Wana Jamiiforums!! Karibuni Tupande Mlima Kilimanjaro

Wana Jamiiforums!! Karibuni Tupande Mlima Kilimanjaro

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
19,489
Reaction score
18,380
Habari za Jioni wakuu,
Kwa wale ambao hawajawahi kuupanda Mlima Kilimanjaro, Nawashawishi sasa tuungane pamoja tuupande huu mlima.

Binafsi nitapanda siku ya ijumaa, na nimepanga kupanda mpaka kileleni kuipeperusha bendera ya
Jamiiforum, niwaambie tu! mlima kilimanjaro ni moja ya kivutio kikuu nchini Tanzania, tunavivutio vingi ila huwezi kuvifananisha na Mlima Kilimanjaro.
Get ready nitaandaa trip maalumu kwa ajili ya wanajamii walioko tayari, baada ya kipindi cha High season kuisha.

Najua humu ndani wamo wataalamu(Guiders) wanaofahamu mambo mengi sana kuhusu mlima Kilimanjaro, hapa pia tutaomba msaada wao.

Kwa wale watakao kuwa tayari, utaratibu nitautoa mwezi mmoja kabla ya safari ili kila mwenye uwezo
wa kupanda aweze kujiandaa vizuri.

Ikumbukwe kupanda kama kundi kuna unafuu mkubwa wa gharama, than to climb as individual,
Hii ni nafasi kubwa sana kwako wewe Mtanzania uliyekuwa na shauku ya kupanda mlima mrefu kuliko yote Afrika na usijue njia za kufuata.

Naomba nitoe gharama kwa ufupi,
Tozo za hifadhi ni sh. 10,000/= kama kiingilio kwa wazawa wa Afrika Mashriki..
5000/= kwa usiku mmoja kwa ajili ya malazi na sh. 2000/= kama tozo ya uokoaji.
Kwa hiyo kama ni kupanda mpaka Kileleni kwa Siku Tano Tozo yote ni sh. 72,000/=

Gharama za Maguide na mapota pamoja na mpishi ni juu yetu wenyewe.

Inawezekana kabisa.
Ni wakati wako sasa....
Mkuu Invisible umewahi kupanda mlima Kilimanjaro wewe? kama bado its your time now..
OLESAIDIMU ulisema nikukumbushe mambo yakiwa sawa, yanakaribia sasa...

NB: Nikianza tripu hiyo siku ya ijumaa nitawa update each and everything...

Karibu sana.

CC; Arushaone, marejesho, PakaJimmy & Filipo
 
Last edited by a moderator:
Ahsante sana mkuu nina ndoto za kufanya hivyo siku zijazo.
 
Hongera kaka, nikutakie safari njema kuupanda mlima. Ila haujatuambia mtazamo wako unaingilia geti gani.... La Marangu mi naona ni poa sana.
 
Hongera kaka, nikutakie safari njema kuupanda mlima. Ila haujatuambia mtazamo wako unaingilia geti gani.... La Marangu mi naona ni poa sana.

marangu gate kaka..
 
Yani 2014 ilivoanza tu Kilimanjaro was on my mind...i bet ts gonna be a great adventuree....it's my dream kufika hadi the top aisee...
Em tujuze japo the basics kama mazoezi hivi,kina sie ambae kwa kweli mazoezi is not part of our lives mana huko juu pressure ndo huwa inaongezeka au inapungua?
Na wale ambao mshapanda pitieni hapa mtupe ujuzi tuje cha kufanya na sie tufikee the highest point in Africa...
 
All the best yani.ufike hadi top..natamanijee sasa..
 
Tuambie pia gharama for a comfortable climb ni sh ngapi tujaze vibubu
 
hongera kwa uhamuzi huo,mimi nilipanda mwaka 2011 mwezi wa tisa na nilifika kileleni,cha msingi ni kutembea taratibu kwa step fupi na ukijisikia umechoka geuka nyuma taratibu vuta hewa ya nyuma maana hiyo ndo hewa ambayo umeishaizoea then anza tena kupanda taratibu.jitahidi ununue Redbull itakusaidia kuongeza nguvu.
 
Wakuu mtakaoenda all the best mi najipanga pia ili cku 1 nami nije kuupanda huo mlima
 
Sehemu ya malazi
 

Attachments

  • 1402339731896.jpg
    1402339731896.jpg
    91.6 KB · Views: 283
Kupanda mlima ni lazima upitie kwa mawakala ambao ndio watakuandalia safari, guide, hema, chakula na kubebwa kurudishwa chini endapo utapatwa na maradhi ukiwa mlimani. Kupanda mlima hadi ufike kileleni inachukuwa siku 4 na vipo vituo 3 vya kupumzikia na kulala, kupitia mlango wa Machame, kutoka mlimani inachukua siku 2 za kushuka. Kila siku wanapanda mlima watu wasiopungua 3,000.

Mlima Kilimanjaro kwa sasa ndio unaongoza kwa mapato kushinda vivutio vingine vilivyopo nchini, mara nyingi wageni wanafika kwenye milango ya kupandia mlima na wanakosa vijana wa guide, hasa kipindi hiki kinachoanza cha msimu wa utalii, kwani wageni ni wengi wengi kupita maelezo na kama umekosa guide huruhusiwi kabisa kupanda mlima.
 
Nimefurahia sana hii thread. Kusema kweli mlima Kilimanjaro ni kivutio kikubwa kupita vyote tanzania. Mimi nimebahatika kufika kileleleni kupitia marangu. Niwaeleze kwa kifupi kuhusu vituo unavyopitia kwa kuanzia mlango wa kupandia kule marangu.

kutoka marangu unaenda mandara. Km 8 kwa kawaida watu wengi hupumzika mandara na kuanza tena safari.
kutoka mandara unaenda horombo km 11 na kwa kawaida safari inakuwa ni ya mwendo wa haraka na njia ni ya mwinuko. Katika safari yangu nililala horombo. Nyumba zao za kulala ni nzuri na zina vitanda vinne kwa kila room. Na kila kituo wanatumia umeme wa solar. Hizo ni kwa zile nilizoziona mandala na horombo. Ila kuna nyumba nilizoziona zenyewe ni kubwa inawezekana zikawa na vitanda vingi zaidi.

Ukitoka horombo unaenda kibo km 9.7 hapa ndiko makutano ya barabara ya rongai na marangu. Mara nyingi safari ya kuupanda mlima huanza saa 5.30 usiku. Mimi nilipofika kibo hali ya hewa ilianza kunibadilikia kiasi cha kukata tamaa. Lakini mtaalamu wetu alitupa maelekezo ya kutosha na zaidi sana alitusisitiza kunywa maji mengi.

nilikuwa ninakunywa maji lt 4 kwa siku. Tulifika kibo saa 11 na tulikula chakula cha jioni na kushauriwa tupumzike na tutaamshwa saa 4 usiku na kwa huo MUDA tutakunywa chai au kahawa. Kusema kweli mimi sikuweza kupata usingizi.

njiani tukitoka horombo kuja kibo tulikutana na baadhi ya watu ambao hali zao kiafya hazikuwaruhusu kuendelea na safari ya kuupanda mlima na iliwalazimu kurudishwa nyuma. Kwa hiyo hiyo hali ilinifanya niwe na hofu ambayo ilinisababishia kukosa usingizi.

ilipofikia saa 5.30 tuliamshwa na tulianza maandalizi ya kuupanda mlima. Ni pamoja na kuvaa mavazi maalumu yanayohimili barafu pamoja na mvua.

ninakumbuka nilivaa suruali zaidi ya 4 na juu suruali isiyopenya mvua ,suweta 3 koti 1 la Sufi na ambalo haliruhusu mvua kupenya ndani. Gloves kwenye mikono. Kofia inayofunika kichwa hadi masikio.

tulianza safari ya kuelekea juu kwenda Giliman , na tulikula tunaenda taratibu na kulikuwa na baridi kali na barafu. Chini kulikuwa ni kweupe sababu ya barafu. Safari yangu hadi Giliman ilikuwa ya saa 8 kusema kweli nilikuwa hoi bin taabani.

baada ya kufika Giliman na kuona kibao kikinipongeza na tayari nimepanda mt 5685kutoka usawa wa bahari nilipata nguvu mpya nikajisogeza mbela kwa taabu kubwa hadi Stella point 5756mts

kwa hapa nguvu ziliniishia kabisa na hali ya hewa ilikuwa ni nzito sana oxygen ilinipungukia nikatapika maji mengi sana ila kiongozi (guide)wangu alinipa matumaini na kuniambia nisiwe na hofu kwani nguvu yangu itaongezeka. Mimi niliona kama ananitania kwa sababu hata Maji yangu ya Akita yalishaniishia kwenye chombo changu

ni kweli guide wangu alinipa Maji kidogo ya Akiba aliyobakiwa nayo na kweli yalinipa tena nguvu . Na kwa mbali kidogo niliona kilele cha mlima mrefu kupita yote afrika na kwa taratibu nilijisogeza kwa hatua mpaka nikafika uhuru peak 5895mts

ni ukweli usiopingika kuwa mlima Kilimanjaro ni Kati ya maajabu Saba ya ulimwengu.

kuupanda mlima inawezekana ila kuna changamoto. Cha msingi uwe na afya isiyokuwa na mgogoro ufanye mazoezi ya kutosha. Ushauriane na dakitari wako
 
Sitathubutu tena kupanda huo mlima, now nitakuwa nauangalia kwenye picha tu, kupanda mlima Kilimanjaro si mchezo ati
 
Back
Top Bottom