Wana Wa Mapokeo.

Wana Wa Mapokeo.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
WANA WA MAPOKEO.

1)napohisi kuna jambo,akili inanituma.
Nitunge niache tambo,fani izidi kuvuma.
Wengi wetu tuna mambo,twalea kwa kulalama.
Sisi wana mapokeo,wana huru watuacha.

2)wengine washika fimbo,fani wazidi kuzama.
Kwetu wengi majigambo,vibuti twenda kusema.
Wao wawatoa ng'ambo,wafanya kitaaluma.
Sisi wana mapokeo,wana huru watuacha.

3)fulusi kwao ni nyimbo,sanaa iwe uzima.
Hivi hatuumwi tumbo,anha ni mwaka na zama.
Yafike kwa kina rambo,tubaki tukitazama.
Sisi wana mapokeo,wanahuru watuacha.

4)hii fani siyo urimbo,uivalie pajama.
Si kaniki ya kitambo,ama fahali wa ndama.
Lau tumshike jumbo,ndovu anapoungama.
Sisi wana mapokeo,wanahuru watuacha.

Shairi=WANA WA MAPOKEO.

Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255642010160.
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom