Wanachama 1,550 wa CCM watimkia CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanachama 1,550 wa CCM watimkia CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DOCTORMO, Feb 6, 2011.

 1. D

  DOCTORMO Member

  #1
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana kikiadhimisha miaka 34 tangu kianzishwe, zaidi ya wanachama wake 1,550 wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Maswa, Luhende Mipawa, alisema kuwa wanachama hao wamerudisha kadi hizo kwa wakati tofauti siku tatu tangu CCM ilipozindua maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa chama hicho.

  “Tangu CCM walipozindua sherehe zao za kutimiza miaka 34, tumepokea wanachama wapatao 1,550 kutoka matawi mbalimbali ya CCM katika Wilaya ya Maswa ambao wamejiunga na chama chetu,” alisema.

  Alisema kuwa dalili hizo zinaonyesha wazi wananchi wa wilaya hiyo walivyo na imani kwa CHADEMA wanachokiamini ndicho chama kikuu cha upinzani hapa nchini.

  “Hizi ni dalili njema kuwa wananchi wanakikubali chama chetu ndiyo maana unaona kwa muda wa siku tatu tumevuna wanachama 1,550, tuna kazi kubwa ya kutimiza kiu kubwa ya wananchi wetu,” alisema.

  Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, mmoja wa wanachama wa CCM aliyehamia CHADEMA, Geni Jilala, alisema kuwa kwa sasa chama hicho kimekosa mwelekeo na kupoteza misingi iliyowekwa na Mwalimu Nyerere na matokeo yake kimekuwa ni cha kuwatumikia wenye fedha huku wanyonge wakiachwa, hivyo CHADEMA ndiyo chama mbadala.

  “CCM ya leo inawakumbatia wenye fedha, kwani ndiyo wana sauti ndani ya chama, sisi wanyonge tumeachwa, hivyo tumeona heri tukimbilie CHADEMA ambacho ndicho chama cha wanyonge,” alisema Jilala.

  Aliongeza kwamba kutokana na mgawanyiko na makundi yanayokitafuna chama hicho wilayani humo, kuna hatari ya kusambaratika na kubaki na jengo la ofisi.

  Hivi karibuni Katibu wa Uenezi wa CCM Taifa, Kapteni John Chiligati, alishindwa kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Maswa katika viwanja wa MADECO, baada ya wananchi kutojitokeza kwa madai kuwa chama hicho hakina jipya la kuwaeleza wakazi wa mji HUO
  HUU NI MWANZO TU WAUNGWANA KWAJINSI NINAVYOONA ANGUKO KUBWA KWA SASA NI 60% KUJOIN UPINZANI NA KUIKOMBOA NCHI.
   
 2. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hii ni safi sana, wimbi hili liendelezwe mpaka maeneo mengine pia. CHADEMA kijipambanue kama Chama Cha Wanyonge na CCM Chama Cha Mafisadi.
   
 3. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Good news
   
 4. z

  zamlock JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  safi sana inatia moyo kwa watu wenye uchungu na nchi yao kama wana maswa safi sana na tuko pamoja tutawapa moyo zaidi na sisi tuko nyuma yenu kwa mapinduzi ya nchi hii na iko siku tutafika pale ikulu na wananchi watabadilishiwa maisha kwa mikakati mizuri itakayo wekwa na chama makini chadema
   
 5. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  ccm lazima ianguke Maswa kwasababu Kikwete anathamini urafiki kuliko uhai wa chama chake. Huyo DC wake pale ni mtu asiye na maadili lakini kwasababu ya kujuana[ hata pale anapomdhalilisha yeye Ras hadharani] hamchukulii hatua za kinidhamu!!Hii inaonesha udhaifu wa uongozi.
   
 6. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  this is a very good news. Taifa lazima likombolewe.
   
 7. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,954
  Likes Received: 1,279
  Trophy Points: 280
  Saaafi sana. Hivi Tanga na Dodoma wamelogwa? Mbona hawabadiliki. Kusini wanabadilika kwa kasi. Shinyanga iingwe na Wagosi
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Na bado, huu ni mwanzo tuu. Kama vuguvugu limehamia vijijini huo ni msiba kwa CCM
   
 9. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kilicho bakia ni kuyachoma hayo majumba ay magofu ya ccm ili yasiwepo kabisa kwenye kumbukumbu ya mtanzania. :roll:
   
 10. mwanaharakati m

  mwanaharakati m Member

  #10
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  safi, CHADEMA sasa ipange mikakati ya kuwafanya wananchi wanaokikimbilia waone kuwa kweli ni kimbilio lao; wawaandalie platfoam vijana wapaze sauti na kuwavutia vijana wenzao, sababu vijana wengi wanapenda CDM lakin CHADEMA bado haija watengenezea jukwaa la wao kujisikia nyumbani na kuonyesha kwamba viongoz wa CDM wanatambua uwepo wao..nashauri CHADEMA waimarishe BAVICHA(baraza la vijana) ili wanapojiunga kama hivi waweze kusaidia kujenga matawi mikoani na kuhamasisha watu zaidi.........vijana ni rasilimali ambayo CHADEMA inayo lakini haiitumii ipasavyo.
   
Loading...