Wana Jamiiforums!! Karibuni Tupande Mlima Kilimanjaro

Wana Jamiiforums!! Karibuni Tupande Mlima Kilimanjaro

Mi nimepanda hills sana uku KLM, na kwa kweli lile baridi plus increasing pressure inabidi pumzi ijae tenki....
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kiwatengu usinisahau katika list ya wapandaji, nilishapanga mwaka huu kupanda huo mlima wetu.
 
Last edited by a moderator:
Yani 2014 ilivoanza tu Kilimanjaro was on my mind...i bet ts gonna be a great adventuree....it's my dream kufika hadi the top aisee...
Em tujuze japo the basics kama mazoezi hivi,kina sie ambae kwa kweli mazoezi is not part of our lives mana huko juu pressure ndo huwa inaongezeka au inapungua?
Na wale ambao mshapanda pitieni hapa mtupe ujuzi tuje cha kufanya na sie tufikee the highest point in Africa...

ya mazoezi ni muhimu sana kwa ajili ya kujijengea pumzi,
afu siyo ngumu sana kama utaamua kwa dhati..
karibu sana.
 
Tuambie pia gharama for a comfortable climb ni sh ngapi tujaze vibubu

comfortable climb, ni utumie siku nyingi kitu kitakachoweza kukugharimu..
best thing ni kuanza mazoezi mapema
ukajijengea pumzi vya kutosha.
njia ya Marangu ni laini
 
Sitathubutu tena kupanda huo mlima, now nitakuwa nauangalia kwenye picha tu, kupanda mlima Kilimanjaro si mchezo ati

acha uoga ram unaweza kabisa kuupanda na ukafika kileleni.
 
Last edited by a moderator:
Nimefurahia sana hii thread. Kusema kweli mlima Kilimanjaro ni kivutio kikubwa kupita vyote tanzania. Mimi nimebahatika kufika kileleleni kupitia marangu. Niwaeleze kwa kifupi kuhusu vituo unavyopitia kwa kuanzia mlango wa kupandia kule marangu.

kutoka marangu unaenda mandara. Km 8 kwa kawaida watu wengi hupumzika mandara na kuanza tena safari.
kutoka mandara unaenda horombo km 11 na kwa kawaida safari inakuwa ni ya mwendo wa haraka na njia ni ya mwinuko. Katika safari yangu nililala horombo. Nyumba zao za kulala ni nzuri na zina vitanda vinne kwa kila room. Na kila kituo wanatumia umeme wa solar. Hizo ni kwa zile nilizoziona mandala na horombo. Ila kuna nyumba nilizoziona zenyewe ni kubwa inawezekana zikawa na vitanda vingi zaidi.

Ukitoka horombo unaenda kibo km 9.7 hapa ndiko makutano ya barabara ya rongai na marangu. Mara nyingi safari ya kuupanda mlima huanza saa 5.30 usiku. Mimi nilipofika kibo hali ya hewa ilianza kunibadilikia kiasi cha kukata tamaa. Lakini mtaalamu wetu alitupa maelekezo ya kutosha na zaidi sana alitusisitiza kunywa maji mengi.

nilikuwa ninakunywa maji lt 4 kwa siku. Tulifika kibo saa 11 na tulikula chakula cha jioni na kushauriwa tupumzike na tutaamshwa saa 4 usiku na kwa huo MUDA tutakunywa chai au kahawa. Kusema kweli mimi sikuweza kupata usingizi.

njiani tukitoka horombo kuja kibo tulikutana na baadhi ya watu ambao hali zao kiafya hazikuwaruhusu kuendelea na safari ya kuupanda mlima na iliwalazimu kurudishwa nyuma. Kwa hiyo hiyo hali ilinifanya niwe na hofu ambayo ilinisababishia kukosa usingizi.

ilipofikia saa 5.30 tuliamshwa na tulianza maandalizi ya kuupanda mlima. Ni pamoja na kuvaa mavazi maalumu yanayohimili barafu pamoja na mvua.

ninakumbuka nilivaa suruali zaidi ya 4 na juu suruali isiyopenya mvua ,suweta 3 koti 1 la Sufi na ambalo haliruhusu mvua kupenya ndani. Gloves kwenye mikono. Kofia inayofunika kichwa hadi masikio.

tulianza safari ya kuelekea juu kwenda Giliman , na tulikula tunaenda taratibu na kulikuwa na baridi kali na barafu. Chini kulikuwa ni kweupe sababu ya barafu. Safari yangu hadi Giliman ilikuwa ya saa 8 kusema kweli nilikuwa hoi bin taabani.

baada ya kufika Giliman na kuona kibao kikinipongeza na tayari nimepanda mt 5685kutoka usawa wa bahari nilipata nguvu mpya nikajisogeza mbela kwa taabu kubwa hadi Stella point 5756mts

kwa hapa nguvu ziliniishia kabisa na hali ya hewa ilikuwa ni nzito sana oxygen ilinipungukia nikatapika maji mengi sana ila kiongozi (guide)wangu alinipa matumaini na kuniambia nisiwe na hofu kwani nguvu yangu itaongezeka. Mimi niliona kama ananitania kwa sababu hata Maji yangu ya Akita yalishaniishia kwenye chombo changu

ni kweli guide wangu alinipa Maji kidogo ya Akiba aliyobakiwa nayo na kweli yalinipa tena nguvu . Na kwa mbali kidogo niliona kilele cha mlima mrefu kupita yote afrika na kwa taratibu nilijisogeza kwa hatua mpaka nikafika uhuru peak 5895mts

ni ukweli usiopingika kuwa mlima Kilimanjaro ni Kati ya maajabu Saba ya ulimwengu.

kuupanda mlima inawezekana ila kuna changamoto. Cha msingi uwe na afya isiyokuwa na mgogoro ufanye mazoezi ya kutosha. Ushauriane na dakitari wako

u struggled mkuu Hongera.
 
kufika kileleni raha bwana...kila la heri kiongozi!!
 
Back
Top Bottom