Wanachokulaga wanajeshi vitani (kama biskuti), ni nini?

Mkuu na vipi kuhusu kua unashiba muda mrefu ni kweli??

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivyo vyakula ulivyovieleza wewe na uzito uliovipa ni 'over expectation' mkuu.

Vyakula hivyo si vyakula vya kula kama ration mkaishana, ni kama vituliza njaa tu, wakati mlo kamili upo.

Hutolewa mbadala kwa kazi za dharura zinazotegemewa kuchukua muda mrefu kumalizika katika utekelezaji wake, kabla askari husika hajarejea kambini na kupata chakula cha moto.

Vyakula hivyo hutolewa kwenye mafunzo, doria za upelelezi na doria za mapigano.

Wakiisha kurejea ama kukwama walipoenda huandaliwa vyakula vya moto kama kawaida na kupelekewa.

Vyakula hivyo ni simple sana; biskuti ngumu, maharage ya kopo yaliyokolezwa mchuzi wa nyanya na sukari ama maharage ya kopo yaliyoungwa vitunguu, chumvi na mafuta, pia na nyama za makopo (beef)na maji ya kunywa.
Ni vituliza njaa tu, hauwezi kusema eti kuna chakula cha kutumia mtu ukapata shibe ya kudumu hapo! Hakuna kitu kama hicho.

Hivyo ndivyo vya msingi, ijapo vipo vingi lakini kwa mtindo wa dry ration kutokana na tamaduni husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za usiku wakuu
Nimekua nikiona kwenye filamu mbalimbali na makala za wanajeshi hasa vitani huwa wanakula vitu flani vipo kama biskuti flani hivi,kwa imani yangu nahisi huwa wanashiba sana na kuna jamaa aliwahi nambia eti wanaweza shiba hata siku mbili,nikamuelewa kwasababu siamini kama wajeda watakua wanakula vitu kujiburudisha.Swali langu je vitu vile ni nini? Na je vinapatikana mtaani??nahitaji nivipate ili hali inapoyumba mfukoni napiga vile burudaani pasi ndefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unavihitaji ili kupunguza gharama? Pasi ndefuuu unajua bei yake ukilinganisha na ugali mchuzi? Au unapenda ubunifu mkuu.

Km ubunifu piga loico mchuzi mix

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni aina mikate isiyotiwa chachu
 
Hicho wanacholishwa hakina aina fulani ya madawa kweli? Maana vitani na kwenda kumfuata mtesi wako, lazima akili isiwe ya kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za usiku wakuu
Nimekua nikiona kwenye filamu mbalimbali na makala za wanajeshi hasa vitani huwa wanakula vitu flani vipo kama biskuti flani hivi,kwa imani yangu nahisi huwa wanashiba sana na kuna jamaa aliwahi nambia eti wanaweza shiba hata siku mbili,nikamuelewa kwasababu siamini kama wajeda watakua wanakula vitu kujiburudisha.Swali langu je vitu vile ni nini? Na je vinapatikana mtaani??nahitaji nivipate ili hali inapoyumba mfukoni napiga vile burudaani pasi ndefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kama biskcuits za eet samoo tu mkuu
Ukila moja umeshiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hicho wanacholishwa hakina aina fulani ya madawa kweli? Maana vitani na kwenda kumfuata mtesi wako, lazima akili isiwe ya kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
Madawa ya kujiondoa mwenyewe just in case umedakwa na adui sio?

Kwa pasi ndefu hakuna haja ya kutafuta hizo biscuits. Pika uji weka chumvi nyingi na sukari kidogo. Koroga kunywa. Hapo uta last long kidogo. Au maji vuguvugu tia chumvi Kunywa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajeshi wa nchi ya viwanda hasa wale walio jiunga na jeshi ktk miaka ya 90's hata hawajui hivyo vitu.

imesomeka!!
 
Hivyo vyakula ulivyovieleza wewe na uzito uliovipa ni 'over expectation' mkuu.

Vyakula hivyo si vyakula vya kula kama ration mkaishana, ni kama vituliza njaa tu, wakati mlo kamili upo.

Hutolewa mbadala kwa kazi za dharura zinazotegemewa kuchukua muda mrefu kumalizika katika utekelezaji wake, kabla askari husika hajarejea kambini na kupata chakula cha moto.

Vyakula hivyo hutolewa kwenye mafunzo, doria za upelelezi na doria za mapigano.

Wakiisha kurejea ama kukwama walipoenda huandaliwa vyakula vya moto kama kawaida na kupelekewa.

Vyakula hivyo ni simple sana; biskuti ngumu, maharage ya kopo yaliyokolezwa mchuzi wa nyanya na sukari ama maharage ya kopo yaliyoungwa vitunguu, chumvi na mafuta, pia na nyama za makopo (beef)na maji ya kunywa.
Ni vituliza njaa tu, hauwezi kusema eti kuna chakula cha kutumia mtu ukapata shibe ya kudumu hapo! Hakuna kitu kama hicho.

Hivyo ndivyo vya msingi, ijapo vipo vingi lakini kwa mtindo wa dry ration kutokana na tamaduni husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mkuu nimekuelewa haswaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom