Wana JF turejee somo la upendo

Wana JF turejee somo la upendo

twijuke

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
547
Reaction score
252
Ndug zangu poleni na majukumu, nimeona tushirikishane hili la "UPENDO"

Ndugu zangu Neno Upendo ni pana, tukianza kujitathimini hapa kila mmoja kwa nafasi yake sehem kubwa wengi wetu tutakili hapa kwa nafsi zetu kuwa hatuna upendo. Hakuna kupenda kuliko kwa kweli isipokuwa pana upendo,wapo watu hawaijui misikiti wala makanisa lakini matendo yao yana aksi upendo, upendo ninao maanisha hapa si ule wa Ke na Me, namaanisha upendo wa ubinadam.

Penye upendo, pana huruma, pana uvumilivu, pana subira, pana imani,pana aman, pana msamaha. Vivyo hinyo pasipo na upendo hapana, subira, amani,amani,uvumilivu,msamaha na mabomengine mengi ukiwemo ubinafsi.

Watu wengi hatutendi wema kwa sababu yatupasa kutenda wema, bali tunatenda wema kwa kuwekaza tukisubiri malipo, kwa maana ya shukrani. Ndo maana badaye huwa tunaumia tunapo kosa malipo. Wengi wetu tumeumizwa na tumebaki na majeraha ndani ya mioyo yetu kwa kuwa tuliowatendea wema hawakuwa na mrejesho kwetu kwa wema tulio tenda kwao. hapa ndo utasikia luga za watu hawana shukrani hivyo nilisha koma kuwasaidia watu.

Kutokusamehe ni kiwango tosha cha kutokuwa chembe ya upendo ndani yetu, mwenye upendo hana kinyongo, aweza kuumia kwa maslahi ya wetu wengine. Je! waweza kuumia au kupoteza muda kwa maslahi ya mtu/watu wengine? yote haya yanatokana na neno upendo, hatuna upendo wa dhati ndani ya mioyo yetu.

Hata haya matusi tunayo yaona hapa Jf ni ushahidi tosho jinsi watu walivyo na arama Z ya upendo, mwenye upendo huheshimu kinywa chake, lakini tumeshuhudia hapa mtu aweza kutukana pasipo haya.

Mwisho kabisa ndugu zangu nawasihi tuwe na moyo wa upendo, kwa kuanza na kuwasamehe wote waliotukosea, lakini pia tuwe wepesi kuomba msamaha pale tunapojua tuliwakosea wenzetu, ndg zangu safari ya maisha ni ndefu ntafurahi kupata shuhuda hapa za watu kutangaza kusamehe, na kuanza upya. Tubebe mambo yaliyo ya maana vichwani na ndani ya mioyo yetu na si vinyongo na visirani. Naomba nimalize kwa kuwapa kisa kimoja.

Mnamo mwaka flani mke wangu alijifungua, kwenye hospital moja iliyo chini ya RC, kuna Sister mmoja alitoa msaada mkubwa kwani ilikua mke wangu ajifungue kwa upasuaji mkubwa, badala yake yule sister akashauri waongeze njia na si upasuaji mkubwa. Katika mazingira hayo nilichukua namba ya mtumishi wa Mungu yule na tuliendelea kujuliana hali.

Badaye nilipoteza simu hivyo kuna siku nikajaribu kuona kama naweza ikumbuka ile namba kichwani, hivyo nikajaribu kutuma ujumbe kwa namba niliyohisi. Niliandika hivi "Pole na majukumu ndgu, wewe ni Sister flani.....? kumbe ile namab haikuwa sahihi, ktk hali isiyo ya kawaida, nilipokea msg iliyosomeka hivi, "wewe ni mk.ndu?" nilijibu hivi " samahani ndgu nilidhani ni sister flani kwani nilipotezana naye, niwie radhi kwa usumbufu. Hata hivyo nashukuru kwa hekima na busara zako.naye akajibu hivi tena, "Samahani sana kaka unajua mimi ni mwanaume ulivyo andika sister nilidhani umenitusi, nisamehe sana kaka yaani nimejisikia vibaya. Nikamjibu hivi, "ndugu uwe na amani, kama naweza kuwasamehe wahuni iweje wewe muungwana?

Yule bwana aliamua kupiga simu na kunielekeza mahali alipo kwenye shuguli zake na akaniahidi angeenda kutubu kwani aliniambia amekosa amani na kama sitoweza kwenda basi yeye aje.

Naipenda sana Jf imenifundisha mengi na kunitoa matongotongo kwenye mboni za macho yangu, imenipanua uwigo tuwe radhi kubebeana mizigo huu ndo uungwana, kila mtu na uwezo wake wa uelewa wake na vipawa tofauti, mfundishe na kumwelekeza asiye jua, tusiwaheshimu tu tunao wajua bali hata tusio wajua maisha ni safari ndefu. Nakaribisha kama kuna mtu anaye weza kutuongoza kwa somo la upendo, karibuni tuelemishane na kukosoana.

Naitakia afya njema Jf Team work.
 
Upendo ni amri ya Bwana

Yesu alisema pendaneni
 
^^
"Kila dakika isipite pasipo mtu kusema wala kutenda mema" Shaaban Robert
^^
 
Back
Top Bottom