WanaCCM Vyuo Vikuu DSM watunukiwa vyeti

Omary Kipingu

Member
Feb 22, 2016
40
48
*WANACHAMA 681 KUTOKA UMOJA WA VIJANA WA CCM VYUO NA VYUO VIKUU MKOA WA DAR ES SALAAM WATUNUKIWA VYETI VYA KUHITIMU MASOMO YAO*.

Ni mahafali ya pili ya CCM Vyuo vikuu dar Mgeni rasmi Naibu katibu mkuu CCM Tanzania Bara Comrade Mpogolo..Pia viongozi mbalimbali walikuwepo:

Kaimu Katibu mkuu UVCCM Taifa comrade Shaka Shaka,;

Kaimu katibu mkuu idara ya vyuo vikuu UVCCM Taifa comrade Daniel Zenda

hawa wote
IMG-20170528-WA0438.jpg
walikuwepo katika kuwapongeza vijana wa CCM vyuo vikuu kwa kuhitimu masomo yao.

*“Ujana ni rika, ujana ni wakati na wakati haurudi nyuma”* haya yalizungumzwa na mgeni rasmi Ndg. Rodrick Mpogoro Naibu katibu Mkuu CCM Bara kwenye mahafali ya Vijana Chama Cha mapinduzi kutoka Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika leo 28/05/2017 katika ukumbi wa King Solomoni Kinondoni.

Ndg. Rodrick Mpogoro alisema, Siri pekee ya kufanikiwa kwa mtu yeyote inategemea namna anavyotazama na kutathmini mambo. Ni mtazamo chanya pekee ndiyo humvusha mtu kwenye mafanikio, hivyo ipo haja kwenu vijana kujikita kutazama fursa zinazowazunguka na kuwa wabunifu ili kujitengenezea vipato vyenu wenyewe kuliko kusubiria ajira, alisema.

"Sura ya Chama Cha Mapinduzi inajengwa na wanachama wenyewe kwa vitendo, jengeni uadilifu, zungumzeni habari ya uzalendo wa nchi yenu, jengeni maslahi kwa wanyonge, jifunzeni historia ya Chama, someni katiba na kanuni zake, fanyeni kazi kwa bidii na jengeni moyo wa kujitolea mkifanya hayo mtafanikiwa*. Alisema.

Alifahamisha kuwa ni vyema kwa wanachama, wananchi na kila mpenda amani, umoja na maendeleo ya Taifa kuendelea kumuunga mkono Rais wetu Mhe Dr. John Pombe Magufuli katika juhudi anazozifanya za kupambana na ubadhilifu wa mali za umma kwani anaiishi misingi ya Chama Cha mapinduzi kama ilivyoainishwa kwenye madhumuni yake kupitia katiba Ibara ya 5. *"Simameni imara katika kumuunga mkono Rais wetu kwani anaiishi misingi ya Chama Cha Mapinduzi katika kujenga uzalendo wa nchi"*.

Mahafali hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama akiwemo Ndg. Shaka Hamdu Shaka K/Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndg. Daniel Zenda Kaimu Katibu wa Vyuo na Vyuo vikuu, Uongozi wa Senate Mkoa wa Dar es salaam Vyuo na Vyuo vikuu na makada kutoka vyuo mbalimbali vya mkoa wa Dar es Salaam.

*Sherehe hii ilihudhuria na wanachama takribani 1,100* kutoka matawi ya vyuo mbalimbali vikiwemo DUCE, UDSM, DIT, ST. JOSEPH, ST.JOHN, MWL NYERERE, TAASISI YA WATU WAZIMA, IMTU, DMI, TIA, DIPLOMASIA, BAGAMOYO, CBE, DIT, KIU, MABIBO HOSTEL, CHUO CHA MAJI, IFM n.k ambao miongoni mwao walikuwemo wanachama waliotunukiwa vyeti vya kuhitimu masomo yao.
IMG-20170528-WA0425.jpg
IMG-20170528-WA0427.jpg
IMG-20170528-WA0433.jpg
IMG-20170528-WA0426.jpg
 
IMG_20170528_215715_719.jpg

IMG_20170528_215458_026.jpg

IMG_20170528_215458_031.jpg
 
*WANACHAMA 681 KUTOKA UMOJA WA VIJANA WA CCM VYUO NA VYUO VIKUU MKOA WA DAR ES SALAAM WATUNUKIWA VYETI VYA KUHITIMU MASOMO YAO*.

Ni mahafali ya pili ya CCM Vyuo vikuu dar Mgeni rasmi Naibu katibu mkuu CCM Tanzania Bara Comrade Mpogolo..Pia viongozi mbalimbali walikuwepo:

Kaimu Katibu mkuu UVCCM Taifa comrade Shaka Shaka,;

Kaimu katibu mkuu idara ya vyuo vikuu UVCCM Taifa comrade Daniel Zenda

hawa wote View attachment 515793walikuwepo katika kuwapongeza vijana wa CCM vyuo vikuu kwa kuhitimu masomo yao.

*“Ujana ni rika, ujana ni wakati na wakati haurudi nyuma”* haya yalizungumzwa na mgeni rasmi Ndg. Rodrick Mpogoro Naibu katibu Mkuu CCM Bara kwenye mahafali ya Vijana Chama Cha mapinduzi kutoka Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika leo 28/05/2017 katika ukumbi wa King Solomoni Kinondoni.

Ndg. Rodrick Mpogoro alisema, Siri pekee ya kufanikiwa kwa mtu yeyote inategemea namna anavyotazama na kutathmini mambo. Ni mtazamo chanya pekee ndiyo humvusha mtu kwenye mafanikio, hivyo ipo haja kwenu vijana kujikita kutazama fursa zinazowazunguka na kuwa wabunifu ili kujitengenezea vipato vyenu wenyewe kuliko kusubiria ajira, alisema.

"Sura ya Chama Cha Mapinduzi inajengwa na wanachama wenyewe kwa vitendo, jengeni uadilifu, zungumzeni habari ya uzalendo wa nchi yenu, jengeni maslahi kwa wanyonge, jifunzeni historia ya Chama, someni katiba na kanuni zake, fanyeni kazi kwa bidii na jengeni moyo wa kujitolea mkifanya hayo mtafanikiwa*. Alisema.

Alifahamisha kuwa ni vyema kwa wanachama, wananchi na kila mpenda amani, umoja na maendeleo ya Taifa kuendelea kumuunga mkono Rais wetu Mhe Dr. John Pombe Magufuli katika juhudi anazozifanya za kupambana na ubadhilifu wa mali za umma kwani anaiishi misingi ya Chama Cha mapinduzi kama ilivyoainishwa kwenye madhumuni yake kupitia katiba Ibara ya 5. *"Simameni imara katika kumuunga mkono Rais wetu kwani anaiishi misingi ya Chama Cha Mapinduzi katika kujenga uzalendo wa nchi"*.

Mahafali hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama akiwemo Ndg. Shaka Hamdu Shaka K/Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndg. Daniel Zenda Kaimu Katibu wa Vyuo na Vyuo vikuu, Uongozi wa Senate Mkoa wa Dar es salaam Vyuo na Vyuo vikuu na makada kutoka vyuo mbalimbali vya mkoa wa Dar es Salaam.

*Sherehe hii ilihudhuria na wanachama takribani 1,100* kutoka matawi ya vyuo mbalimbali vikiwemo DUCE, UDSM, DIT, ST. JOSEPH, ST.JOHN, MWL NYERERE, TAASISI YA WATU WAZIMA, IMTU, DMI, TIA, DIPLOMASIA, BAGAMOYO, CBE, DIT, KIU, MABIBO HOSTEL, CHUO CHA MAJI, IFM n.k ambao miongoni mwao walikuwemo wanachama waliotunukiwa vyeti vya kuhitimu masomo yao.View attachment 515787View attachment 515788View attachment 515789View attachment 515790

Sisi inatuhusu nini???
 
Hapo bado hatujaanzisha chuo chetu kwa ajili ya makada, chadema endelea kutumia ruzuku kusafiri dubai
 
Bila shaka hapo kuna walimu wa masomo ya Arts waliograduate
Wasitegemee uteuzi wajiajiri
 
Back
Top Bottom