Wana-MMU hebu niambieni mimi ni mwanaume wa ajabu?

Mke mmoja huwezi kuwa na furaha, hapo unafurahia furaha ya familia yako... sio furaha yako deep down unaigiza tu.
Mkuu, pole sana kwa mawazo yako potofu.
Nijuvyo mimi, furaha yako ni wewe mwenyewe ndie mwenye jukumu na wajibu wa kuitengeneza.
 
Mkuu, pole sana kwa mawazo yako potofu.
Nijuvyo mimi, furaha yako ni wewe mwenyewe ndie mwenye jukumu na wajibu wa kuitengeneza.

Sahihi kabisa, ila tu ujue sio rahisi kujua kama ni kweli unafurahia wewe... au unafurahia tu kuona familia yako ina furaha.

Sitarajii unielewe kirahisi, ila kama ni kweli unafurahia mke mmoja basi umebarikiwa sana.

Hongera mkuu!
 
Kupata pesa kidogo tu ushaanza kuona watoto watakumalizia muda wako wa kuenjoy life.. Wafaransa wana kauli yao ya kusema kuwa "La finale est la vieillesse" kibongobongo tunaweza kumaanisha kuwa "Fainali ni uzeeni"
 
Tumia mbinu za life skills kuna concept mbili decision making na problem solving ukizi-combine zitakusaidia kufanya maamuzi mazuri kwako
 
Saaawa hutaki sisi hatujabisha
Tatizo linakuja waaaapi, , Mbeeeegu za kutungisha mimba unazooooo?
 
Habari zenu wana-MMU.

Nataka maoni yenu katika hili swala. Swala hili linaonekana la ajabu kutokana na mila na tamaduni zetu za ki-Afrika ila SIO DHAMBI kabisa.

Mimi siitaji kuja kuwa na mtoto katika maisha yangu yote ila nataka kuoa niwe na mke TU. Hii ni kawaida sana kwa nchi za ulaya na marekani unakuta kuna familia/ndoa za namna hii nyingi sana lakini sio hapa Afrika. Hapa nyumbani(Tanzania) formula ni Ndoa = Watoto.

Ili ndoa ionekane imefanikiwa basi iwe na watoto japo mimi binafsi siamini hivyo.

Katika maamuzi hayo yawezekana ntakumbana na changamoto nyingi, lakini Kubwa ni Kupata mwanamke ambae atakubali kuwa ndani ya ndoa bila mtoto.

Wana MMU nipeni maoni yenu kuhusu hili swala kwa sababu sijiskii KABISA kuwa nina deni la kuwa na mtoto, sina tatizo lolote kiafya la kunizuia kuwa na mtoto ila SITAKI TU.

1. Mna maoni gani ?

2. Je, kuna msichana ambae anataka kuolewa lakini hana mpango wa kuzaa ?(kama baadhi ya wanawake wa ulaya/marekani)

Asanteni, mchana mwema.
Mm nina dada mmoja rafiki yangu, yeye ni mkenya. Nae aliniambia anataka kuolewa lkn hataki kuwa na mtoto..
So ni uchaguzi wa maisha yako uliyo chagua hi hivyo ni sahihi pia kwa sababu maisha yako ni maamuzi yako. Hakuna mtu atakaye kuchagulia namna ya kuishi.
Ni hayo tu mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kitu muhimu kama watoto kwa sasa huwez ona umuhimu wao ila uzeen au ukipata shida mke anaweza kukukimbia ukiwa na shida lakn watoto hawawez kukuacha
 
Back
Top Bottom