Wanafunzi chuo kikuu cha Dar, wagoma kusaini fedha ya kujikimu (Boom)

Nimepaona hapo rev square nimeanza kulimiss kunji..anzishen kunji vijana mtaishije kwa hvyo vijipesa vya karanga?afu kumbuken hapo udsm ndo mnategemewa na vyuo vingne,kwa hyo piganieni haki yenu vijana ila in peacefully way..msimdhuru au kumtukana mtu.
 
Ukimpa mtu elimu atajitambua na kutambua dhuluma zinazofanywa na Ccm. Sasa serikali imeamua kunyima watu elimu kwa kuweka vikwazo vingi ili hiendelee kutawala miaka na miaka. Mmejiuliza ni kwanini mikoa masikini ndio Ccm wanapata kura nyingi kuliko mikoa iliyoendelea? Ni kwasababu hawana elimu wa uelewa wowote.
DARUSO piganeni mhakikishe wadogo zetu wanasoma kama walivyosoma hao wagawa mikopo.
Kwani ccm huwa wanapata kura au wanaiba? (Kwa mujibu wa upinzani)
 
kama wanasiasa wameshindwa kupaza sauti vijana wameamua kumnyoosha mkuu wa kaya kwa kumgomea vijisenti vyake.
UDSM ni chuo kikuu chenye hadhi nchini ni haki yenu kulifanya hili kwa maslahi ya walio vichochoroni.Asante UDSM,Magufuli amekalia kuti kavu,UDSM umesema hakuna mbabe tunagomaga tu.
 
Kimenuka na bado ss tuko kwenye maandaliz
Mpaka magu aelewe tu.
Huu sio ukuta bal ni operation mikopo
 
YUKO KWAAJIRI YA MASKINI NA ALICHAGULIWA NA MASKINI NA ATAWATUMIKIA DAIMA. Asante Raisi mtukufu.
 
KUBETI KUNALIPA SOMETIMES

Kama serikali jana ingempa PSG,ARSENAL,BARCELONA,ATLENTICO,MADRID NA BAYERN MUNICH halafu waweke Bilion 6 kwenye mkeka hakika leo wanafunzi wa elimu ya juu wangepata mikopo tena ya 100%

NB:haya ni mawazo wangu najua serikali inasema haina hela.
..Tatizo ni Hapa unapodhani serikali Haina Hela
 
Maoni Yangu Ya Wazi

Ndugu Watanzania, binafsi katika mambo ya msingi ambayo ningependa kuona nchi ikiyapa kipaumbele ni Elimu. Mimi ni mwanafunzi bado na mnufahaika wa Bodi ya Mikopo. Lakini katika hili sidhani kuna haja ya kuikubalia Serikali.

Mh. John Pombe Magufuli, Rais wetu katika kampeni zako uliahidi sana kulifanyia hili kazi. Uliahidi kuongeza na kufanya maboresho katika sekta hii ya Elimu na ukazungumzia suala la Mikopo ya juu. Tena na kupumbuka pale Jangwani nilisimama juani ukatamka ukiwa mbele ya Mh. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa unashangaa kwanin mtu anayekopa anacheleweshewa kupewa mkopo wake? Najaribu kuyakumbuka mengi ila nikiyaandika nitafanya waraka huu kuwa mrefu, ila ndugu Mh. Kikwete Rais mstaafu alitabasmau kama kawaida yake. Hapo ndio nawaza kumbe kuna uwezekana nchi yetu ni masikini sana sana na sana, kwamba Mh. Kikwete alitabasamu na moyoni labda alisema, "Muda wote utafika Ndugu yangu Pombe John"

Serikali ya awamu ya nne, licha na kasoro zake zote ilizokuwa nazo na kukusanya kiwango cha 700bn kwa mwezi, watanzania tulikuwa na haueni sana ya Madawa, Pesa za Kujikimu, Mishahara (*hata kama ilikuwa ikisuasua). Ni serikali hiyo ya awamu ya nne ya Mh. Kikwete ambayo iliongeza kima kutoka 7,500/=Tshs mpaka 8,500/=Tshs. Ni serikali hiyo hiyo ambayo ilidahili hadi wenye Division III na IV za mwanzo kusoma Shahada.

Sasa Mh. John Pombe Magufuli, Rais wetu sisi bado tuna imani na wewe baba lakini kwenye hili tuoneane huruma. Hatupendi tukukose lakini hapa tuwe wa kweli kama wewe unavyosema kuwa ni mkweli. Mh. Magufuli hivi karibuni TRA walisema kuwa kwa sasa mapato yaani makusanyo ni 1.2 Trilioni, karibu asilimia 70% zaidi ya ile ya serikali ya awamu ya Nne. Hivi hayo makusanyo yanaenda wapi? Sawa umenunua Ndege, sawa umesahihi ujenzi wa reli ya kisasa hivi karibuni na umetenge 1 Trilioni kuanza huo mradi. Hayo mambo na kusifia, lakini kwenye hili la fedha za kujikimu hapana!!!

Nakuomba Mh. Rais wetu hebu kaa na washauri wako, na mawaziri wako mpitie upya hili jambo. Naomba msitumie nguvu kutukandamiza. Naamini watu na watanzania bado wana Imani na Serikali yako. Mh. Rais Elimu ni jambo la muhimu sana na wote tunatamani sana kupata elimu bora.

Kwa shingo upande niliunga mkono na kupongeza ile jitihada ya kubana ufaulu na kuwafanya wenye Division I na II kusoma shahada, huku Division III za mwanzo zikiruhusiwa kwa baadhi ya kozi. Lakini hili la kupunguza fedha ya kujikimu jamani tusidanganyane.

Na pia watanzania wenzangu kuna wakati ufuasi wa siasa tuuweke kando. Elimu ni suala lenye maslahi ya taifa. Naamini hao wataalamu tunaozalisha watafanya kazi na kuwahudumia watanzania wote. Hivi karibuni kuhusu sakata la Dawa, hata Mh. Rais alisema kuwa kama dawa zikikosekana hata mfuasi wa Chadema akienda hospitali atakosa tu, akiwa na maana hayo ni mambo yanayoiitawala jamii nzima bila tofauti yoyote.

Tusiitumie siasa kutugawa, kwani mimi nikimaliza nikawa Daktari nitahudumu kwa kuwagawa?

Mnaposema kuwa pesa tunapewa nyingi ndio maana tunanunua simu, laptops, TV nk! Ndio tunanunua lakini je hivyo sio vitu vya msingi kwa Kijana wa Karne hii kuwa navyo. No offence, hata ndugu zetu Bodaboda na wasukuma mikokoteni wanazo simu nzuri na TV majumbani/maghettoni kwao. Je mimi mwanafunzi wa chuo kikuu sipaswi kununua hivyo vitu? Leo hii ni nani asiyejua mchango wa teknolojia ya mawasiliano kwenye Uchumi, nk

Pesa hii 8,500/Tshs ambayo tunaililia mnadhani inatosha?

Pesa hii inapunguzwa na huku ikiwa haitoshi. Chukua mfano wanafunzi tunaosoma vyuo vya binafsi ambazo ada zetu kwa sisi tunaosoma udaktari ni mara 2/3 au hata 4 ya ile inayotozwa kwenye vyuo vya Serikali. Bado hatuna malazi kama wenzetu wa serikali wengi tunapanga vyumba vya kuishi maana vyuo vingi havina maradhi na tunatoa takribani 70,000 mpaka 100,000 kwa mwezi. Bado kuna mahitaji ya kula, maji, umeme nk

Nifupishe maana nina mengi ya kuandika na sipendi kuwachosha.

Nawaunga mkono Ndugu zetu wa UDSM waliotangulia kunauwezekano nasisi vyuo vingine tukawafuata. Cha msingi tutume wawakilishi kwanza,naamini kuwa hii serikali ni sikivu watasikia kilio hiki. Ndugu zetu TAHILISO tunaomba sana mtupiganie.

Mwisho
Rutasingwa AV
Alhamisi
Oktoba 20, 2016.
 
Anzisha thread yako..........
 
selikali hii inazngua sana lakini mheshimiwa Magufuli kumbuka ahadi zako pale Jangwani wakati ukifungua kampeni zako mwaka 2015
uliahidi mkopo kwa kila mwanafunzi wa Elimu ya juu sas a cjui ndo nin unafanya au ndo uahapata basi kila mtu atajua mwenyewe
 
sio msaada huo mkuu hizo hela LAZMA KURUDISHA ukishaajiriwa

Ukishaajiriwa na nani? Ajira ziko wapi mwenzangu
 
Mwanapropaganda na Freyzem Hivi nani unadhani analipwa ili awe mjinga? Nyie kila kitu huwa mnapinga, yaani hata vile vinavyoonekana. Mfano Mh Mbowe juzi kafurumushwa jengoni mkaanza kumtetea. Unajua unanikumbusha kuna jamaa alikuw ahapa kazini yaani yeye alikuwa kila siku kumtukana Dkt Magufuli, kuitukana serikali kila kukicha na mpaka mi nikawa najiuliza hivi huyu ana akili kweli? Yaani yeye kila kitu alikuwa ni kupinga kama mlivyo ninyi kwenye mitandao, ila kilichotokea yeye anakijua. Kumbe jamaa alikuwa na vyeti fake. Baada ya uhakiki wa pili kutaka kuja aliandika barua ya masaa 24 kuacha kazi, mpaka sasa yupo kitaa anapiga miayo tu. Na ndicho ninachojifunza kwenu ninyi, kuwa wengi mliishi kwa kudhulumu haki za watu wengine na huu ndiyo mwisho wenu wezi nyie. Kuhusu mikopo hili ni suala linalojulikana halihitaji jiniasi, kila mtu anaelewa umuhimu wa elimu na kila kijana anahitaji elimu ya chuo kikuu.
Yaaani wewe haujaongea kitu yaani ni siasa tupu za chama fulani so hebu comment mambo yanayohusu elimu hasa hili la mikopo, hivyo hayo mambo ya akina mbowe hatuyahitaji hapa.
 
Back
Top Bottom