Wana ndoa haya ya kweli?

Wana ndoa haya ya kweli?

nyabibuye

Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
83
Reaction score
16
Heshima kwenu wadau!

Jana katika mazungumzo yangu na marafiki zangu nilipata kusikia hoja ngeni kwangu, rafiki yangu huyu anadai 90% ya wanandoa wanaotumia usafiri wa pamoja kwa maana ya gari lao waendapo kazini au kwenye shughuli zao asubuhi hawaonekani kufurahi wala kucheka.

Ina maana kuwa hakuna mazungumzo ya hapa na pale yanayoambatana na bashasha, na ikitokea ukaona mwanamke au mdada na mwanaume wako ndani ya gari na wanacheka na kufurahi eti walio wengi si wa na ndoa.

Nimeona nifanye kuuliza kwa wadau hapa, Je ni kweli hali hiyo ipo na inasababishwa na nini hali hiyo?
Asanteni!
 
Siyo kweli. Ni vile tu siyo kila siku mtu unakuwa na bashasha za kucheka cheka au kufurahi.
 
Wana ndoa wana kazi

Kwa hiyo mlitaka wachekecheke tu kwenye gari
 
huu nao ni utafiti, ccm itatawala milele.
 
Sio kweli.labda anaowaonaga ivo ndo walivyo ila sio kua ni wanandoa wote.
 
Sasa wajichekeshe kwani wanatongozana? hilo la kujichekesha liliwapita zamani, hapo kila mtu serious na maisha, huku shule wanangoja school fees, umeme unataka kulipwa, shangazi mgonjwa anakuja Dar kutibiwa, mwingine shule huko kisha mtoa meno mwenzake, dawasco washakutumia meseji kama hujalipa wanakuja kukata maji. Fundi wa gari anadai hela zake alizobadilisha breki. Huku bar maid kapiga simu asubuhi asubuhi anadai pesa za mzee alipokuwa anaweka heshima bar. Jana katika kuweka heshima bar, umerudi umelewa nyang'anyang'a game likakushinda...

Kuna kucheka hapo?
 
Hahahaahhahhah!!!!!!!! Unaanzaje labda kuchekacheka..
 
sasa wajichekeshe kwani wanatongozana? Hilo la kujichekesha liliwapita zamani, hapo kila mtu serious na maisha, huku shule wanangoja school fees, umeme unataka kulipwa, shangazi mgonjwa anakuja dar kutibiwa, mwingine shule huko kisha mtoa meno mwenzake, dawasco washakutumia meseji kama hujalipa wanakuja kukata maji. Fundi wa gari anadai hela zake alizobadilisha breki. Huku bar maid kapiga simu asubuhi asubuhi anadai pesa za mzee alipokuwa anaweka heshima bar. Jana katika kuweka heshima bar, umerudi umelewa nyang'anyang'a game likakushinda...

Kuna kucheka hapo?

nakubali mkuu! Maisha magumu. Kucheka ni cku ya honey moon!
 
Wacheke cheke ovyo kwani matahaira??????
 
Itakuwa kutoa lift kunasababisha mnawaharibia faragha yao ndio maana wanapoteza furaha.
 
wana mambo mengi kichwani.......kwahiyo hawawezi kucheka hovyo ........
 
Tumeongea na kucheka sana home, tuendelee na barabarani? Isitoshe miaka 15 tuliyoishi pamoja tumeongea sana, tumecheka sana! Kwa hiyo kuongea na kucheka kwetu sio issue kivile.
 
Sasa wajichekeshe kwani wanatongozana? hilo la kujichekesha liliwapita zamani, hapo kila mtu serious na maisha, huku shule wanangoja school fees, umeme unataka kulipwa, shangazi mgonjwa anakuja Dar kutibiwa, mwingine shule huko kisha mtoa meno mwenzake, dawasco washakutumia meseji kama hujalipa wanakuja kukata maji. Fundi wa gari anadai hela zake alizobadilisha breki. Huku bar maid kapiga simu asubuhi asubuhi anadai pesa za mzee alipokuwa anaweka heshima bar. Jana katika kuweka heshima bar, umerudi umelewa nyang'anyang'a game likakushinda...

Kuna kucheka hapo?

hahahahaaaaaa.... dadangu hapa umemuela vema sana....kiufupi maisha yamekaba... kuchekacheka ilishapita...
 
Back
Top Bottom