Wanafunzi Masasi girls waandamana kupinga uhamisho wa mwalimu wao

Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,146
4,054
Katika hali isiyo ya kawaida, huku taifa likiadhimisha kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa mwl Julius kambarage Nyerere Siku ya tar 14 Oct. Wanafunzi wa shule ya wasichana Masasi waliandamana alfajiri kuelekea ofisi za Mkuu wa wilaya ya Masasi kupinga uhamisho wa mwl wao.

Taarifa nilizozipata kutoka kwa mwl huyo ambaye huwa tunakuwa pamoja mara kadhaa ni kuwa, mkurugenzi wa halmashauri ya mji Masasi aliwaita walimu zaid ya 50 na kufanya nao kikao cha kuwahabarisha kuwa wanatakiwa kuondolewa kwenye shule zao na kupelekwa shule za msingi kwa mkopo.(KUAZIMWA)
Aliendelea kusisitiza kuwa walimu hao hawatapata stahiki zao za uhamisho kwa kile walichokisema kuwa huo sio uhamisho Bali ni kuazimwa.

Yasemekana kikao kilikuwa kirefu kutokana na mvutano wa pande mbili kwa vile walimu hawakukubaliana na suala hilo.
Habari za uhamisho wa mwl huyo ziliwafikia wanafunz wa kidato cha tano na sita ambao hufundishwa na mwl huyo somo la historia.

Wanafunzi waliamua kuandamana kwa kile walichodai kuwa mwl huyo ni mahiri katika somo hilo hivyo hawako tayari kumpoteza kwenda shule za msingi. Vyombo vya usalama na viongoz mbalimbali walijaribu kuwatuliza wanafinzi hao na kufanikiwa kuwanyazisha Mara baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa saa3, huku DAS wa Masas akimwakilisha Mkuu wa wilaya akiwa ndiye kiongoz pekee wayemkubali kumsikiliza.

Taarifa hii ilirushwa pia katika habari ya tarehe 14 Oct Azam two ambapo member mwenzetu wa Jf alionekana akihojiwa na mwandish wa habari John Kasembe kutoka Mtwara. Mwl huyo alidai kuwa uhamisho huo uliojaa uonevu na unyanyasaji ulitumiwa kama fursa pekee kwa wakuu wa shule kuwaondoa walimu ambao walikuwa mstari wa mbele kuhoji mapungufu yao.

Kwa kauli ya mwisho ya DAS (kama nilivyoona kwenye AZAM HABARI) ni kwamba uhamisho wa mwl huyo umetenguliwa na amekiri kuwepo kwa mapungufu kwenye uteuzi wa walimu wanaopelekwa shule za msingi hivyo zoezi litapitiwa upya kuondoa madhaifu hayo.

Hongera mwana jf mwenzetu (ID yake sitoiweka kwa kuwa tukio hilo lilishamtambulisha kwa umma). Haya ni matunda ya jamiiforums ambako ni kisima cha fikra pevu. Hongera kwa kutetewa na umma dhidi ya majungu na uonevu....hayo yote ni matunda ya uwajibikaji uliotukuka.
 
Dahhh...
huyo ticha atakuwa ni mfuasi na mwenye hisia za chama fulani cha upinzani...

maana majukumu makubwa waliopewa hawa wateule, ni kupambana na kila chembe yenye hisia kali za wapinzali
 
Duuh nouma sn yaan mwalim wa sekondari mweny degree na masters primary akafundishe nin? mbona wanataka kutengeneza bom baya kwa watoto wa shule za msingi?
Walim wa shule za msingi walisomea kufundisha watot wa shule ya msingi(saikolijia yalioyosoma ni tofauti na saikolojia ya sekondari)
Solution ni kuajiri walimu wa shule za msingi na sio Kuwahamisha wa sekondari waende msingi, na pia kama kuna ulazima sana wa kutekeleza swala hili basi hao walim wapewe stahiki zao kwani hakuna kuazimwa katika ajira afu unatoka kutoka kituo x kwenda kituo y. huko ni KUHAMA SIO KUAZIMWA
NIULIZE KASWALI KIDOGO WANA JF;
SASA HAWA WALIM MKUU WAO WA IDARA NI ATAKUA NAN? AFSA ELIMU WA SEKONDARI au AFSA ELIMU WA MSINGI?
 
Mkuu hivi masasi Girls si ipo pale karibu ila opposite na gereza la Masasi? Najaribu kuvuta kumbukumbu.. Ni karibu na njiapanda ya nachingwea sijui.
 
Nimeshangaa sana, wapo walimu wengi mtaani na hawana ajira lakini wanawasumbua hao wenye msaada mkubwa A-level.

Kwanini Viongozi wetu wana chuki kiasi hiki!

Nchi ipo mikononi mwa Washamba na Malimbukeni.

Inasikitisha sana!!

lengo lao ni kukomoa sio kuleta maendeleo.
 
Back
Top Bottom