Wanafunzi Karne hizi Wanapata Ujasiri wa Kubishana na Walimu wao?

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
kweli zama zimebadilika sana siku hizi unakuta mtoto wa form one anaambiwa shika chini na mwl wake anamjibu anavyotaka mara sishiki mara hoo huniwezi kunichapa wewe,

Kipindi chetu mwl anaweza kukuchapa hata viboko 8 wala usitoe neno lolote tena anaweza kukwambia useme Asante na ukifika nyumbani ni kimya hakuna hata mzazi kujua ila siku hizi hata mwanafunzi awe na kosa akichapwa viboko viwili tuu aisee kijiji kizima kitajua,Tumesoma na wanafunzi wakubwa kama kaka zetu ila walikua wanashika chini na viboko wanakula kwa Sana na bado adhabu nyingine watafanya.

Viboko ni kama Sanaa kazi ya Sanaa ni kuelimisha,Kuburudisha,kufurahisha na Pia kuonya,Kwa maendeleo ya Elimu yetu ni vyema tuwalee watoto wetu vizuri kuanzia nyumbani wakiwa na Nidhamu kuanzia nyumbani hata shuleni watatii walimu wao tuu.

Nidhamu ndo kila kitu.
 
Walimu wenyewe wa sasa mashalo wanaingia adi disko la welcome form one unategemea nn
 
Enzi zenu ndio zipi hizo mkuu..!

Mimi kumbukumbu zangu zinanirejesha nyuma nakumbuka nilipokuwa darasa la kwanza 1998, wanafunzi wa madarasa ya mbele niliowakuta pale shule, walikuwa watu wazima, wababe, wakorofi kiasi kwamba hata walimu wa rika lao walikuwa wanafyata mikia.. na muda mwingine walimu wanoko wanoko walikuwa wanapigwa mno na hao wanafunzi, na mambo yaliendelea hivyo hivyo hadi sekondari hadi vyuoni lakini nyakati zilivyokuwa zinasonga mbele wanafunzi tuliokuwa tunahitimu tukuwa bado na umri mdogo sana kiasi kwamba hata kama tungekosa nidhamu basi tungekuwa waoga tu wa kubishana na amri ya mwalimu..

Sasa sijajua hao wanafunzi wa siku hizi wakoje!
 
Wanavuta bangi sana kama huyu amekuwa teja
7d7a992cae48ded677261dad64c526c3.jpg
 
Mimi Niko shule za vijijini sasa huwa tunawaomba wanafunzi watuletee maji japo galoni moja la Lita tatu ,sasa Leo ilikuwa ni kituko baada ya mwalimu wa zamu kukagua usalama wa maji hayo kwenye magaloni hayo na kubaini panya aliyekufa na kuoza ndani ya galoni la mwanafunzi pia nirejee katika shule hii hakuna bomba la maji wala kisima cha maji hivyo tunafanya kuwaomba,kwaiyo tulivyobaini hilo hatukulifumbia macho tuliwaathibu sana sitegemei kama watarudia tena kwaiyo niseme kwamba wanafunzi wa sasa hawana uoga wala staha mbele za walimu na wazazi kwa ujumla
 
Back
Top Bottom