer ni nini, they would rather wrestle with atomic theory ambayo haiko applicable bongo kwa sababu hatuna sehemu ya kuifanyia kazi kuliko kutoa solution ambayo mamilioni ya watu wanaihitaji.Hili swala mimi mwenyewe nimejiuliza, hivi mimi na ma gadget yangu yote haya siku nikiingia nayo bush kubwa huko hamna umeme si yatakuwa useless tu, hawa jamaa wametoa bonge la solution.

  Uzuri wa solution si lazima utokane na complexity, actually the simpler a solution is the more elegant it is bound to be.Natures symmetry, which provides the underlying fabrics for the deeper reasons for the universal laws of physics, is known for its simplicity, not its complexity.

  Kwa hiyo hii dhana mgando ya kwamba solutions ni lazima zitishe na kuwa unapproachable ili ziwe na maana ndiyo maana halisi ya kukosa elimu, typical kwa some graduates wetu wa Choo Kikuu Cha Manzese.
   
  Last edited: Jul 24, 2009
Loading...