Wanachama 50 wa CCM watimka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanachama 50 wa CCM watimka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ilumine, Nov 4, 2009.

 1. Ilumine

  Ilumine Senior Member

  #1
  Nov 4, 2009
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Adam Fungamwango
  Bundi bado anaendelea kulia kwenye tawi la CCM Mwananyamala Kisiwani, baada ya watu wanaodaiwa kuwa ni wanachama wa chama hicho kutimkia chama cha upinzani cha CHADEMA.
  Mweka Hazina wa CHADEMA katika Kata ya Makumbusho, Amir Hussein Ikoi, amesema kuwa amepokea wanachama 50 wa CCM ambao wamekiacha chama hicho na kujiunga na chama chao.
  Taarifa za kutimkia CHADEMA kwa wana CCM hao ni muendelezo wa madai ya kutokea mpasuko uliojitokea kwenye tawi hilo la ccm Mwananyamala Kisiwani mara baada ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kumalizika.
  CCM, wenyewe kwa wenyewe walikuwa wakishutumiana wakati wa kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwa walikuwa vigeugeu wakiwemo baadhi ya viongozi wa tawi, ambao walikuwa wakiipigia debe CUF na kuiwezesha kushinda kwenye kinyang'anyiro hicho.
  Sababu ilielezwa kuwa ni kisasi cha wao kwa wao, hasa kwavile mgombea waliokuwa wakimtaka apitishe aligonga mwamba.
  Kutokana na hali hiyo, ilizuka tafrani kubwa kwenye tawi hilo, baada ya wanachama kufunga ofisi za tawi na kuwataka viongozi wajiuzulu.
  "Nafurahi kuwa nimepokea wanachama 50 wapya toka CCM... na hao ni wachache, waliokuwa wakitaka kadi ni wengi, ila zikaaniishia tu. Hivi sasa nataka kwenda makao makuu nikachukue kadi nyingine ili nivune wanachama wengi zaidi toka CCM," akasema Ikoi.
  Mweka Hazina huyo amesema kuwa kutokana na chama sasa kuwa na wanachama wengi, kinatarajia kufungua ofisi yake na ana uhakika kujiimarisha ili waweze kuingia kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Madiwani.
  "Hata mwaka huu, tumeshiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa Mwananyamala Kisiwani, lakini mgombea wetu Hamadi Namkambe ameshindwa kwa kupata kura 17...ila hiyo haitukatishi tamaa," akasema.
  Ikoi amewataka wana CHADEMA ngazi za juu, kuangalia pia mizizi na kusema kuwa chama hicho kinaonekana kusahau kuweka mizizi chini na badala yake kuangalia zaidi ngazi za juu.
  Akasema katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, walitumia gharama zao wenyewe kwenye kampeni, huku yeye akilazimika kuuza ng'ombe wake wawili wka ajili ya kuimarisha nguvu za chama chao.  CHANZO: ALASIRI
   
Loading...