Wanachuo MUHAS wanazimiwa AC na WiFi Ila wakiwemo wasudan zinawashwa

Smkwawa

JF-Expert Member
Feb 18, 2014
651
964
Hii kali sana kweli ngozi nyeusi ni nyeusi tu..

Rafiki yangu aliepo MUHAS, katika story za hapa na pale akawa ananielezea kuwa licha ya JOTO la Dar hili lote madarasa wanayotumia kusomea na yenye WiFi huwa yanawashwa AC tu ikiwa hawa wanafunzi wageni wa SUDAN wakiwa wanafundishwa .. (ikumbukwe madarasa/lecture rooms wanashare wote).. wakitoka tu ama vipindi vyao vikiisha walinzi wanakuja kuzima AC ..zinazimwa ukijaribu kuuliza unaambiwa nyie sio watu maalum tumepewa maelezo AC ni kwa ajili ya wanafunzi wa Sudan..

Ikumbukwe wanafunzi hawa wa Sudan wapo MUHAS kusoma sababu ya hali ya kiusalama nchi kwao kuwa sio nzuri wamekuja huku ili kuendeleza masomo yao ambayo walikuwa wanasoma..

Namnukuu.
.
"Kama sisi watu weusi tunafanyiana hivi, kuna haja gani ya hawa waSUDAN wawepo? Bora wasiwepo ili tuendelee kupambana na joto" sisi ngozi nyeusi tuna shida gani hasa tukiona ngozi nyeupe? Upo radhi umkandamize mwenzako kisa sio mweupe?
"
Mwisho wa kunukuu..

Waungwana hii ni sawa?..
 
Labda wanalipa zaidi kufidia gharama za AC. All in all AC inapaswa kua hitaji la lazima kwa joto la huo mji wa daslam
Joto la sudan na la DSM halipishani Sana ingawa la sudan Ni kiboko nahisi 50° kwa 33° kwa dsm

Pia huwenda hao wamesha zoea kusoma na ac na kule ac ni sswa na Bei bure Hadi nyumb za makuti wanaweka ili mradi tu uwe na umeme

Hv by the way Prof janabi hayumo huku kujibu tuhuma hzi
 
Kuwashwa kwenye special occasion Mfano watu wamelipia Kwa ajili ya kutumia hayo madarasa Kwa semina zinawashwa.Hayo madarasa Sio tu Kwa ajili ya wanavyuo pekee
Special occasion Ni muda wa wanafunzi wa Sudan wakiwa wanasoma tu, wakiingia wanafunzi wa MUHAS wanazimiwa..? Mbona wakati hawajafika waSUDAN AC Zilikuwa zinatumika.. muda wote. Kwani waSUDAN wamebadili nini?

Msiwafanyie vijana hivyo hata wao wanalipa ADA .. Joto la DAR hili lote bado unawafanyia watoto hivyo wewe ungekubali? Ufanyiwe hivyo ilihali AC ziliwekwa sababu ya matumizi hayo.
 
Wasudani ni VIP nyie hata ada hamlipi mpaka mletewe JKT ndo mnalipa kutokea mifukoni kwenu, wengi wenu mkopo wa serikali.Ingekuwa maamuzi yangu hata shoti mpigwe, madaktari mna roho mbaya sana linapokuja suala la rushwa Hanna utu hata kidogo.Kwani mlikotoka kwenu kule Maganzo kuna AC?
 
Back
Top Bottom