ibra87
R I P
- Jul 22, 2015
- 5,614
- 5,347
Kitendo cha polisi kituo cha kigamboni kuwakamata wanawake wanaouza miili yao mchana kweupe ni udhalilishaji ambao unapaswa kukemewa kwa nguvu zote. Kuwafukuza Wanawake mchana kweupe wakiwa uchi wa
mnyama katikati ya MITAA sio sahihi kabisa.
Tunajua ni biashara ambayo inapingwa kila kona lakini hilo halihalalishi polisi kuwafanyia kama wanayoyafanya
Harafu cha ajabu polisi hao hao huwakamata Wakina mama hao na wanapofika kituoni hulipishwa faini na kuachiwa tena wakiruhusiwa kuifanya biashara hiyo. Nilichokishuhudia leo sio kitu kizuri machoni mwa watu wastaarabu. Kumfukuza mwanamke akiwa mtupu tena ukiwa askari wa kiume ni kosa kisheria.
Askari kumpiga mwanamke mpaka kuvuja damu kama maji sio kitu sahihi. kama hamuwahitaji pale kwanini msivunje vibanda vyao? Hao mnao wadhalilisha mchana kwa kuwafukuza wakiwa uchi wa mnyama ndio hao mnao wakopa mnapokuwa mmeishiwa. Alichokisema Yule mama kimewavua nguo polisi na kuwafanya wazomewe na Wananchi.
Kamanda SiRO Mulika kituo cha kigamboni kimejaa uzembe mkubwa huku askari wake wakiongoza kwa kuwasaidia wezi wa mafuta na wakati mwingine wao wenyewe kushiriki. UDHALILISHAJI WALIOUFANYA LEO SAA SITA MCHANA HAUWEZI KUFUMBIWA MACHO na hili linaweza kuleta
UHASAMA KATI YA WANANCHI NA POLISI.
BORA ASKARI WOTE WAHAMISHWE WALETWE WAPYA