Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,610
Arusha.
Wanafunzi wawili wakazi wa Olkeryan jijini Arusha wamefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye shimo lililokuwa likitumika kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya mchepuko inayotoka Ngaramtoni kuelekea Moshono.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo leo Jumatano Aprili 11, 2018 amewataja wanafunzi hao kuwa ni Hadija Hans aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Olkeryan na Christina Kivuyo mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya Msingi Mt Meru.
Mkumbo amesema Hadija alikuwa akipita karibu na shimo hilo hilo jana saa 11;30 jioni na kutumbukia na kwamba Kivuyo alipokwenda kwa nia ya kumsaidia naye alitumbukia katika shimo hilo na wote kufariki dunia.
Amesema baada ya tukio hilo wafanyakazi wanaojenga barabara hiyo kwa kushirikiana na wananchi na polisi walienda eneo la tukio na kukuta miili ya wanafunzi hao, ambayo waliipeleka Hospitali ya Mt Meru.
mwananchi