NYARUKURURU
JF-Expert Member
- Aug 22, 2016
- 349
- 199
CHADEMA NI CHAMA CHA WAFANYA BIASHARA NA WATU WASIOKUWA NA KUMBUKUMBU.
Watanzania wenzangu tuweni makini ipo siku tunaweza kutawaliwa na Chama ambacho watu wake wanapoteza kumbukumbu kama Chadema, na walafi wa madaraka huku wakitudanganya kuwa ni watetezi wa wanyonge.
Kama mnakumbuka tarehe 15, September 2007 Chadema kupitia Katibu wao mkuu Dr,Slaa na Lissu walitaja" A list of shame" pale mwembe Yanga Tandika jijini Dar es salaam, miongoni mwa mafisadi waliotajwa ni Edward Lowasa wakimuita fisadi papa lakini kwasasa ndio boss wao mkubwa na hata kufikia kumuingiza kwenye kamati kuu kwa njia za panya, yaani kinyemera bila kufuata utaratibu.
Tundu lissu kwasasa anamtetea mpaka mapovu ya sabuni yanamtoka mdomoni kuwa ni msafi, ni hakika viongozi wa juu wa Chadema wanapoteza kumbukumbu Lowasa huyu huyu alipochukua form kugombea Urais kura za maoni kupitia CCM wapinzani walisema hasafishiki lakini alopohamia Chadema wakamsafisha kwa sabuni ya OMO mpaka katakata hadi kuwa na mvi nyeupe.
Chadema haohao walimuita Rais Kikwete kuwa ni dhaifu hapaswi kuongoza Taifa letu na kusema Taifa letu lilipofikia linataka Rais mkali, sasa tumempata Mh,Magufuli anayesimamia mambo kwa umahiri wanasema ni dikiteta hafuati katiba, cha kushangaza wamekuwa wakisema anavunja katiba lakini hawatwambii amevunja katiba kipengere kipi?
Chadema walikuwa wanasema serikali ya Mh,Kikwete ni regelege haikusanyi kodi, na sasa JPM anakusanya kodi wamegeuza kibao na kusema anafukuza wafanya biashara na wawekezaji.
Chadema hihi viongozi wake walisikika wakisema hadharani kuwa My,Kikwete ni dhaifu hawachukulii hatua mafisadi na wafanyakazi wazembe. Kwasasa Mh,JPM anawafukuza wafanyakazi wazembe na mafisadi Lissu na Mbowe wanasema anawaonea wafanyakazi asiwafukuze kuwa ni kinyume cha haki za binadamu.
Mh,Magufuli alipoanza kazi walisema anatekeleza Ilani yao lakini hawakutwambia katika ilani yao mahakama ya mafisadi imeandikwa page gani na chapter gani, kama haitoshi baada ya kuona watanzania tunamkubali JPM wakaanza kusema ni dikiteta.
Ndugu zangu watanzania kuweni makini na hawa watu tusije kuwa kama Libya walivyo danganywa kuwa tuiondoe serikali ili tulete mabadiliko, leo hii waliowadanganya wao kwa wao wamekuwa wakipigania madaraka na kuwafanya wananchi wakimbizi kuelekea Italy.
Kama kweli Mbowe ni mtetezi wa wanyonge awambie watanzania kwa nini ana miliki nyumba kubwa huko Marekani, Saud Arabia na huko South Afrika kwa kutumia ruzuku ya Chama chake inayolipwa na Watanzania Wakati Chadema ikiwa haina hata jengo la ofsi za makao makuu iliyojengwa kwa zaidi ya miaka 24 tangu kianzishwe.
Kama kweli Mbowe anawapenda watanzania wa hali ya chini atuambie kwanini yeye watoto wake wote saba wanaishi Marekani?
Hii inaonesha kuwa Mbowe na chama chake hana uchungu wowote ule na wanyonge wa nchi hii, angekuwa anatuonea huruma asingetumia Mali za chama kujenga majumba ya kifahari nje.
Ukitaka uamini maneno yangu fuatilia hotuba za Bunge letu uone ni lini imeletwa ajenda ya kuwataja watu walioficha pesa nje Mbowe akaisapoti? Hajawahi kufanya hivi kwasababu na yeye kaficha pesa nyingi huko Asia.
Ni lini imeletwa ajenda ya kupanda kwa nauli za mabasi kwenda mikoani Mbowe au Lowasa wakatetea? haijawahi na wala haitatokea kwa maana ndo wamiliki wakubwa wa mabasi nchini.
Ni lini Mbowe na Lowasa wametetea kushusha bei ya mafuta nchini? Sasa basi kama haya yote Chadema haijawahi kutetea unategemea kuwa ni sahihi ni chama cha wanyonge hiki si kweli hiki ni chama cha wafanyabiashara nchini wapiga madili wote huamia Chadema.
Mwisho ndugu zangu tumsapoti Mh,JPM ni Rais wakuigwa duniani hayumbishwi na mtu, hakika nawambieni kama Chadema waliweza kumsafisha Lowasa na kumuita mwana mabadiliko na Mh,Magufuli leo akihamia Chadema watamuita Malaika.
JPM piga kazi Mh,achana na hawa wapoteza kumbukumbu sisi watanzania tunakuunga mkono.
Imeandaliwa na wenu,
MWITA NYARUKURURU
mwitanyarukururu@gmail.com