Elections 2010 Wanachadema wakiri: Chadema ni chama cha Chuki na Fitna

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
naam leteni habari, kama kweli nyie chama makini mbona jamaaa wameamua kuachia mchuma?

chadema kelele na mbio zao ziko humu tu lkn kule hamna lolote zaidi ya hayo aliosema kada wenu

Kikwete aiumiza Chadema

SIKU 10 tangu aanze kampeni za kuomba kuongoza tena Tanzania kwa miaka mitano ijayo, mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), Jakaya Kikwete, ameanza kuvutia wapinzani wake kisiasa kwa sera na kuungana naye katika safari hiyo ya kuomba
kurejea Ikulu.

Chama cha kwanza kupoteza wanachama wake wakiwamo viongozi wa juu wa ngazi ya mkoa ni Chadema, ambayo leo kimepoteza wanachama 367 na viongozi wa mkoa akiwamo Katibu wa Mkoa wa Mbeya, Ipyana Seme.

Kikwete aliyezindua kampeni za CCM kwenye viwanja wa Jangwani, Dar es Salaam, Agosti 21 mwaka huu, tayari amepita mikoa ya Mwanza, Kagera, Kigoma, Rukwa na Mbeya, ambako leo alipokea wanachama hao kutoka Chadema waliomweleza kuwa sera zake safi, zimewavutia kujiunga naye.

Mbali na Seme ambaye amekuwa Katibu wa Chadema wa Mkoa kwa miaka mitano na Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Mbeya Vijijini kwa miaka 15, wengine alioondoka nao ni Mwenyekiti wa Wanawake wa Wilaya na Diwani wa zamani, Martha Seme.

Pia wamo Mweka Hazina wa Wilaya, Lilian Peter; Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Wilaya, Reuben Ndilo; Mjumbe wa Halmashauri ya Wilaya, Fatuma Diwani; Mwenyekiti wa Vijana wa Kata ya Utengule Usongwe, Frank Kasambala na Mshauri wa Wanawake wa Wilaya, Salome Anganile.

Viongozi hao walipokewa na Kikwete kwenye mkutano wa kampeni jana asubuhi kwenye stendi kuu ya mabasi ya Mbalizi, Mbeya Vijijini.

Akizungumza kabla ya kurejesha kadi yake ya Chadema na nyingine za wanachama 367 na kukabidhiwa ya CCM na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Kikwete, Seme alisema anaondoka Chadema kwa sababu amegundua CCM ina Ilani safi ya Uchaguzi, sera safi na imefanya maendeleo makubwa chini ya uongozi wa Kikwete.

“Leo ni heshima kubwa kwangu kusimama hapa mbele ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete. Nimekuwa katika chama ambacho leo nakipungia mkono wa kwa heri kwa miaka mingi. Lakini naondoka kwa sababu nimegundua sera nzuri,” alisema Katibu huyo wa Chadema wa Mkoa.

“Nilikuwa Askofu wa kubatiza watu na kuwapeleka Chadema, lakini sasa naondoka na viongozi saba wa wilaya, madiwani na wanachama 367. Narudi CCM. Tumeona mengi yaliyofanywa na CCM. Kule kwa wengine ikiwamo Chadema, kazi yao ni fitina, majungu, kugombanisha watu na matusi.

“Mheshimiwa Kikwete nchi inakupendeza, mwenyewe unapendeza na watu wanakupenda,” alisem,a na kuongeza kwamba ataiimarisha CCM Mbeya Vijijini ili kuhakikisha inashinda urais kupitia kwa Kikwete; ubunge kupitia kwa Mchungaji Luckson Mwanjale na madiwani wote.

Awali, maelfu ya wakazi wa Mbalizi walimpa mapokezi makubwa na
baadhi yao wakiwamo walimu wanachama wa Chama cha Walimu Mbeya Vijijini, walibeba mabango yenye ujumbe wa kumwahidi kura, licha ya madai kwamba mgombea huyo amekataa kura za wafanyakazi nchini.

Baadhi ya mabango hayo yalisomeka, “Hata wakuzushie eti huzitaki kura za wafanyakazi, sisi walimu wana Shirikisho tunakuahidi bila woga hatutapangiwa nani tumpe kura zetu, zaidi yako wewe viongozi wetu mpendwa unayetujali na kututhamini.”

source: HabariLeo | Kikwete aiumiza Chadema
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom