WANA-MAGAZIJUTO NA MSHAHARA WA TSh.315,000/= | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WANA-MAGAZIJUTO NA MSHAHARA WA TSh.315,000/=

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by NasDaz, Aug 22, 2010.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  [FONT=&quot]Nilitoa changamoto kwamba nieleweshe ni namna gani tunaweza kuwa na mapato ya ziada yatakayoweza ku-accomodate mshahara wa kima cha chini wa Sh.315,000/=! Kama kawaida yao, hamna aliyejibu hoja mbali ya matusi! Hata hivyo, angalau mtu mmoja akajaribu kukokotoa ni namna gani Sh.315,000 inavyoweza kulipika( Ingawaje mie nilihitaji bajeti ya mapato, na sio matumizi)! Akapiga hesabu zake, na kutoa figa isiyofika hata Trilioni 2 endapo serikali itaamua kulipa kiwango hicho! Mantiki yake ilikuwa kwamba, JK ni muongo kwa madai yake kwamba endapo kima kitapanda hadi Sh.315,000 basi bajeti ya mshahara itakaribia Sh. Trilioni 6 (wakati mapato hayafiki hiyo Trilioni 6!) Akatokea mwana-JF aliyeniona mimi ni sawa na mbumbumbu coz' siwezi kufanya hata simple mathematics!! Mwana JF huyu akaweka assumption kwamba wafanyakazi wa serikali wanafikia laki nne, hivyo kwa mshahara wa Sh.315,000 (xlaki 4) plus zile zinazoenda kwenye pension funds hazifiki hata Trilion 2! Huyu bwana, akanikejeli kwamba eti pamoja na umbumbu wangu sitashindwa kuifahamu hesabu ndogo kama hiyo!!!! Sasa ndo najiuliza, ina maana kima cha chini kikiwa Sh.315,000/= ina maana from hapo gvt salaries zitakuwa flat rates!? Huyu bwana nae, anajigamba eti ni GREATEST THINKER; ingawaje hafahamu kwamba hakuna ki2 kinachoitwa flat rates kwenye mishahara! Huyu bwana na wenzake(Greatest thinkers) hawajui hata kidogo kwamba unavyopandisha mshahara wa chini, almost the whole aggregate payroll ita-shake! [/FONT]
  [FONT=&quot]Mimi sina mengi ninayofahamu kuhusu serikalini lakini b4 sijaandika huwa nachunguza kidogo kuliko kukurupuka! According to Tangazo la Kazi lililokuwa limetolewa na Sekretarieti ya Ajira ya Utumishi wa Umma (Daily News April 21,2010) nilikuta the Lowest Grade ni Grade TGOS. A( ambayo slary scale yake ni btn TZS. 104,410 to TZS. 146,570). Grade hii inachukuwa watu kama wasaidizi wa ofisi(wapika chai, wafagizi, and the like) na walinzi! Likewise, fresh graduates wanaanza na Grade D (for non science oriented graduates) ambayo salary yake ni Sh.324,260/= hadi TShs. 401,880) na Grade E (for science oriented graduates) ambayo salary yake ni TZS 408,560/= hadi TZS 505,030! Ikumbukwe, hizo ni grade za chini sana kwenye organization chat! Hivyo basi, tunaposema KCC iwe Sh.315,000/= maana yake ni kwamba Mhudumu wa ofisi alipwe Shs.315,000/=. So, ina maana viwango vingine vibaki vilevile like b4?! Jibu ni kwamba HAIWEZEKANI! Au hata kama vitabaki vilevile, hiyo mantiki ya flat rates ya 315,000/= inatoka wapi?! Jibu lake ni kwamba JF is no longer The Home of Greatest Thinkers, but The Home of Greatest as well as Shallowest Thinkers! Mimi nilinukuu maneno ya JK kwamba endapo KCC itakuwa Sh.315,000 basi bajet ya salary peke yake kwa mwaka itakuwa abt 6 Trilioni! Hesabu za Wana-JF zinaonesha JK ni muongo kv at TSh. 315,000 plus benefits zinazoenda kwenye pension funds, bajeti ya salary itakuwa haifiki hata Sh. Trilioni 2 (kwa assumption kwamba Employees 400,000 @ 315,000/=!!!!!!!!) Ama kweli, wa-TZ tuna safari ndefu! Ikiwa huyu nae anajiita Greatest Thinker, yule aliye Shallowest Thinker atakuwaje?[/FONT]
  [FONT=&quot]Yeyote anayehitaji kutoa approximation zake kuhusu bajeti ya salary itakuwaje lazima aangalie yafuatayo![/FONT]
  ·[FONT=&quot]Kuna grades ngapi za mshahara and their corresponding salary values[/FONT]
  ·[FONT=&quot]Kuna wafanyakazi wangapi kwenye kila Grade[/FONT]
  ·[FONT=&quot]From 104,000 to 315,000 ni increase for abt 200%; kuwe na increase ya % ngapi kwa kila grade iliyosalia![/FONT]
  [FONT=&quot]Ukishapata hayo majibu, ndipo unaanza kukokotoa and not as simple as taking 315,000(KCC) x 400,000(employees)x12(annual budget) and apply MAGAZIJUTO CONCEPTS!!![/FONT]
   
 2. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mbona ile thread haijafutwa kwanini usijibu pale maana hapa umeamua kureply thread kwa kuanzisha thread nyigine mods take action plz!
   
 3. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Naamini Mods wanajua kazi yao badala ya kuwatuma nini cha kufanya! anyway, nimeifanya iwe fresh ili kuwafanya wale wenye data sahihi, watuambie idadi ya salary grades and their corresponding salary values, idadi ya wafanyakazi kwenye kila grade na assumption zinazotumiwaga (% increase ya salary kwa kila grade).Likifanyika hilo, tutafahamu kwa yakini if JK lied the public or not!
   
 4. Nachingwea

  Nachingwea Senior Member

  #4
  Aug 22, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 173
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
   
 5. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
   
 6. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
   
 7. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
   
 8. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
   
 9. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu Nasdaz,
  Watu wote tunayo haki ya kujadili na kusema tunalotaka kusema ili mradi hatuvunji sheria. Tunao professional researchers wenye kazi yao ya kufanya research kama wewe unayekosoa wenzako ni qualified professional researcher tuambie tujue. Kuanza kukosoana eti kwa kuonyeshana umahiri wa kufanya mahesabu na kuwaponda wengine kwamba sio Great Thinkers hakusaidii lolote. Nyie mnaojidai mnajua kufanya utafiti na kutoa figures mnazodai ndizo sahihi [FONT=&quot][/FONT]basi tafitini mtuletee figures za matumizi yote bogus yanayofanywa na viongozi wa Serikali, na mishahara minono na posho nono zinazotolewa kwa watu wa ngazi za juu kwenye seminars na mikutano mingine ya kupikwa halafu mlinganishe na mishahara midogo inayolipwa watumishi wa ngazi za chini na makato wanayokatwa mtuambie kama kuna uhalali ama uwiano wowote wa mgawanyo wa keki ya Taifa.

  Fedha zinazokusanywa kwa njia mbalimbali kama vile kodi n.k. sio halali ya watu wachache bali ni kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote kwa ujumla waajiriwa na wasio waajiriwa wa Serikali. Kwa maana hiyo lazima uwepo uwiano wa mgawanyo wa mapato hayo ya taifa kwa manufaa ya Watanzania wote hata wale wasio kwenye formal ajira. Kinachotokea hivi sasa ni wachache kujimegea/kumegewa mapande makubwa makubwa ya keki ya Taifa wakati wananchi wengine wanaachwa solemba. Inabidi na inapaswa waajiriwa wote iwe wa Serikali ama sekta binafsi wapate kima cha mshahara kinachoweza kukidhi mahitaji yao ya lazima ya kila siku. Halikadhalika, wananchi wengine wasioajiriwa wakiwamo wakulima wawezeshwa na kuwekewa mazingira mazuri ili waweze kukuza uzalishaji wa bidhaa zao na wapunguziwe makali ya maisha kwa kupewa bure huduma muhimu za jamii kama vile elimu na afya ili na wao wanufaike na pato la taifa. Hata wale ambao wamesoma na wana taaluma zao wanastahili pia kuwekewa utaratibu wa kupewa posho za kuwawezesha kuishi wakati wanahangaika kutafuta ajira. Uwezo huo upo kama kweli Serikali inayo nia ya kutaka kuwasaidia wananchi wake. Tugawanye pato la taifa kwa uwiano unaomfaidisha kila raia wa nchi hii.

  Sasa enyi mnaojiona ni Great Thinkers kuliko wengine, kaeni chini mfanye hesabu za namna ya kugawa pato la taifa ili liweze kuwanufaisha Watanzania wote na si wachache kama ilivyo sasa.
   
Loading...