Wanachuo wataka sifa ya anayegombea ubunge iwe angalau degree moja

Wanachuo wataka sifa ya anayegombea ubunge iwe angalau degree moja

Elias Msuya

Senior Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
173
Reaction score
671

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu Mkoa wa Dar es salaam, wamependekeza sifa ya mtu kugombea ubunge iwe pamoja na elimu ya shahada ya kwanza, tofauti na sasa ambapo sharti la elimu ni kujua kusoma na kuandika.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi hao jana Juni 22 jijini Dar es Salaam, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Angasi Robert Okechi, amesema baadhi ya wabunge wameonyesha udhaifu mkubwa katika kutekeleza majukumu yao kutokana na elimu duni waliyo nayo.

Angasi amekosoa tabia ya kuchagua wabunge kwa misingi ya umaarufu au uwezo wa kifedha bila kuzingatia elimu na uelewa wa masuala ya kisheria na kiuchumi.
“Haiwezekani mtu mwenye elimu ya darasa la saba, kwa sababu tu anajua kusoma na kuandika, anazo fedha na anajua kuzungumza vizuri, apewe jukumu la kutunga sheria za kuongoza taifa. Bunge ni chombo nyeti kinachopaswa kuwa na watu makini,” amesisitiza.Angasi amehimiza Watanzania kuwaamini vijana waliobobea kutoka vyuo vikuu na vyuo vya kati, kwa kuwa wanaweza kuibua mipango madhubuti ya kulisaidia taifa kwa nguvu na maarifa yao.

Amesema tofauti na matarajio ya wananchi kwa wabunge hao kuwatetea, wengi wao huingia bungeni kwa lengo la kupanga mbinu za kisiasa zitakazowarejesha madarakani ifikapo mwaka , badala ya kujadili masuala ya msingi ya maendeleo.“Mbunge anatakiwa aingie bungeni kuwasemea wananchi wake kwa maslahi mapana ya nchi. Lazima awe na uwezo wa kuandaa mpango mkakati na kuupeleka bungeni ili utungwe sheria zenye manufaa kwa wananchi,” amesema.
 
Watatekwa kisa wamepinga jambo, ila wangesifia wangepewa posho
 
SAwa, ngoja tuone.

Hii nayo ni moja ya reforms?
Hivi Benson Kigaila ana elimu kiasi gani ?
 
Back
Top Bottom