Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,091
- 136,650
Hili jambo la wanafunzi wanaotaka kusoma elimu ya juu kunyimwa mkopo mimi silielewi kabisa.
Mkopo wa pesa ni pesa ambazo mtu anakuazima kwa makubaliano ya kwamba utazirudisha kulingana na masharti mliyoafikiana.
Kwa hiyo, nijuavyo mimi, mkopo hurudishwa.
Sasa tuje kwa hawa wanafunzi wanaonyimwa mkopo.
Sielewi kwa nini wanyimwe ilhali watakuja kuurudisha tena na riba juu yake.
Ningeelewa endapo ingekuwa ni scholarships, grants, n.k., ambazo labda zinalenga katika kuwasaidia wanafunzi wasiojiweza kiuchumi.
Hapo nisingekuwa na tatizo kabisa kwa sababu grants na scholarships ni msaada ambao kwa kawaida huwa hauna matarajio ya kurudishwa, at least siyo kwa njia ya fedha kama ilivyo kwa mkopo.
Sasa hizi habari za watu kunyimwa mikopo kisa sijui wamesoma shule za watu wanaojiweza kiuchumi, haziingii akilini kabisa.
Mtu anayejiweza kiuchumi kwa nini umnyime mkopo? Aliye na uwezo kiuchumi na aliye na uwezo mdogo kiuchumi ni yupi kati yao mwenye mwelekeo mzuri wa kuulipa huo mkopo?
Mikopo ya elimu inapaswa kuwepo kwa yeyote yule atakayetaka madhali katimiza tu sifa zilizo za msingi kabisa: ana sifa ya kusoma chuo, keshadahiliwa na chuo, n.k.
Uwezo wa wazazi au walezi usiwe kigezo cha wanafunzi kupewa au kunyimwa hiyo mikopo.
Uwezo wa wazazi au walezi labda uwe moja ya vigezo kwenye grants na scholarships huko. Mikopo hapana.