Wanachama wa SIMBA SC wamekumbuka shuka kumekucha.

Wanachama wa SIMBA SC wamekumbuka shuka kumekucha.

ebaeban

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
2,205
Reaction score
2,707
Wanachama wa kilabu cha samba wamekumbuka shuka kumekucha.
Wajameni wenzenu tumecheka kweli , tunawacheka wanachama wa Kilabu cha mnyama yaani SSC kwani wanafunga zizi ng`ombe waliisha ibiwa siku nyingi. Hebu someni hapo chini;-
[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 359"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 359"]
[TR]
[TD] WAKATI Mkutano Mkuu wa wanachama wa Simba ukitarajiwa kufanyika leo Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, baadhi ya wanachama wameomba kufanyika kwa mabadiliko katika baadhi ya vipengele vilivyomo kwenye Katiba ya klabu hiyo ili kuendana na wakati.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzake, Daniel Kamna (kadi namba 100), alisema jana kwamba lengo la kutaka mabadiliko hayo ni kuendana na mfumo wa uendeshaji wa soka duniani kwa mujibu wa mashirikisho ya soka, ikiwemo la kimataifa (Fifa), Afrika (CAF), na Tanzania (TFF).
Kamna, alivitaja vipengele hivyo kuwa ni pamoja na ibara ya 26 inayohusu sifa za wagombea, ambapo kifungu cha tano kinasomeka kuwa Mwanachama akitiwa hatiani kwa kosa la jinai asigombee nafasi yoyote, hivyo wanaomba mabadiliko yasomeke: Asiwe ametiwa hatiani kwa kosa la jinai lenye adhabu ya kifungo cha zaidi ya miezi sita bila mbadala ya faini.


Pia someni pala inayofuata:- Aidha, baadhi ya wanachama wamesema kuwa katika mkutano huo lazima kieleweke kuhusu fedha zilizochangwa katika mkutano huo mwaka jana, kwa ajili ya kumalizia uwanja wa klabu hiyo kama zilifanikisha hilo, ikiwa ni pamoja na kuonyeshwa hati ya kiwanja hicho.

Wanachama hao ambao waliogopa kutajwa majina yao kwa kuwa Mwenyekiti Ismail Aden Rage anatumia udikteta wa kuwazuia kuongea katika vyombo vya habari, leo watamtaka awaonyesha kilipo kipengele hicho katika katiba, kwani huenda wao katiba zao hazina.

Wameahidi kuhoji ziliko fedha za mauzo ya mchezaji wao Emmanuel Okwi, aliyeuzwa miezi sita iliyopita na kama bado hazijatolewa, itakuwaje mchezaji wao aitumikie klabu hiyo.



Hivi wanachama wa Simba na mwenyekiti wao Rage nani mototo wa mjini zaidi,.Rage hivi kuna mtanzania asiye mjua tabia zake?

Tunawatakia kheri mkutano wao uishe salama.

Ebaeban
Tel.aviv.


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Hahahaha mzee wakupanda na mguu wa kuku jukwaani, cheza na mtt wa mjini wewe!
 
Hahahahahaha.
Mwenzio akinyolewa................................
 
Back
Top Bottom