Wanachama UPDP: Tunaendelea kumtambua Mwenyekiti wetu Fahmi Dovutwa kama Mwenyekiti halalii

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,810
11,979
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAMKO LA WANACHAMA WA UNITED PEOPLES DEMOCRATIC PARTY (UPDP)

Ndugu waandishi wa habari tumewaiteni hapa ili kuwajulisha juu ya taarifa zinazoenea na kuripotiwa na vyombo vya habari juu ya madai ya kuwepo kwa mgogoro wa kiuongozi ndani ya Chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP).

Kwa mujibu wa Katiba ya UPDP Ibara 15 (3) (d) Mamlaka ya nidhamu ya Mwenyekiti wa Chama Taifa ni Mkutano Mkuu wa Chama ambao kimsingi ndio unaomchagua Mwenyekiti lakini pia unaweza kumuondoa ikiwa kuna sababu za msingi za kufanya hivyo na si vinginevyo.

Tarehe 01/12/2019 Katibu Mkuu wa UPDP aliitisha kikao cha Halmashauri Kuu kinyume na taratibu na bila kushauriana na Mwenyekiti kama ambavyo Katiba ya UPDP Ibara ya 7 (14) (e) inavyotaka.

Kikao hicho pamoja na kuwa hakikuwa halali pia kilihudhuriwa na wajumbe ambao hawakuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu kwa hiyo hakikuwa na wajumbe halali.
Ajenda ya kikao hicho ilikuwa kutathmini hali ya Chama lakini Katibu Mkuu alibadilisha ajenda na kuleta ajenda mpya ambayo aliita Mwenyekiti kuvunja Katiba hivyo ipigwe kura ya Mwenyekiti kuvunja Katiba au kutovunja Katiba.

Kama tulivyoelezwa hapo awali mamlaka ya nidhamu ya Mwenyekiti ni Mkutano Mkuu ambao ndio unaamua hatma yake lakini katika kikao kile wakaamua kuwa Mwenyekiti avuliwe nafasi yake kinyume na Katiba.

Sisi wanachama wa UPDP tunaamini kuwa kikao hicho kilifanyika kihuni na kinyume na Katiba ya Chama na wao wanajua kikao kilichoamua hakikuwa na Mamlaka ya Kubadili uongozi wa juu wa Chama hasa Mwenyekiti wa Chama.

Kimsingi wamefanya maamuzi kinyume na Katiba ya Chama, Sheria za nchi na taratibu na wamegawana vyeo kwa watu wote wanaotoka upande mmoja wa muungano. Mfano Kaimu Mwenyekiti aliyekaimu uenyekiti kinyume cha Katiba anatoka Zanzibar, Makamu Mwenyekiti anatoka Zanzibar, Katibu Mkuu anatoka Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu hajachaguliwa na kamati tendaji Bara kinyume na ibara 16.3 (b) ya Katiba, kujaza nafasi zilizowazi katika uongozi kwa kuteua wanachama makada wa kukaimu hadi vikao vinavyohusika na uchaguzi au uteuzi.

Ndugu waandishi wa habari, baada ya kikao cha Zanzibar na maamuzi yaliyochukuliwa Mheshimiwa Dovutwa alilalamikia maamuzi hayo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa barua ya tarehe 11/12/2019 akimueleza juu ya uvunjifu wa Katiba na Sheria hata hivyo Msajili wa Vyama vya Siasa huku akijua kuwa kulikuwa na uvunjifu wa Katiba na Sheria alibariki maamuzi na ubatili ule na kusema walichokifanya kilikuwa sawa.

Baadaye tarehe 02/01/2020 Msajili wa Vyama vya Siasa aliwazuia maofisa wa Ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali pale walipotaka kuja ofisi za UPDP kwaajili ya kufanya ukaguzi.

Mfululizo wa matukio haya na mengine yanaonyesha kuwa mgogoro huu ndani ya Chama hiki umechagizwa na umetengenezwa na Msajili wa Vyama vya Siasa kama ambavyo amekuwa akifanya katika vyama vingine kuanzia mwaka 2015 baada ya Uchaguzi Mkuu.

Tumeona baada ya Uchaguzi wa Mkuu 2015 walianza kuvuruga Chama cha Wananchi CUF na tunajua mwisho wake ulivyokuwa.
Hakuishia hapo baadaye alihamia Chama cha DP na kukivuruga, akahamia SAU na kukivuruga, na sasa wamehamia UPDP na kuna mpango pia ambao tunaufahamu wa kukivuruga pia Chama cha NLD.

Ndugu waandishi wa habari kwa mujibu wa Sheria, kazi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ni ulezi kwa vyama vya Siasa na si mtengeneza migogoro. Kwa mtazamo wetu hivi sasa ameacha kutekeleza majukumu yake yaliyopo kisheria ambayo ni kulea Vyama na kuanza kuvibomoa vyama.

Sisi wanachama wa UPDP tunapenda kuwaambia wanachama wa UPDP nchi nzima kwamba waendelee kuwa imara, waendelee kukipigania chama chao na kwamba bado tunamtambua Mheshimiwa Fahmi Dovutwa kama Mwenyekiti halali wa UPDP.

Kama tulivyoeleza hapo juu chama kinaelekea kuitisha Mkutano
Mkuu tunaendelea kumtambua Mwenyekiti wetu Fahmi Dovutwa
kama Mwenyekiti halali mpaka pale ambapo Mkutano Mkuu
utaamua vinginevyo.

Sisi wanachama wa UPDP kwasasa tunamtaka Katibu Mkuu kwa kushauriana na Mwenyekiti Mheshimiwa Fahmi Dovutwa kama Katiba ya Chama inavyotaka waitishe Mkutano Mkuu kama kutakuwa na tuhuma yoyote dhidi ya Mwenyekiti ziletwe kwenye Mkutano Mkuu ili wanachama waweze kuzijadili na kuchukua maamuzi kama Katiba ya Chama inavyoelekeza.

Imesomwa na;

Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa

Asha Chuma.
IMG_20200113_110045_5.jpg
 
Hahah Dovutwa namuonaga kwny hafla zote pale ikulu na ile kofia yake,CCM hainaga marafiki Dovutwa ashapigwa fitna tayari.
Hivi ni vile vyama vya ccm. Wakiona umewageuka wanakutoa. Kosa la Dovutwa ni kususia uchaguzi wa Serikali za Mtaa. Hukumu yake atolewe. Wanaogopa asije akasusia na uchaguzi mkuu wa October 2020 kwa hiyo wanamuwahi mapemaa

dodge
 
Hivi ni vile vyama vya ccm. Wakiona umewageuka wanakutoa.
Haya ni maandalizi ya kuweka watu wao kwa upande wa Zanzibar. Si mwaka 2015 CHADEMA walipata kura nyingi kuliko CCM upande wa Zanzibar kutokana na UKAWA. Wanataka watu watakaovuruga aina yoyote ya ushirikiano wa vyama pinzani kwao.
 
Ofisi ya msajili wa vyama ni kitengo kisichokuwa rasmi cha ccm kinachotumika kudhoofisha vyama vya upinzani.

Kwenye katiba mpya inafaa ofisi hii ifutiliwe mbali na vyama visajiliwe kwenye wizara ya mambo ya ndani kama nchi zingine zinavyofanya.

Kwa utaratibu huu wa sasa huyu msajili ni kibaraka tu anayetumiwa na rais kukidhi malengo yake ya kisiasa ikiwemo kuhujumu vyama pinzani.
 
Back
Top Bottom