Wana-Singida tunasubiri UKAWA, tumechoka na porojo za CCM

Riziki Magembe

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
887
0
Nipo katika mji wa Singida katika mitaa ya Mitunduruni,Posta,Mwenge,Namfua na stand wananchi wengi wanasema wao wamechoka na porojo za CCM wanasubiri UKAWA na wanaunga mkono UKAWA kwa kuwa wanatetea katiba inayotokana na mawazo waliyotoa mbele ya tume ya Warioba lakini CCM wanayadharau.

Pili wanasingida wanasema CCM tumewapa nchi badala ya kuleta maendeleo wao wanaleta ahadi mpya kupambana na UKAWA na kueneza propaganda maendeleo hatuyaoni.

Kubwa wanasema Singida wana utajiri wa madini ya urenium lakini hadi leo hayana msaada kwa wanasingida.

Kubwa kabisa mkoa wa Singida wananchi wake wamepigika sana na hakuna msaada kwa CCM zaidi ya porojo.

Hivyo wao kama wanasingida wamekwenda uwanjani kwa CCM kwa kuwa wamelipiwa nauli,pili wamepewa posho na tatu kuagana na CCM maana kuanzia Octoba serikali za mitaa hawana chao na mwakani ndio kwishaaa.

UKAWA ndio habari ya Singida kupitia CHADEMA jembe lao.
 
Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,202
2,000

Hivi Tundu Lissu kafanya nini kuleta maendeleo kwenye Jimbo la Singida Mashariki? Tunasikia tu anazuia wananchi kuchangia maendeleo huku hata yeye hachangii!
 
Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,007
2,000
Nilimsikia Nape akituambia waliokuwa wanatoka mkutanoni kuwa walikuwa wanakwenda kunywa maji na wangerejea!!!!!!!!!!!!
 
kirikuu10

JF-Expert Member
May 4, 2014
249
0
Hivi Tundu Lissu kafanya nini kuleta maendeleo kwenye Jimbo la Singida Mashariki? Tunasikia tu anazuia wananchi kuchangia maendeleo huku hata yeye hachangii!

Kwani wabunhe wa ccm wamefanya nini kwenye majimbo yao? Shida za singida ndio shida za wanachi nchi nzima acheni unafiki.taja ni tatizo gani lipo singida na mikoa mingine halipo? Zaid zaidi singina wametuzidi michango ya kipuuzi yenye lengo la kulisha mafisadi nooo!
 
yunuskb

Member
Apr 2, 2014
55
0
Mtu anaeshabikia CCM, kama hajalipwa posho ili atetee CCM, bac babake ni fisadi au ye yeye mwenyewe ni mwizi, kwa mtu anaeelewa historia ya nchi hii, na rasilimali zilizopo, alafu akaangalia mambo yanayofanywa na hawa watu, alafu ukaangalia umaskini walionao watanzania, alafu ukiritimba na rushwa kwenye taasisi za umma, HUWEZI KUTHUBUTU KUIUNGA CCM MKONO, tuamke watanzania, CCM wanatumaliza, tuache kuridhika na ujinga wa CCM, nchi hii haijalaaniwa mpaka tuwe maskini kihivyo
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
20,364
2,000
CCM wanakodi vijana wa bodaboda, magari kusomba watu toka vijijini - then wanajidanganya wenyewe kwa wenyewe mkutanoni - UKAWA ni mpango wa Mungu!!

Hili suala la katiba halitaiacha CCM salama -- amini amini nawaambieni.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom