Wanafunzi na Mwalimu .

Wanafunzi na Mwalimu .

sir Ganto G

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
573
Reaction score
114
Mwalimu "Watoto wazuri kesho kila mtoto aje na hadithi ya kusimulia,na atawaambia watoto wenziwe kuwa inawafundisha nini"
Siku ya pili, haya tuanze hadithi zetu,haya rose pale,
Rose " siku moja mama alinituma kununua soda nne za wageni,njiani na mimi nikatamani soda,nikakaa chini nikanywa moja,nilivorudi nyumbani wageni kwa bahati mbaya wakawa wameondoka,mama akasema nirudishe soda dukani.
Mwalimu "inatufundisha nini?"
Rose"tusinywe soda za wageni kama hatuna kiu"

John "siku moja nilitumwa dukani kununu maziwa,wakati narudi nikakuta marafiki zangu wanacheza mpira nikaweka maziwa pembeni nikaingia kucheza,baadae rafiki yangu akapiga mpira ukagonga jagi na maziwa yakamwagika".
Mwalimu "inatufundisha nini?"
John "Tusililie maziwa yaliyomwagagika"

Dogo Jose" mi nina hadithi nzurii mtaipenda wenyewe.Kwenye vita ya Uganda Baba angu akawa ndo askari pekee aliyebaki kwenye kikosi chake baada ya wote kuuwawa,alibaki na vitu vitatu,whiski,risasi tatu na singe.
Walitokea askari sita wa adui, baba akachukua whiski akanywa yote,akapiga askari watatu kwa risasi,akamalizia wale watatu kwa kuwachoma kwa singe".
Mwalimu" daah ni hadithi nzuri ilioje lakini inatufundisha nini?"
Dogo Jose" hata siku moja usije mchezea baba angu akiwa amelewa".
 
Back
Top Bottom