Wanachotambia Chenge na Ngeleja hiki hapa

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,143
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaongozwa,pamoja na sheria nyingine za nchi, na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni Kanuni za Kudumu za Bunge ndizo zinazotumika mara kwa mara Bengeni kuongoza mijadala na kufikia maazimio/maamuzi. Kanuni za Bunge ndizo hasa huelekeza uchaguzi wa Spika,Naibu Spika na Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge za kisekta na zisizo za kisekta.

Wenyeviti wa Kamati za Bajeti (Andrew Chenge) na Katiba, Sheria na Utawala (William Ngeleja) wamehusishwa na Escrow. Wametakiwa na maazimio ya Bunge kuwajibishwa/kuwajibika. Katika kuwajibshwa/kuwajibika kuna mvutano kwelikweli. Yaani,nani hasa anaweza kuwawajibisha Wenyeviti hawa wa Kamati za Bunge? Rais Kikwete amejitoa na kujiweka mbali sambamba na Spika Anne Makinda.

Nimelazimika kuzipitia Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la 2007) kuona wa kuwawajibisha akina Chenge. Nikajielekeza katika Kanuni ya 113 inayozungumzia Muundo wa Kamati za Kudumu za Bunge. Kanuni husika yenye fasili za 1 hadi 11 inazungumzia kuteuliwa kwa wajumbe wa kamati;mipaka ya kuteuliwa;mteuzi wa wajumbe wa Kamati (ambaye ni Spika-fasili ya 5);kipindi cha kuhudumu ujumbe wa kamati pamoja na uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati.

Wenyeviti na Makamu wao wa Kamati wanachaguliwa na wajumbe wa Kamati husika. Hii ni kwa mujibu wa fasili ya 10 ya Kanuni hiyo ya 113. Kimsingi,Kanuni zipo kimya kuhusu kuondolewa/kuwajibishwa kwa Wenyeviti au Makamu Wenyeviti. Kuodolewa/kuwajibishwa hakuzungumziwi popote katika Kanuni za Bunge.Hata Kanuni ya 114 yenye fasili za 1 hadi 19 inayoratibu utaratibu na mwenendo wa Kamati za Bunge haitoi nafasi kwa wajumbe wa Kamati kuweka mezani hoja binafsi kikaoni kuhusu kumuondoa au kumuwajibisha Mwenyekiti.

Ndiyo kusema, tambo na kutowajibika kwa Chenge na Ngeleja ni kutokana na mapungufu ya kikanuni. Labda waombwe kiungwana kutii maazimio ya Bunge juu yao kama Spika Makinda alivyotoa rai jana.
 
Wenyeviti wa Kamati za Bajeti (Andrew Chenge) na Nishati na Madini (William Ngeleja) wamehusishwa na Escrow. Wametakiwa na maazimio ya Bunge kuwajibishwa/kuwajibika. Katika kuwajibshwa/kuwajibika kuna mvutano kwelikweli. Yaani,nani hasa anaweza kuwawajibisha Wenyeviti hawa wa Kamati za Bunge? Rais Kikwete amejitoa na kujiweka mbali sambamba na Spika Anne Makinda.

Nimelazimika kuzipitia Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la 2007) kuona wa kuwawajibisha akina Chenge. Nikajielekeza katika Kanuni ya 113 inayozungumzia Muundo wa Kamati za Kudumu za Bunge. Kanuni husika yenye fasili za 1 hadi 11 inazungumzia kuteuliwa kwa wajumbe wa kamati;mipaka ya kuteuliwa;mteuzi wa wajumbe wa Kamati (ambaye ni Spika-fasili ya 5);kipindi cha kuhudumu ujumbe wa kamati pamoja na uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati.

Wenyeviti na Makamu wao wa Kamati wanachaguliwa na wajumbe wa Kamati husika. Hii ni kwa mujibu wa fasili ya 10 ya Kanuni hiyo ya 113. Kimsingi,Kanuni zipo kimya kuhusu kuondolewa/kuwajibishwa kwa Wenyeviti au Makamu Wenyeviti. Kuodolewa/kuwajibishwa hakuzungumziwi popote katika Kanuni za Bunge.Hata Kanuni ya 114 yenye fasili za 1 hadi 19 inayoratibu utaratibu na mwenendo wa Kamati za Bunge haitoi nafasi kwa wajumbe wa Kamati kuweka mezani hoja binafsi kikaoni kuhusu kumuondoa au kumuwajibisha Mwenyekiti.

Ndiyo kusema, tambo na kutowajibika kwa Chenge na Ngeleja ni kutokana na mapungufu ya kikanuni. Labda waombwe kiungwana kutii maazimio ya Bunge juu yao kama Spika Makinda alivyotoa rai jana.

Inamaana wakati maazimio ya kuwawajibisha yanapitishwa hawakujua kua haiwezekani kuwawajibisha bila ya wao kuridhia? Halafu wanaibuka vilaza wanatuambiwa kua hii ndio taasisi iliyobaki ikiwa safi wakati tunaona mawaziri wakichafuka wanaachia uwaziri wanendelea kua wabunge(pamoja na uchafu wao).
 
Kwahiyo unataka kusema nini.

Wamekubaliana ku-take advantage ya upungufu ulioko katika kanuni na kukataa kujiuzulu huku wakijua wanatuhumiwa kwa ufisadi wa kupokea fedha za escrow ambazo ni za umma
 
Nikipata ubunge nitajitahidi kupitia bifungu na kanuni hizi
 
Makinda angeweza kuwa-swap kwa kuwapeleka kamati nyingine ambapo wasingeweza kwenda na vyeo vyao.

Pamoja na mabadiliko ya wajumbe wa kamati kwa kila mwaka sidhani kama wenyeviti na makam wake hubadilishwa kamati.Nadhani hubakia kamati ileile mpaka mwisho wa bunge otherwise itokee vingine kama kuvunjwa kwa kamati kama ilivyokuwa kwa Zitto enzi za POAC.
Makinda ktk hilj anatuchezea akili tu na bosi wake Tezidume. Kama kuna ugumu kuwawajibisha kwa nini asivunje kamati kama nilivyosema awali kwa Zitto ili vyeo vyao vife na uchavuzi mwingine wa nafasi zao ukafanyika!?. Labda niulize,kwa POAC aliwezaje!?.Hebu Zitto njoo utufafanulie hapa.
Halafu wanaJF kaa mnakumbuka vyema Chenge hakuchaguliwa huo uenyekiti na wajumbe bali ni Makinda mwenyewe ndio alimteua.Suala hili watu walilalamikia sana ikiwemo wabunge wenyewe lakini huyu mama alifunika kombe na mwanaharamu Chenge akapita,sasa iweje leo ashindwe kumtoa!?

Hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu inahusika hapa ili Tezidume na huyu Bibi Kiroboto waone haja ya kuwawajibisha hawa watu kwa namna wawezavyo.
 
Last edited by a moderator:
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaongozwa,pamoja na sheria nyingine za nchi, na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni Kanuni za Kudumu za Bunge ndizo zinazotumika mara kwa mara Bengeni kuongoza mijadala na kufikia maazimio/maamuzi. Kanuni za Bunge ndizo hasa huelekeza uchaguzi wa Spika,Naibu Spika na Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge za kisekta na zisizo za kisekta.

Wenyeviti wa Kamati za Bajeti (Andrew Chenge) na Katiba, Sheria na Utawala (William Ngeleja) wamehusishwa na Escrow. Wametakiwa na maazimio ya Bunge kuwajibishwa/kuwajibika. Katika kuwajibshwa/kuwajibika kuna mvutano kwelikweli. Yaani,nani hasa anaweza kuwawajibisha Wenyeviti hawa wa Kamati za Bunge? Rais Kikwete amejitoa na kujiweka mbali sambamba na Spika Anne Makinda.

Nimelazimika kuzipitia Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la 2007) kuona wa kuwawajibisha akina Chenge. Nikajielekeza katika Kanuni ya 113 inayozungumzia Muundo wa Kamati za Kudumu za Bunge. Kanuni husika yenye fasili za 1 hadi 11 inazungumzia kuteuliwa kwa wajumbe wa kamati;mipaka ya kuteuliwa;mteuzi wa wajumbe wa Kamati (ambaye ni Spika-fasili ya 5);kipindi cha kuhudumu ujumbe wa kamati pamoja na uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati.

Wenyeviti na Makamu wao wa Kamati wanachaguliwa na wajumbe wa Kamati husika. Hii ni kwa mujibu wa fasili ya 10 ya Kanuni hiyo ya 113. Kimsingi,Kanuni zipo kimya kuhusu kuondolewa/kuwajibishwa kwa Wenyeviti au Makamu Wenyeviti. Kuodolewa/kuwajibishwa hakuzungumziwi popote katika Kanuni za Bunge.Hata Kanuni ya 114 yenye fasili za 1 hadi 19 inayoratibu utaratibu na mwenendo wa Kamati za Bunge haitoi nafasi kwa wajumbe wa Kamati kuweka mezani hoja binafsi kikaoni kuhusu kumuondoa au kumuwajibisha Mwenyekiti.

Ndiyo kusema, tambo na kutowajibika kwa Chenge na Ngeleja ni kutokana na mapungufu ya kikanuni. Labda waombwe kiungwana kutii maazimio ya Bunge juu yao kama Spika Makinda alivyotoa rai jana.

Dawa ha mijitu kama hii mijizi inayochezea udhaifu wa maamuzi ya Bunge vs kanuni, dawa yao ni ngumi na kuwazoa mzobe-mzobe kama Mh. Lema et al wanavyokusudia kukamilisha kwa Mwizi mwingine wa Escrow Profesa juha - Muhongo! Hakuna kuchezea haki na nguvu ya umma hata kama kanuni ni mbovu [ambazo akina Chenge hao hao ndio walioshiriki kuzituna], inabidi kutumia nguvu kuwang'oa na kwa hilo Spika asifungue midomo maana alishasema hana la kuwafanyia wenyeviti ha wezi! Ni kwa Tz tu wanawalea hawa na kusubiria mwizi atumia busara zake au uungwana wake mwenyewe kujiwajibisha...ni ndoto za nchana...! mwenye haki kufanya ubia na mwizi ni dhambi ya asili...
 
Three MPs resign over escrow billions bounty
Dar es Salaam. Three parliamentary committee chairpersons have resigned over the Sh306 billion Tegeta escrow account scandal. Those who handed in their letters to the Office of the Speaker are Bariadi West MP Andrew Chenge, Sengerema MP William Ngeleja and Lupa MP Victor Mwambalaswa.
Mr Chenge and Mr Ngeleja-both from CCM-chaired Parliament's Budget Committee and Legal Affairs and Governance Committee respectively and Mr Mwambalaswa chaired the Energy and Minerals Committee. The trio received about Sh1.7 billion in total, out of which Mr Chenge alone got a whopping Sh1.6 billion from Mr James Rugemalira, who was a shareholder in Independent Power Tanzania Limited (IPTL).
 
Kila kitu hakiwezi kuandikiwa kanuni au sheria!
Tunachohitaji zaidi kuliko sheria na kanuni ni VIONGOZI BORA!
Hata kama tutatunga sheria na kanuni nzuri zinazotuongoza hadi namna ya kulala usiku na kuamka asubuhi, bila ya kuwa na viongozi wenye akili nzuri, wanaochukia uovu, yote tutakayofanya yatakuwa bure!
Tatizo hapa ni uongozi wa Bunge (Spika)
 
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaongozwa,pamoja na sheria nyingine za nchi, na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni Kanuni za Kudumu za Bunge ndizo zinazotumika mara kwa mara Bengeni kuongoza mijadala na kufikia maazimio/maamuzi. Kanuni za Bunge ndizo hasa huelekeza uchaguzi wa Spika,Naibu Spika na Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge za kisekta na zisizo za kisekta.

Wenyeviti wa Kamati za Bajeti (Andrew Chenge) na Katiba, Sheria na Utawala (William Ngeleja) wamehusishwa na Escrow. Wametakiwa na maazimio ya Bunge kuwajibishwa/kuwajibika. Katika kuwajibshwa/kuwajibika kuna mvutano kwelikweli. Yaani,nani hasa anaweza kuwawajibisha Wenyeviti hawa wa Kamati za Bunge? Rais Kikwete amejitoa na kujiweka mbali sambamba na Spika Anne Makinda.

Nimelazimika kuzipitia Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la 2007) kuona wa kuwawajibisha akina Chenge. Nikajielekeza katika Kanuni ya 113 inayozungumzia Muundo wa Kamati za Kudumu za Bunge. Kanuni husika yenye fasili za 1 hadi 11 inazungumzia kuteuliwa kwa wajumbe wa kamati;mipaka ya kuteuliwa;mteuzi wa wajumbe wa Kamati (ambaye ni Spika-fasili ya 5);kipindi cha kuhudumu ujumbe wa kamati pamoja na uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati.

Wenyeviti na Makamu wao wa Kamati wanachaguliwa na wajumbe wa Kamati husika. Hii ni kwa mujibu wa fasili ya 10 ya Kanuni hiyo ya 113. Kimsingi,Kanuni zipo kimya kuhusu kuondolewa/kuwajibishwa kwa Wenyeviti au Makamu Wenyeviti. Kuodolewa/kuwajibishwa hakuzungumziwi popote katika Kanuni za Bunge.Hata Kanuni ya 114 yenye fasili za 1 hadi 19 inayoratibu utaratibu na mwenendo wa Kamati za Bunge haitoi nafasi kwa wajumbe wa Kamati kuweka mezani hoja binafsi kikaoni kuhusu kumuondoa au kumuwajibisha Mwenyekiti.

Ndiyo kusema, tambo na kutowajibika kwa Chenge na Ngeleja ni kutokana na mapungufu ya kikanuni. Labda waombwe kiungwana kutii maazimio ya Bunge juu yao kama Spika Makinda alivyotoa rai jana.

Wakae tu maana hata pangelikuwa kuna kanuni inayo wawajibisha, hakuna anayeweza kuusimamia na kufanya Hivyo katika utawala huu.

Muda waja si punde, wananchi tuta waajibisha vema October 2015, pasipo kurudia makosa.
 
Back
Top Bottom