Wana_CCM wachoma nyumba za wafuasi wa upinzani Kigoma Kusini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana_CCM wachoma nyumba za wafuasi wa upinzani Kigoma Kusini

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kingwipa1, Nov 2, 2010.

 1. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Habari nilizopata usiku ni kwamba kuna nyumba takribani tano zimechomwa maeneo ya Nguruka baada ya matokeo ya awalu kuonyesha NCCR-Mageuzi inaongoza kwenye kiti cha ubunge. Eneo hilo ambalo limo ndani ya jimbo la Kigoma Kusini ambalo lilikuwa na upinzani mkubwa kati ya David Kafulila (NCCR) na Gulam Kifu (CCM) ndio ngome kubwa ya mgombea wa CCM kwani ni mahali alipozaliwa. Kutokana na wakazi wengi wa eneo hilo kuchoshwa na Gulam kwa tabia yake ya kuwa karibu na wahalifu watu waliamua kumtenga ingawa wanakaa naye na kumkubali kijana Kafulila. Baada ya Gulam kushindwa kwa kura nyingi ndani ya eneo lake inasemekana wafuasi wake waliamua kuchoma nyumba za watu wanaosadikika ni wafuasi wa NCCR-Mageuzi. Na mpaka jana usiku nyumba tanao zilikuwa zimeshachomwa.
  Gulam Kifu amewahi kushind ubunge akiwa Chadema na NCCR-Mageuzi na baadae kupoteza nafasi kwa kushindwa kesi na kuenguliwa. CCM kwa kuna kuwa kijana huyo ana nguvu katika jimbo hilo waliamua kumshawishi kujiunga nao ambapo walifanikiwa Wakati wakifanya hivyo hawakujua kuwa ndugu Gulam ameshapoteza umaarufu eneo hilo na kuwa wakazi wa maeneo hayo wanamuona kama chanzo cha vurugu nyingi na matukio ya wizi katika maeneo yao.

  Source: reliable source - kutoka huko
   
 2. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Lt. Gen. Shimbo yuko wapi mpaka yote haya yanatokea au anasubiri yale ya Urais?
   
Loading...