Wanafunzi 400 wajisaidia porini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi 400 wajisaidia porini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NguchiroTheElde, Jan 17, 2011.

  1. N

    NguchiroTheElde Member

    #1
    Jan 17, 2011
    Joined: Jun 13, 2010
    Messages: 22
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Wanafunzi 400 wajisaidia porini


    na Ambrose Wantaigwa, Tarime

    Tanzania Daima, 17 January 2011, pg 6.
    [​IMG]
    SHULE ya msingi Nyairoma iliyoko katika kata ya Sirari wilayani Tarime yenye wanafunzi zaidi ya 400 inakabiliwa na upungufu wa vyoo na kusababisha wanafunzi kujisaidia porini.
    Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki shuleni hapo, mwenyekiti wa kijiji cha Sirari, Nyangoko Paulo, alisema atalazimika kuitisha kikao cha dharura cha serikali ya kijiji, ili kuwanusuru watoto hao kukumbwa na magonjwa ya mlipuko.
    “Wanafunzi wanalazimika kujisaidia vichakani ama katika vyoo vya shule jirani ya Sirari mita chache kutoka shuleni hapo hali inayowaweka katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu,” alisema.
    Alisema uamuzi wa kuitisha kikao cha dharura cha serikali ya kijiji umechukuliwa baada ya kamati ya shule hiyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo kutokana na ufinyu wa bajeti. Mmoja wa wazazi, Marwa Masese alitishia kuhamisha watoto wake wawili ikiwa shule hiyo haitachukua hatua za haraka kukabiliana na mazingira mabaya ya kiafya yaliyoko shuleni hapo ikiwa pamoja na kuchimbwa vyoo.
     
Loading...